Elections 2010 Waraka wa Waislam Kuhusu Uchaguzi Wakamilika

Elections 2010 Waraka wa Waislam Kuhusu Uchaguzi Wakamilika

Inakuaje ule waraka wa mwanzo ukaitwa wa Wakatoliki na huu wa sasa tunakimbilia kuuita wa Waislamu?.

Inamaana kuna asasi inayowaunganisha waislamu wote wa Tanzania imeubariki waraka huo ama ndio mazoea yaleyale ya kuwa wepesi kukimbilia, waislamu hivi, waislamu vile na tukija kwa wakristo tunaheshimu utafauti wao?

Shura ya Maimamu na Muungano wa Taasisi za Jumuiya za Kiislamu ni makundi tu ya waislamu na sio ndio waislamu. Na hivyo unapswa kutambulika kama waraka wa Shura ya Maimamu na Muungano wa Jumuiya za Kiisalamu na sio vinginevyo.

Kesho tutasikia waislamu wamefanya hivi mkiristo, waislamu wamemfranya vile mpagani, waislamu wamefanya haya....mambo ambayo tayari yamekuwa yakiendelea katika jamii yetu na tunaona ni ya kawaida.....

Ukivunja MISINGI uwe tayari MISINGI kukuvunja wewe....

omarilyas
 
Huo waraka umeandikwa na nani ? Na mashekhe wote hawa wamekuja kwenye ufunguzi ama ndiyo wamekuja kuweka mawazo pamoja ? Kuiga kubaya huku na kusema sema nako kuna matatizo .Wacha tuangalie mwelekeo
 
Jamani tuweni makini sana ndugu zangu tukiungana na kutoa msimamo mmoja ili tupate dawa ya kupambana na hawa mafisadi kwani sasa tumechoka jamani tusiwape nafasi mafisdi.
 
Hivi ilani, waraka na mwongozo ni kitu kimoja??

Nijuavyo mimi waraka na mwongozo wa hawa wana dini ni kuwaelimisha wananchi namna ya kupata viongozi bora wakati ilani inalenga waambia wananchi nini wategemee kutoka kwa chama iwapo watakipa mamlaka ya kuongoza nchi.

They are all directives in which the sole purpose it to provide guidance/guideline!
 
Inakuaje ule waraka wa mwanzo ukaitwa wa Wakatoliki na huu wa sasa tunakimbilia kuuita wa Waislamu?.

Ukivunja MISINGI uwe tayari MISINGI kukuvunja wewe....

omarilyas

Omar,

Shukrani kwa kutusahihisha. Tumekimbuilia kusema ni waraka wa Waislamu na si kikundi fulani cha Waislamu, kama ilivyokuwa Waraka wa Wakatoliki ambao haukuwa ni uwakilishi kamili wa Wakristo wote hata kama kuna mambo ambayo kila mtu bila kujali dini anaweza kuwa anakubaliana nayo.
 
Usichokijuwa kuwa kuna tofauti ya uislamu, wako waislamu wa siasa kali , wapo waislamu kanzu , wapo waislamu jina na tabaka nyingi nyingi hivyo huu wingi wao katika nafasi za uongozi hakuna maana yoyote.
tehtehtehtehtehtehtehtehtehteh.
Wewe uko katika kundi gani?
I guess lako ni wale waislamu kanzu! Nimekosea?😀
 
Ye yote mwenye kutaka kutoa waraka wake atoe, nasi tutauhukumu waraka kwa yaliyomo yake.
 
Bakwata siku zote hawataipinga Serikali kwenye lolote lile, imekuwa kama kitengo cha CCM. Wao ufisadi uliokithiri na unaopigiwa kelele ndani ya CCM na Serikali wala hawaoni kabisa! Hawa Bakwata nao ni mafisadi tu.

Halafu ndio tunataka serikali ituanzishie Mahakama ya Kadhi ili itudhibiti!
 
SERIKALI imewatahadharisha Waislamu kuhusu mpango wao wa kutoa mwongozo wa uchaguzi kwa waumini wake, ikisema kuna haja ya kutafakari kwanza ili kuona kama kuna ulazima wa kufanya hivyo au la.

