Waraka wa Shigongo kwa Ze Original Komedi

Waraka wa Shigongo kwa Ze Original Komedi

UKWELI KUHUSU SEKI

Kwanza si yatima, mama na baba yake wapo Ifakara na wapo hai. Ndugu zake ni hawa
Wiliuma Ndeketela (Mafinga) Edwin Ndeketela (Dar) Denis Ndeketela (Dar) Edah Ndeketela (Ifakara), Doris (UDSM), Prisca (Dar).

Ninayeandika hapa, mama yake na Seki ni mama yangu mkubwa toka nitoke na mama
yangu.

Si yatima (Seki) baba yake anaitwa David Ndeketela (72), na mama yake anaitwa Elizabeth Zacharia. Wako hai.

Hivi Shigongo anajua maana ya neo yatima?

Kwanza hao vijana kazi yao ni kuigiza, walikutaja moja kwa moja? Au unajihisi? Huu ni unafiki mkubwa sana.

Kaka yangu Seki si yatima, umeniudhi sana Shigongo
 
Nadhani Shigongo hajakosea , pia mwana kapatia kuitia humu hii habari. JF ni jukwaa zuri la mawazo na uchambuzi.

Ukitazama mtiririko wa Shigongo wa watu mashuhuri waliododa haupingiki, hivyo bila kujali moral authority ya mtoa mada ni kweli hawa vijana wa orijino komedi wamelewa sifa na wanadhani wako juu ya jamii.

Hawana adabu,sio wachambuzi na wanaongozwa na maslahi binafsi zaidi ya hali ya halisi.
Tuwape muda kidogo kwani nijuavyo mimi rafiki wa kweli wa FISADI ni maslahi sio vinginevyo, wakishatimiza lengo walilonunuliwa umuhimu wao utapungua and they will become redundant
 
Unajua kwenye kutafuta maisha sioni kosa la ze comedy kumwagilia mbali mengi na EATV yake..hapo kinacho matter ni MASLAHI...fulll stop.

Wewe unaposema wanamkashifu Mengi..Je Lowassa alipokuwa waziri mkuu?...je Pinda walivyo mkashifu hajui kuvaa?...sembuse Mengi??...kwani Mengi ni nani?....tusichukulie Mengi anachafuliwa au anakashifiwa na zecomedy kwakuwa eti..waliondoka kwake na ionekane ni beef..ichukuliwe kama wanavyowakashifu wengine na kuwadhalilisha kina pinda...

Kuhusu Shigongo na ushauri wake..mie naona yeye tu amekuwa mpuuzi kuweka ushauri uliojaa kashfa kwenye gazeti na kuwashauri watu specific...kama ze comedy..angekuwa smart ANGETOA USHAURI KWA VIJANA WOTE WA TANZANIA WALIO MAARUFU NA WANAOCHIPUKIA...ndiooo....mbona yeye shigongo asimshauri Ray na mwenzake yule wa kike nani yuleeeee Johari ...maana ni maarufu kama Ze Comedy tu...wacheza sinema wake hawashauri kwenye magazeti bali wengine anawashauri kwa kashfa kwenye magazeti...

Hapa braza Shigongo sikuungi mkono...maana unapiga madongo mafanikio ya vijana kuwa wanamiliki harrier wanaona wamefika...kwa hiyo unataka kusema vijana hawajui yapo magari mengine ya kifahari?...wao mwisho wao wa kujua ni hicho ki-harrier cha Masanja?..hii ni kashfa kaka...uyatima wa Seki unahusu nini zaidi ya kumkashifu na kumkejeli?...huoni aibu kumwita mtu yatima ilihali ni mipango ya Mungu kutokuwa na wazazi?..na ujuwe kiasi cha kujuwa kuwa u-yatima kwa mtu kama Seki anayejitegemea na kuendesha maisha yake sio hoja ya msingi kabisaa....weka hoja juu ya hoja..na hoja hujibiwa kwa hoja

Wamemwigiza mfanyabiashara mwenzako aliyefilisika....ok...kwanini kama wewe ni rafiki yake usimwinue na unamwacha anahangaika chini??...naona kama vijana walikushika pazuri...tenda wema kwa mwenzako aliyeanguka na usitoe matents Mbagala wakati mashaka matongo anakufa njaa mikononi mwako....KAKA SABUNI IKICHAFUKA ITASAFISHWA NA NINI???..ndiooo..wewe naona ni sabuni chafu..tukusafishe na nini? i guess ZE COMEDY wamekuletea sabuni ya kujisafisha.....

