Elections 2010 Waraka wa Waislam Kuhusu Uchaguzi Wakamilika

ila kama hawa waislam walikuwa wanaupinga waraka katoliki wao wanasababu gani kutoa nao waraka, kazi sana

SIMPLY BECAUSE...............If you cant beat them, join them!!!!!!!
 

Kwani comments za Serikali zinakuwaje?
 

Kwani comments za Serikali zinakuwaje au zinasemwa na nani?
 
acha nyaraka zitolewe jamani..nawasihi na wasabato nanyi mtoe wenu..si wananchi tuna elimishwa kuhusu kuwapigia kura viongozi waadirifu?..acheni kuwazuia vyombo vya kidini kutoa elimu hii muhimu..
sema ndugu zangu waislam kwenye nyaraka zenu ni muhimu mkawashirikisha walioenda shule..maana karibia kila sheikh pale nkiangalia kwa haraka haraka naona ni darasa la 7 tu..samahani sina nia ya kuwatukana ila huo ndiyo ukweli..maana mufti nae si darasa la 7 tu yule..
ukinuna kanusha kwa kutoa cv zao hapa..sio kubisha ka mwendawazimu..
ule wa wakatoliki nimeona cv za jamaa zimetulia..elimu ya dunia na ya dini..
sasa wa waislam isije ikawa waliosomea alifu be te see tu...
 
Kama hii ni njia mojawapo ya kutoa elimu ya uraia kwa wananchi, basi ni jambo jema sana kwani kuna raia wengi wanaoamini maneno ya viongozi wao wa dini kuliko mtu yeyote yule. Ni imani yangu kuwa waraka huo hautachanganya mambo ya dini na mambo ya uraia wa kawaida, yaani waraka uwe kama ulitolewa na wakatoliki ambao kimsingi unaweza kusomwa na mtu wa dini yeyote ile. Itakuwa si jambo jema endapo waraka huo utaegemea upande wa kidini au utajitokeza kama vile ni ushindani dhidi ya ule waraka wa wakatoliki.
 

Nadhani kitu muhimu siyo kuzindua waraka. Ilitakiwa tu tuone ama kuunga mkono waraka wa Wakatoliki, kuuboresha ama kuupuuza. Lakini sasa ninachoona ni kama mashindano. Kitu ambacho ni 'offpoint'.

Jana nilipita Kariakoo na pale wanaposubiria magari ya kwenda Mbagala kama kawaida jioni huwa kuna mjadala dhidi ya Ukristo au Kanisa Katoliki. Niliukuta na kwa kawaida unapata washabiki wengi hasa wenye vibandiko. Kitu nilichosikia ni pamoja na kwamba Ukristo unapendelewa hapa Tz kuliko Uislamu: Balazi wa Vatican, tax free, upendeleo wa ajira etc.

Watoa mada wakawa wanasema kwenye Uislamu wanafundishwa "Kama mtu hakunyanyasi na wewe usimnyanyase. Lakini akikunyanyasa na wewe inabidi umnyanyase kwa njia yoyote ile hata kama ni ya kumwaga damu. Na haya ni mafundisho ya Qur'an siyo jambo la hiari ya mtu."

Niliposikia hivyo, nikasema naogopa sana msimamo wa namna hiyo na dini kama hiyo naiogopa kama ukoma. Wakasema habari ndiyo hiyo! Halafu alipita mwumini mmoja amevaa kanzu nyeupe na amefuga ndevu ndefu sana na akasema: "hayo mnayoonge subirini Ijumaa. Kuna waraka mchungu sana unakuja!" Na mwingine akadokeza: "Sisi tunahamasishana kutomchagua kafir yeyote..." Niliona kama huo mjadala haunifai, nikajiondokea zangu!
 
serikali inakimbia kinvuli chake,kweli uchaguzi ujao utakuwa wa ukweli zaidi. kila mtu atoe mwingozo lengo ni moja kupata watu waadilifu katika uongozi wa nchi, na mabudha na wahindu nao tusijeshangaa wametoa wa kwao.!


katoliki wanazo 2 at per sasa sijui unaongelea upi kati ya hizo 2
 
Jamani ni jioni sasa na huo waraka ilikuwa utoke mchana .Hakuna mwenye nao auweke hapa ndugu zangu waislam wenzetu ?
 
Mambo ya dini kuchanganywa na mambo ya kiserikali sio mambo ya mzaha. President should act NOW! Ni kichekesho kuona rais katika yale mazishi ya Askofu Mayalla anapewa lecture na Cardinal Pengo.

Tumefika vipi hapa?!!!!!!!

[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif][SIZE=+1]Of all the tyrannies that afflict mankind, tyranny in religion is the worst. Every other species of tyranny is limited to the world we live in, but this attempts a stride beyond the grave and seeks to pursue us into eternity.
[SIZE=-1] -- Thomas Paine, as quoted by Joseph Lewis in Inspiration and Wisdom from the Writings of Thomas Paine[/SIZE][/SIZE][/FONT]
 

Yaani wewe unaona ni kichekesho?!
Acha vituko bwana!
 