Kauli hiyo imekuja huku Shura ya Imamu wa Tanzania, ikikusudia kutangaza mwongozo wake kwa waumini wa madhehebu ya Kiislamu katika uzinduzi utakaofanyika leo Kinondoni jijini Dar es Salaam

Tahadhari hiyo kwa Waislamu, ilitolewa jana na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Philipo Marmo, ambaye kabla ya kutoa waraka huo, ni vyema kwanza Waislamu wakapima athari zake kwa jamii ya Watanzania.

Alisema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, baada ya kufungua mkutano wa kujiandaa na mvua za Elnino.

“Miongozo ya mwaka huu imeleta malumbano makubwa, kwa hiyo viongozi wa dini wapime athari na manufaa kwa nchi na kwa waumini wao na si kuleta mtafaruku kwenye jamii,” alisema Marmo na kuongeza:

“Wote tunapenda nchi isiathirike na malumbano maana jamii ikianza kusambaratika wote tutaathirika si Wakatoliki au Waislamu ,”alisema Marmo.

Hata hivyo Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), limesema halina taarifa yeyote kuhusiana na uzinduzi wa mwongozo wa pamoja Waislaam kuelekea katika uchaguzi mkuu wa 2010 na zinduzi wa moto wa siasa za ukombozi , utakaofanyika leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=14173
 
Wana JF,
Waraka wa Waislamu kuhusu Uchaguzi wa 2010 ndio umeshafika je huu ni majibizano ya makundi ya kidini kama ya "MIPASHO" baada ya ule wa Wakatoliki au ndio haki ya kila kundi kusema linachokifikiri?

Salim Said na Ummy Muya

SHURA ya Maimamu Tanzania imezindua rasmi mwongozo wa pamoja kwa Waislaam kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu mwakani.

Waraka huo, ambao umetumia maneno "sidanganyiki kwa wanasiasa wasio waaminifu na kupiga kura ya kundi" unawaelezea waumini wa dini ya Kiislamu sifa za kiongozi anayefaa kuchaguliwa katika chaguzi zijazo.

Mwongozo huo una kurasa 45 na sehemu 19 zinazoeleza taswira ya uchaguzi wa mwaka 2005, dhana ya uchaguzi, uhuru wa kutoa maoni, tumefikaje hapa tulipo, maadili, elimu, afya, kilimo, fedha na uwezeshaji, maisha bora, sheria, umoja na amani, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, uwakilishi wa umma, hadaa za uchaguzi na dira katika uchaguzi na hitimisho.

Akizungumza katika uzinduzi wa mwongozo huo uliohudhuriwa na mamia ya waislamu kutoka mikoa 22 ya Tanzania na kufunguliwa na amiri wa shura ya maimamu, Sheikh Mussa Kundecha, mhadhiri wa msikiti wa Idrisa, Sheikh Ally Basaleh aliwataka Waislamu kushikamana na kupiga kura kama kundi maslahi na kuwaambia wanasiasa wasio waaminifu kuwa hawadanganywi tena kwenye chaguzi.

Katibu wa kamati kuu ya siasa ya Shura ya Maimamu, Sheikh Ponda Issa Ponda ndiye aliyezindua mwongozo huo.

"Waislaam nchini tumedanganywa sana na wanasiasa wasio waaminifu chini ya serikali ya Chama cha Mapinduzi, lakini kuanzia sasa tunaingia katika uchaguzi na kupiga kura ya maslahi kama kundi maslahi, na hili si jambo baya," alisema Sheikh Basaleh.

"Tumedanganywa, hatukudanganywa? Tumedanganywa, hatukudanganywa," alihoji Basaleh na kujibiwa na umati wa waumini wa madhehebu mbalimbali ya Kiislaamu kwa sauti ya pamoja wakisema: "Tumedanganywaa."

Alisema: "Katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu na ule wa urais, wabunge na madiwani mwakani, waislamu tuseme hatudanganyiki."

Aliwaeleza kuwa kura itakayomkomboa kila mwananchi ni kura ya maslahi pekee.

Awali akifungua mkutano huo, Sheikh Mussa Kundecha aliiomba serikali kuufuata mwongozo huo ili kuweza kuzitawala nyoyo za wananchi na kwamba iwapo itaupuuza itawaongoza wananchi katika maafa makubwa ambayo hayajawahi kutokea nchini.

"Mwongozo huu ni wa watu wote na Waislaam. Serikali ... ikiupuuza itawaongoza wananchi katika maafa makubwa ambayo hayajawahi kutokea nchini hata mara moja," alisema Sheikh Kundecha.