Hitimisho...nakushauri uache hii approach yako ya kushauri watu kwa magazeti...kwani mdogo wako nyumbani au mwanao huwa ukimshauri unamwandikia gazeti asome au unamwita mnaongea???...mbona tumaini dudubaya ulimwita mkaongea na kumshauri?..kwann hukumwandika gazetini?...au tuendelee kuhisi kuwa ze comedy wamakataa kuingia tollywood na kucheza senema zako?....angalia tunakuwa suspicious na ambitionz zako kuwacontroll wasanii wazuri wote wa tv....punguza kiu ya pesa..DUNIA TUNAPITA.... We Dare To Talk Openly

Achana na kuwaandika watoto kwa majina...sasa unataka tusome nini kuhusu seki toleo lijalo??....kwamba ni yatima?..au kashfa juu ya kashfa za zecomedy?...MKUBWA SASA KAKA ACHANA NA HAWA WATOTO..ASIYEFUNZWA NA MAMAYE HUFUNZWA NA ULIMWENGU...WAACHE DUNIA INAWASUBIRI KUWAFUNZA NA ULIMWENGU NDIO MAMA
 
Sasa kama sekioni ni yatima tatizo ni nini ? Sekioni alikuwa anaishi kimara baruti na hakuwahi kulelewa na reginald mengi kama shigongo anavyotaka tuamini

Tatizo la watanzania ukiwapo na wewe hampendi kusoma vitu na kutakari. Acha uvivu soma uelewe. Maana ya kulelewa ni kukaa kwa mtu?
 
Hapo ndipo point ilipo, kwamba kumbe mabaya 'aliyonayo' Shigongo hayazuii kuwakosoa Original Comedy !! Basi kwa mwandiko huo uko ukurasa mmoja na Shigongo, jambo ambalo ndo linatakiwa.

Unapokosoa kwa kuingiza sumu inapoteza kabisa point zako. na hasa ukizingatia unayoyapigia kelele wewe au ndugu yako anayafanya na hujanyoosha kidole kukemea. HUO NI UNAFIKI, UZANDIKI, UKUWADI NA UPUUZI wa daraja la juu sana.
 
kwa kuwa Shigongo kakosea na inatazamwa kama hana maadili hata kushauri basi ZE COMEDY ORIJINO waendelee na tabia hiyo ya kuwacheka watu walioanguka.

Ndiyo ni tabia yao. Ni tabia yao kuanzia EATV walipomsakama Mr Nice, wakaja kwa wengine hata Mpakanjia,masahaka na hivi karibuni mwanamuziki mgonjwa.

Ze comedy endeleeni kuifundisha jamii kuwa kumcheka aliyeanguka au aliyetaabani kutokana na masahibu yaliyomkuta ni jambo JEMA SANA.

Endeleeni kuinyea mikono mliyopitia kinyesi chote. Msisaze. Ifundisheni jamii hili nalo ni jema.

Ze comedy mdumu Shigongo zii.

Laiti ningejua umri wako ningeweza kukujibu au kusoma lolote kuhusu uliyoandika. Naogopa kutwanga maji
 
UKWELI KUHUSU SEKI

Kwanza si yatima, mama na baba yake wapo Ifakara na wapo hai. Ndugu zake ni hawa
Wiliuma Ndeketela (Mafinga) Edwin Ndeketela (Dar) Denis Ndeketela (Dar) Edah Ndeketela (Ifakara), Doris (UDSM), Prisca (Dar).

Ninayeandika hapa, mama yake na Seki ni mama yangu mkubwa toka nitoke na mama
yangu.

Si yatima (Seki) baba yake anaitwa David Ndeketela (72), na mama yake anaitwa Elizabeth Zacharia. Wako hai.

Hivi Shigongo anajua maana ya neo yatima?

Kwanza hao vijana kazi yao ni kuigiza, walikutaja moja kwa moja? Au unajihisi? Huu ni unafiki mkubwa sana.

Kaka yangu Seki si yatima, umeniudhi sana Shigongo

Maneno hayo!!!!!......!
 
unajua nini,SHIGONGO IS DYING TRYING!tumwacheni hivyo hivyo.
 
Ok hapa ni kwamba
tope limechafua vumbi...
kazi kweli kweli
 
wiki ijayo nitamwongelea sekioni david, yatima aliyesaidiwa na reginald mengi ambaye hivi sasa kila kukicha anamtukana mzee huyo sababu leo hii anafadhiliwa na yusuph manji.

alisaidiwaje wakati alikuwaakifanya kazi kwa uwezo wake na kulipwa kwa kazi yake?

Shigongo huna maana
 
Dear all,

I am in London, for a special mission, but have been irked by this debate and I would like to give my contribution without abusing. First of all let me remind our contributors that 'If all of will decide to use abusive language, this forum won't be the home of great thinkers but the heaven of puppets.