MIMI NADHANI HAYA YA KUTOA WARAKA YATAJAKUWA kama ni kitu cha kawaida na mazoea tu, cha muhimu nkama hawa watu nwa dini wapo serious inatakiwa KUWATENGA HAWA JAMAA KABISA,
KAMA WAKATOLIKI WAMEWEZA KUMTENGA FR NKWERA, FR KARUGENDO NA mapadre wengine inashindikana nini kumtenga MTU KAMA CHENGE AU EL
 
Jamani kuna mtu ana copy tuanze kuusoma kabla wachambuaji hawajatufanya tuwe biased.
 


Mkuu ulitaka JK pale msibani afanye nini ? Yeye alienda nyumbani kwa watu hata kama ni rais.Alialikwa angaliweza angalikataa kwenda .Hakuwa lectured alikuwa anatolea utanda machoni .Hana analoweza kufanya .Unamata a act ? Yeah kwel bora ku act now wa kuwakamata wala rusha wanao pelekea Tiafa kugawanyika kwa matendo yake JK na NEC yake na washikaji wake wanao liibia taifa langu .
 

Kila mtu ana kiasi flani cha uhuru wa kuamua nini ni cha muhimu na nini chakufanya. Wao wanendesha mashule, wanaendesha mahospitali, etc. na sasa wameona ni vyema kutoa waraka.

Wewe umeutumiaje huo uhuru wako? Labda wewe sasa ndio zamu yako kutoa waraka wa kilimo bora.


Tunajua, ila kwani kuna ubaya gani kukumbushana? Nini kinakukera kwa hili?

Mtu mwenye njaa atachukua pesa kutoka kwa fisadi hata akijua kufanya hivyo ni vibaya.

Kwa hiyo ni vyema watu wachague wezi?


Kwa hiyo tukiendelea kuchagua wezi na kufanya hayo unayosema ndio tutatatua matatizo yote?
 
Jamani kuna mtu ana copy tuanze kuusoma kabla wachambuaji hawajatufanya tuwe biased.

Huo waraka Magezi alishauweka hapa.

Hata hivyo, ingekuwa gazeti la maana lingesema kuna nini kwenye waraka hasa hasa kinachosababisha sokomoko. Huwezi kuandika tu reaction za Kingunge na Mashehe na Wadau bila kusema action yenyewe ni nini.

Habari bongo fyongo mno. Ukisoma hilo gazeti huwezi elewa Waislam wanaripotiwa kwamba wanalipiza walichofanya Wakatoliki, au huu ni mpango wao wa toka awali:

Sijui kimesemwa nini hapo. Sasa ukichanganya na mavurundo ya wasemaji wetu kinachotoka hapo ni sumu ya panya. Philip Marmo walivyomripoti huwezi jua reaction yake juu ya Waraka wa Wakatoliki ni nini.

Sioni Waziri aliposema - kama gazeti lilivyomsemea bila nukuu- kwamba Waraka wa Katoliki umesabisha malumbano, ni mbaya. Sijui kasema au hakusema. Msimamo wa serikali unabaki uko hewani hewani, baadhi yetu wananchi hatuelewi kinachoendelea, kila tafsiri na uhoro tunaosoma magazetini cha mbele, Kikwete nchi inamuelemea, solutions zake za kwenye vikao vya chama zina backfire, vipeperushi vimesambaa mpaka UN, watoto wanakufa mabwenini kwa mishumaa, wasafiri wanauawa na majambazi, na madereva wanaolisha rushwa mapolisi, mishahara ya Wakubwa inaongezwa, maskini wanazidi kuwa kapuku, vurugu tupu. Hiyo 2015 ije haraka aende zake Mkuranga au akapewe season tickets na Hashimu kabla hajatuletea machafuko na mtandao wake.
 
Last edited:
kesho watakuja walutheri, kisha wasababato, kisha waanglican na walokole n.k

lazima nchi ichukue hatua kinyume chake itakuwa balaa



Kanisa lilisema tusipoingilia kati,serikali inayotetea fisadis baadaye itatetea homosexuals!

Sasa kazi na sijui kama jeshi na polis litaweza kuingilia na kutisha kama wafanyavyo Pemba.
 
Mtakuja kuniambia tu, hizi nyaraka ndo kiama cha mafisadi na ccm yao, ni lazima wazihofie tu!
 
 

Wewe unayataka mwenyewe hayo, hii si mara ya kwanza kutuletea simulizi za kituo cha mabasi ya kwenda Mbagala na matusi ya dini. As long as ushawajua na unaiogopa hiyo dini why bother kusikiliza mashambulizi hayo time and again?
 
Serikali inaposhindwa kazi matokeo yake ndio hayo.Wanachi wamepiga kelele weee lakini Serikali inapuuza .Laiti serikali ingekuwa inafanya kazi zake kwa umakini mambo ya waraka yasingekuwepo.Muda si mrefu tutaanza kuambiwa nao wapagani nao wanaanda waraka wao au wanyakyusa au wamasai nao wanaandaa nyaraka zao.Yote hayo kiini chake ni viongozi wetu wabovu,akina Kingunge na wenzake akina Makamba msitupigie kelele mumeshindwa kuonyesha njia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…