Kwa mujibu wa Kundecha, mwongozo huo umetolewa baada ya serikali kushindwa kudhibiti makundi ya dini kutoa maoni yao binafsi, kitu ambacho alisema kinalenga kuvuruga amani, usalama na umoja wa kitaifa.

Aliilaumu serikali kwa kushindwa kuwashirikisha Watanzania katika mambo yanayowahusu na Waislaamu katika mambo yanayowahusu.

"Kwanza, tunakutana hapa kama Waislaam; pili kama Watanzania ili kuieleza serikali kwamba inapaswa kuwashirikisha Waislaam mapema katika mambo yanayowahusu bila ya kushinikizwa," alisema.

Mjumbe wa kamati kuu ya siasa ya shura ya maimamu, Sheikh Mohammed Issa alisema Tanzania ina makabila 120 na watu zaidi ya milioni 40 hivyo serikali inapaswa kujenga umoja katika makabila hayo badala ya kuendeleza ubaguzi mtu, dini na ukabila.

"Ukifanya ubaguzi wa aina yoyote unatengeneza bomu na dhambi kubwa isiyofutika. Kwa Tanzania, Waislaam ndio waliobeba uhuru na ukombozi wa nchi hii," alisema Issa.

"Waislaam hawapaswi kukubali kudhulumiwa hata kidogo na serikali haipaswi kufanya ubaguzi wa aina yoyote kwa sababu sote tunaipenda nchi yetu, sote tuna haki ya nchi yetu na sote ni muhimu na hakuna aliye muhimu zaidi kuliko mwingine."

Alisema wazee wa kiislaam walisimama katika viwanja vya Mnazi Mmoja miaka 50 iliyopita kupambana na dhulma, uonevu na kudai ukombozi wa Tanzania na kwamba na wao wamekutana hapo kufanya kama kile kilichofanywa na wazee hao.

"Tutachagua kiongozi mwenye imani ambaye atakuwa muadilifu na hatutakubali kubabaishwa na suti ya mtu yeyote. Sisi kuingia katika uchaguzi kama kundi maslahi si dhambi," alisema Issa.

Pia alimshukia Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Philip Marmo kwa kuwaonya Waislaam kutoa mwongozo huo wakati alishindwa kufanya hivyo kwa waraka wa Kanisa Katoliki uliotolewa miezi kadhaa iliyopita.

"Hii yote ni kwa sababu serikali haina mdomo mbele ya kanisa na hata Kingunge ambaye alionya waraka huo amezidiwa nguvu na kufunga mdomo kwa kusema 'No Comments' alipoulizwa na vyombo vya habari juzi,"alisema.
Baada ya hotuba hizo, mwongozo huo ulianza kuuzwa kwa Sh2,000 kwa nakala na watu walijipanga kwenye misululu wakisubiri kununua waraka huo.

Chanzo:http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=14210
 
Kwa hiyo Serikali inatakiwa ifuate MWONGOZO la sivyo hawatapewa kura au namna gani? Au tuseme kama atatokea mwanasiasa mwenye kuukubali MWONGOZO ndiye atakayepewa kura? Tunamsubiri mzee 'no comment' kikongwe wa kikomunisti Kingunge, mzee wa 'hapa patamu' Makwaia wa Kuhenga na 'bwana madevu' maalim Seif kuupinga waraka huo kama walivyoupinga ule wa Kanisa Katoliki otherwise tutakuwa tumewajua janja yao ililenga kwenye nini!
 
It will be very interesting to see what Maalim Seif will say on this "Mwongozo". If you read between the lines of what has been reported in the papers today you get the impression that the Mwongozo is indirectly urging moslems to punish CCM by way of protest vote. If this happens who will benefit from this fallout? Your guess is as good as mine. Ni dhahiri CUF "watavuna" kura hizi na hivyo Maalim Seif is on the spot. Siasa inanoga sasa! Stay tuned.
 
Makubwa hayo1Nilijua toka mwanzo kuwa hayoyatatokeakwani waswahili husema'Usipoziba ufa utajenga ghorofa'.Serikali kutokuwana meno ya kukemea mambo yanayofanywa kiholela na baadhi ya watu kwa kisingizio cha imani za kidini ni kukaribisha machafuko ambayo hakuna awezae kuyazuia matokeo yake ni kama yaliyotokea Rwanda,Burundi,Lebanoni,Irelana kaskazini n.k.
Jamani tuungane pamoja kupiga vita mambo haya kwani leo huyu kasema hivi na kesho yule atasema vile.
 