These guys are not rich let alone being celebs. When Eric is talking about Magari ya Kifahari, I don't understand him. Toyota Chaser or GX100 0R 110 used from Japan is not a posh car or Porsche. In Bongo, we have given people the power and title they don't even deserve.

In Dar, where 80percent of vehicles cruising on the roads are used and reconditioned from Japan and Dubai, we have created non-existing millionaires.

In Dar I have there are not more than 10 Posh cars.( Porsche Cayenne four wheels drive 2, Sports Mercedes Benz 4-Masha, Mkono, and Others, Pirrali owned by Tanil Somaiya anyway kwa shingo Upande there are also dozens of Vogues).

The Problem is we tend to say thing without doing a research. Magari ya Kifahari Kwa Komedi? Noway.

My friend have you DONE a research as you are CLAIMING? hivi magari ya kifahari yana KIPIMO CHAKE???

Naombwa kueleweshwa hapa ni magri gani ya kiahari na yasiyokuwa? ni standard gani inatumika? KUULIZA SIO KUPINGA jamani nielewesheni mwenzenu maana huku kwetu kwetu kijijini tuna mpaka baiskeli za kifahari, kweli tena sasa kama inatumia injini na kijiji kizima anayo huyu mwenyekiti peke yake na hakuna mwenye ndoto ya kuwa nayo kwa kuzingatia hali zetu si basi tu tunaona ni ya KIFAHARI?
 
Kwa inavyo onekana hapa kuna makundi mawili:

1.Wanao kubaliana na Shigongo alicho kifanya
2.Wasio kubaliana na Shigongo alicho kifanya

Binafsi sikatai kwamba mambo aliyo yaandika Shigongo baadhi yana ukweli. Ni kweli wana takiwa kuwekeza hela wanazo pata sasa kwa manufaa ya baadae. Ni kweli wameanza kulewa umaarufu. Ni kweli siyo jambo jema kukashfu watu hata kama ni utani kuna utani uliozidi mpaka kwa mfano kitendo chao cha kumsanifu Abiola. Ni kweli siku hizi wanalewa sifa nk.

LAKINI, pamoja na mapungufu ya ze komedi ilikuwa sahihi kwa Shigongo kuandika alicho andika kwa umma? Kwa nini asinge wapa ushauri wakiwa wenyewe aidha kwa kuwa pigia simu?(maana waandishi wake wana kila number ya supastaa)? Kwa nini aende hadharani?

Kuna pia wanaodai kuwa hata kama Shigongo hana moral authority ya kuwasema lakini kasema ukweli. Jamani does that make sense? Useme hata kama hana moral authority ya kuwasema awaseme tu? Leo fisadi aki simama jukwani aseme msiibe mta kaa mum sikilize kweli? Kwa yoyte ambaye ameona magazeti ya huyu mkuu inabidi ajiulize kwanza yeye hajajiona? Hayo magazeti yake haya kashfu au kudhalilisha watu? Your can't accuse someone of doing the same thing you are doing even if you are doing it in a different way. Sasa ze komedi jirekebisheni kutusi watu lakini ukiangalia magazeti na yeye Shigongo ana fanya hivyo hivyo tofauti ni kwamba ze komedi wana fanya kwa kutumia t.v. yeye kwa kutumia magazeti.

What is being questioned is not the integrity of Shigongo's message what is being questioned is Shigongo's on integrity & the purpose of making his advise public wakati huo huo akidai hatafuti umaarufu.

See it as you may lakini hapa ni mamba kumsema chatu.
 
UKWELI KUHUSU SEKI

Kwanza si yatima, mama na baba yake wapo Ifakara na wapo hai. Ndugu zake ni hawa
Wiliuma Ndeketela (Mafinga) Edwin Ndeketela (Dar) Denis Ndeketela (Dar) Edah Ndeketela (Ifakara), Doris (UDSM), Prisca (Dar).

Ninayeandika hapa, mama yake na Seki ni mama yangu mkubwa toka nitoke na mama
yangu.

Si yatima (Seki) baba yake anaitwa David Ndeketela (72), na mama yake anaitwa Elizabeth Zacharia. Wako hai.

Hivi Shigongo anajua maana ya neo yatima?

Kwanza hao vijana kazi yao ni kuigiza, walikutaja moja kwa moja? Au unajihisi? Huu ni unafiki mkubwa sana.

Kaka yangu Seki si yatima, umeniudhi sana Shigongo
KAMA KWELI SEKI SI YATIMA BASI HUYU SHIGONGO AMEFANYA KOSA KUBWA SANA.
............ ANGALIENI MSITUANZISHIE MOVIE NYINGINE WAKATI HATUJAMALIZA MENGI V/s ROSTAM, MWEE!!!!
 