Kama Waraka utakuwa ni kwa Mustakabali wa Taifa then I real welcome it, tuuchambue ila kama ni COUNTER ROMAN CATHOLIT WARAKA then watakuwa wameshindwa kabla hawajaanza

Waraka wa kiislamu na wala si wa waislamu haujamlenga muislam bali jamii nzima, hauzungumzii kanisa limekosea wapi bali wananchi wanabainishiwa wajibu wao.

MAONI BINAFSI JUU YAKO.
Unaweza kubadilisha hiyo picha yako maana kusema ukweli napata tabu sana kusoma mchango wako au kulazimika kuuacha kabisa kama utakuwa mrefu.

Thanks for your understanding
 
It will be very interesting to see what Maalim Seif will say on this "Mwongozo". If you read between the lines of what has been reported in the papers today you get the impression that the Mwongozo is indirectly urging moslems to punish CCM by way of protest vote. If this happens who will benefit from this fallout? Your guess is as good as mine. Ni dhahiri CUF "watavuna" kura hizi na hivyo Maalim Seif is on the spot. Siasa inanoga sasa! Stay tuned.

Unafikiri sisi Waislam huwa tunaburuzwa kama Wakiristo? Hiyo block vote haipo ndugu yangu. Tutapima, kwa sasa CCM inayolalamikiwa imejaa Waislam na hatuna kipimo kinachokubalika kupima Muislam safi ni nani kati aliye na CCM na aliye CUF.
 
Baija Bolobi!

Yanapokuja malumbano ya kidini naomba nisichangie kwani katika makuzi nilifundishwa kuheshimu kila mtu linapokuja swala la imani kwani tulio wengi hatujawahi kuchagua tuwe waislaam au wakristo inategemea tu ulipozaliwa wazazi wako walikuwa dini gani.

Huo waraka sijausoma ila nimeguswa na bei inayouzwa Shilingi 2000 nakala moja? isije kuwa kuna wajanja wameanzisha DECI kwani kila penye mauzo yatakiwa risiti na kodi ya KAISARI ikusanywe au nakosea!

Hivi ule waraka wa WARUMI(Wakatoliki) ulikuwa unauzwa bei gani au ulikuwa bure. Sitaki kulumbana na Mashehe nisije somewa dua mbaya.

Hivi ni waislamu wangapi wanaweza kulipa elfu mbili kununua waraka badala ya kuongezea na kununua futari. Nisameheni tena huu ni mwezi wa toba kuna haja ya mpambano au kuganga njaa ili wajanja fulani wapate vijisenti vya kuserebuka kwenye sikukuu za Eid Mubarak !!! Huo waraka si ungetolewa baadae au uchaguzi ni Oktoba 2009.

Kuuliza sio ujinga ila ni kutaka kuelimishwa.
 
Waraka wa kiislamu na wala si wa waislamu haujamlenga muislam bali jamii nzima, hauzungumzii kanisa limekosea wapi bali wananchi wanabainishiwa wajibu wao.

MAONI BINAFSI JUU YAKO.
Unaweza kubadilisha hiyo picha yako maana kusema ukweli napata tabu sana kusoma mchango wako au kulazimika kuuacha kabisa kama utakuwa mrefu.

Thanks for your understanding

Lazima utakuwa na Makengeza, maana sioni sehemu yoyote uliyoniquote nasema Waraka wa Waislam.

Nini tofauti kati ya Waislamu na Kiislamu, niambie ili nisije nikayachangaya haya maneno
 
Waachiwe watoe waraka wao na sisi wananchi tuchambue kama ni pumba tuwahukumu kwa pumba zao sidhani kama kuna sababu ya kuwazuia kutoa waraka wao.
Jamani waislamu go on leteni huo waraka ni haki yenu sisi turuhusuni kuusoma msije mkawa mmeuandika kwa lugha yenu ile ya kiarabu. Hapo tutawauliza maswali.

Tatizo la CCM na serikali yao wanaona kuwa kitu chochote kitakachotishia wao kuondolewa madarakani ni uvunjaji wa amani na kuhatarisha usalama wa taifa.