Binafsi sikatai kwamba mambo aliyo yaandika Shigongo baadhi yana ukweli. Ni kweli wana takiwa kuwekeza hela wanazo pata sasa kwa manufaa ya baadae. Ni kweli wameanza kulewa umaarufu. Ni kweli siyo jambo jema kukashfu watu hata kama ni utani kuna utani uliozidi mpaka kwa mfano kitendo chao cha kumsanifu Abiola. .

WANATAKIWA KUWEKEZA SAWA!lakin je,wanashauriwa kuwekeza BAADA YA KUMCHANA LAIVU ABIOLA?kama shigongo ni mzuri kiasi hicho,basi angewashauri kuwekeza MAPEMA SANA!tangu wakiwa EATV,tangu wakimuiga LOWASSA,KEPTEN KOMBA,n.k.kinachonishangaza ni ushauri kuja baada ya KUMSHIKA PABAYA ABIOLA(ambaye ni professional-mate wa ERICK)...............udhaifu mkubwa huo shigongo,unaonyesha hasira zako HADHARANI,KISILANI,MTIMA NYONGO n.k na nilidhan rafikiyo abiola ANGEKUWA WAKWANZA KUSHAURIWA KUWEKEZA.pia usitumie majigambo ya kumnusuru dudu ILI UOGOPWE!angeweza kuwa yoyote tu.

MTIZAMO WANGU:komedi originale walikuwa wanajaribu kutuonyesha namna RAFIKI WA KWELI NA ASIYE WA KWELI WALIVYO.mlokole shigongo ASINGEKUWA TAYARI KUONA ABIOLA YUPO KWENYE HIYO HALI (kama kweli ni jamaa yake)

kimsingi i don't find anything SO SPECIAL kwenye hiyo waraka,zaidi ya VISILANI!

waache komedi wale BATA baba shigongo
 
Umesema kweli. Kama kweli Abiola ni swahiba wake kiasi hicho kwa nini asim saidie kwa hali na mali? Ange muacha awekatika hali hiyo? Huyu jamaa kaona chance ya public relations kujionyesha kwa jamii ndiyo kaitumia. Ze Komedi wame watania watu wangapi hajasema? Mbona ni wengi tu ze komedi wamewa kashfu na japo sisupport kumkashfu mtu yoyote kwa nini aji tokezeleo?Siku zote haoni wanacho fanya? Kaona hao wengine angesema angeonekana anaji komba sasa safari hii ana tumia gia ya "urafiki" na ndugu Abiola kujidai imem touch personally.

SITETEI MAKOSA YA ZE KOMEDI LAKINI SIKUBALIANI NA SHIGONGO. SIKU ZOTE ALIKUA WAPI WAKI PONDWA WENGINE? NI YALE YALE YA ZEUTAMU. WALICHAFULIWA WENGI IKA LALAMIKIWA WEE LAKINI HAKIKU FANYIKA KITU MPAKA WALIPO MDHALILISHA BOSI WAO.
 
Kweli hawa vijana wamekosa adabu. waraka huu ni funzo kwa kila mmoja wetu, tupo makazini kuna siku tutatoka na kustaafu kufukuzwa etc na tutakumbuka makosa tuliyoyafanya nyuma kutojiandaa na maisha ya uzee. Hawa bado ni vijana na umaarufu wao unashuka si kama walivyoanza. siku hizi hakuna anayekatiza shughuli zake kuwahi ze komedi. Hiyo ni ishara tosha kuwa wnakwenda mwisho, na vimenza kuchosha watu. they are going out of fashion

huyo mhaya awaeleze wenzake: WAHAYA WANASEMA "ENTASIMA EKALYA OMUTIMA GWEMANZI" MENGI AMESAIDIA KUWAWEKA WALIPO.

Na TBC1 wajue siku wakiwatema watawatukana hivyo hivyo kama wanavyofanya kwa Mengi.
 
Shigongo huna jipya wivu unakusumbua mlokole wewe umeona jamaa sasa mambo mswano kuliko walivyo kuwa EAT umeshaanza kuweka unoko wako kama kawaida yako...
 
Shigongo huna jipya wivu unakusumbua mlokole wewe umeona jamaa sasa mambo mswano kuliko walivyo kuwa EAT umeshaanza kuweka unoko wako kama kawaida yako...

Wala si wivu. alichowambia vijana hawa ni sahihi kabisa, vijana wana lewa sifa na pesa za mafisadi, sasa wamegeuka kuwa safisha mafisadi?

Kila mtanzania mzalendo anaye ipenda nchi yake hawezi kufurahia kundi la namna hii!

Shigongo wafunde labda wanaweza kukusikia.
 
Back
Top Bottom