Kwa kuwa wanajua kuwa kama watu hawatawapigia kura na wao wamezoea kujitangaza washindi basi patazuka vurugu. Dawa ya kuchaguliwa si kutisha wananchi bali tumia nafasi uliyojitwalia ya kuongoza nchi kuwashawishi watu kwa kuboresha maisha yao, tengeneza ajira, kuza uchumi, shughulikia mafisadi hata kama ni rafiki zenu. Hamuwezi kuendelea kushika dola kwa ujanja ujanja na kudanganya watu takribani miaka 48 sasa tokea uhuru.

Wananchi (waislamu, wakristo, et al) wana haki yao ya msingi kikatiba kueleza kuwa wanataka kiongozi wao awe wa namna gani. Huu ujanja wa kutumia polisi na UWT kuwathibiti watu kwa kisingizio cha kuchanganya dini na siasa hauna justification kwenye democratic society, otherwise ni kutangaza kuwa Tanzania inaendeshwa kwa mfumo wa kidikteta.

Serikali inahofia nini kuhusu hizi nyaraka?. Kama kweli wao wamefanya kile walichokiahidi katika kampeni na kuwa wao ni safi hakuna haja ya kutoa maonyo ambayo msingi wake unaonekana wazi kuwa ni kulinda maslahi ya watawala wachache na chama chao

1251533506_3.jpg

1251533506_4.jpg

1251533506_5.jpg
 
Baija Bolobi!

Yanapokuja malumbano ya kidini naomba nisichangie kwani katika makuzi nilifundishwa kuheshimu kila mtu linapokuja swala la imani kwani tulio wengi hatujawahi kuchagua tuwe waislaam au wakristo inategemea tu ulipozaliwa wazazi wako walikuwa dini gani.

Huo waraka sijausoma ila nimeguswa na bei inayouzwa Shilingi 2000 nakala moja? isije kuwa kuna wajanja wameanzisha DECI kwani kila penye mauzo yatakiwa risiti na kodi ya KAISARI ikusanywe au nakosea!

Hivi ule waraka wa WARUMI(Wakatoliki) ulikuwa unauzwa bei gani au ulikuwa bure. Sitaki kulumbana na Mashehe nisije somewa dua mbaya.

Hivi ni waislamu wangapi wanaweza kulipa elfu mbili kununua waraka badala ya kuongezea na kununua futari. Nisameheni tena huu ni mwezi wa toba kuna haja ya mpambano au kuganga njaa ili wajanja fulani wapate vijisenti vya kuserebuka kwenye sikukuu za Eid Mubarak !!! Huo waraka si ungetolewa baadae au uchaguzi ni Oktoba 2009.

Kuuliza sio ujinga ila ni kutaka kuelimishwa.

Mkereme
Waraka wa WARUMI haukuuzwa, ulitolewa bure na ulilenga waumini wao.
Hii habari ya wajanja hata mimi naona kuna hatari ya kuwa tunatumiana ili kuganga njaa ya watu. Lakini nisiseme mengi, maana sisi tulio bara tumeambiwa tutaletewa na hatukuambiwa tuandae fedha.
 
"Ukifanya ubaguzi wa aina yoyote unatengeneza bomu na dhambi kubwa isiyofutika. Kwa Tanzania, Waislaam ndio waliobeba uhuru na ukombozi wa nchi hii," alisema Issa.
Enyi waislamu ni nani aliyewaroga kuwa ninyi peke yenu mlipigania uhuru wa Tanzania?Tanzania ilitawalia na nani? Mwalimu Nyerere nini?

Ukishakuwa taharia utaongea hovyo sana.

Kama ni uhuru wa Tanganyika aliyepigania tena mstari ni mkatoliki Julius Kambarage Nyerere, narudia tena nyie mlikuwa fuata upepo, kwani muda mwingi wa kampeni mlikuwa hamna kazi ya kufanya zaidi ya kucheza bao, hivyo ilikuwa rahisi kwenu kufuata mikutano ya Nyerere.

Mfano mzuri ni zile movement za Martin Luther, waislamu na vikofia vyao walikuwa nyuma nyuma kama walinzi vile.
Kwahiyo mwataka kusema nanyi(waislamu) mlipigania uhuru wa watu weusi Marekani.

Acheni ulimbukeni na mizuka ya kipepo pepo hiyo, uhuru wa Nchi hii alipigania Nyerere.

Ninyi hamna historia ya kupigania uhuru zaidi ya kujilipua na mabomu.

Karume alishindwa kumtoa mwarabu zenj, ikabidi Nyerere kwa kushirikiana Okello ndiyo zoezi likafanikiwa.

Back
Top Bottom