WARAKA WA WAZI KWA LADY JAY DEE kUHUSU WIMBO YAHAYA

WARAKA WA WAZI KWA LADY JAY DEE kUHUSU WIMBO YAHAYA

Mimi ni miongoni mwa mamilioni ya watanzania ambao wana ji identify themselves kama mashabiki wako wakubwa. But kina kitu kimoja ambacho kwa maoni yangu ninaona hakipo sawa . Nacho ni kuhusu wmbo wako uitwao YAHAYA. Wimbo wako ni mzuri na unaelimisha jamii but kwa nini usingetumia jina tofauti na YAHAYA. Kwanini ninasema hivyo?

1. YAHAYA ni jina la kiislamu, na miongoni mwa majina ya kiislamu yenye maana kubwa kwa waislam.
2. Wewe ni mkristo wa madhehebu ya wasabato.
3. Hapa kwetu nchini Tanzania kuna vugu vugu la waislamu na wakristo. Waislamu wamekuwa makini sana kwa kila kitu kinacho fanywa na mtu yoyote yule mwenye jina la kikristo hususani pale maslahi ya dini ya kiislamu ama jina la kiislamu linapotajwa. Sihitaji kulizungumzia hili kwa kina kwa sababu naamini huwa unafuatilia taarifa mbalimbali za habari so am sure as hell unafahamu ni kitu gani kinaendelea kati ya wakristo na waislamu Tanzania wakati huu.

( KITU CHA MSINGI KUELEWA HAPA NI KWAMBA, KITU CHOCHOTE KILE KITAKACHO TAJWA NA MKRISTO DHIDI YA UISLAMU AMA MUISLAMU KWA NAMNA YOYOTE ILE KINAWEZA KUCHUKULIWA KAMA KASHFA DHIDI YA UISLAMU )

Hivyo basi wimbo wako wa YAHAYA ingawa una ujumbe mzuri, but unaweza kukuletea matatizo na waislamu wa Tanzania ambao wanaweza kuuchukulia kama kashfa dhidi yao. Maadui zako wanaweza kuitumia hiyo kama loop hole na ku dress beef lenu kulifanya lionekane kama beef kati yako waislamu.

MAPENDEKEZO: Nikiwa kama shabiki wako, ninakushauri ubadilishe haraka iwezekanavyo jina la wimbo YAHAYA na kutafuta jina lingine lolote lile. Katika kutafuta jina nakushauri utafute jina ambalo halihusiani na jina la dini yoyote kati ya ukristo na uislamu. Unaweza kutumia majina yanayo tumiwa na watu wa dini zote kama vile MAWAZO.
Ukibadilisha jina la wimbo wako, utajijengea heshima kubwa sana kwa mashabiki wako ambao ni waislamu na watachukulia hiyo kama heshima kwao.
Sina mengi ya kuongea zaidi ya hayo. Natumaini umenielewa.

NAKUTAKIA MAANDALIZI MEMA YA MAADHIMISHO YA MIAKA 13 YA LADYJAYDEE.

mfyuuuuu ujinga huuu wewe ndo mdini mkibwa alshababu weye
 
Jina ni jina achana na maneno ya watu coz hapo cdhani kama kuna shida yyt wala udini,,unachofanya ni kuelimisha jamii yahaya ni jina tu
 
uwezo wako mdogo sn wa kuchanganua mambo na uache udini c lazma uandike km huna cha kuandika
 
hyo ni sawa na muislam kwenda bar kunywa pombe afu then uanze kucomplaign kwamba umeseviwa pombe kwenye glassi yenye harufu ya mafuta ya nguruwe.
 
non sense ungekuwa unajua kama lugha ni sauti za nasabu usingeandika haya uliyoandika...
 
Kweli asee
 
Attachments

  • uploadfromtaptalk1380403076765.jpg
    uploadfromtaptalk1380403076765.jpg
    32.9 KB · Views: 185
Mimi ni miongoni mwa mamilioni ya watanzania ambao wana ji identify themselves kama mashabiki wako wakubwa. But kina kitu kimoja ambacho kwa maoni yangu ninaona hakipo sawa . Nacho ni kuhusu wmbo wako uitwao YAHAYA. Wimbo wako ni mzuri na unaelimisha jamii but kwa nini usingetumia jina tofauti na YAHAYA. Kwanini ninasema hivyo?

1. YAHAYA ni jina la kiislamu, na miongoni mwa majina ya kiislamu yenye maana kubwa kwa waislam.
2. Wewe ni mkristo wa madhehebu ya wasabato.
3. Hapa kwetu nchini Tanzania kuna vugu vugu la waislamu na wakristo. Waislamu wamekuwa makini sana kwa kila kitu kinacho fanywa na mtu yoyote yule mwenye jina la kikristo hususani pale maslahi ya dini ya kiislamu ama jina la kiislamu linapotajwa. Sihitaji kulizungumzia hili kwa kina kwa sababu naamini huwa unafuatilia taarifa mbalimbali za habari so am sure as hell unafahamu ni kitu gani kinaendelea kati ya wakristo na waislamu Tanzania wakati huu.

( KITU CHA MSINGI KUELEWA HAPA NI KWAMBA, KITU CHOCHOTE KILE KITAKACHO TAJWA NA MKRISTO DHIDI YA UISLAMU AMA MUISLAMU KWA NAMNA YOYOTE ILE KINAWEZA KUCHUKULIWA KAMA KASHFA DHIDI YA UISLAMU )

Hivyo basi wimbo wako wa YAHAYA ingawa una ujumbe mzuri, but unaweza kukuletea matatizo na waislamu wa Tanzania ambao wanaweza kuuchukulia kama kashfa dhidi yao. Maadui zako wanaweza kuitumia hiyo kama loop hole na ku dress beef lenu kulifanya lionekane kama beef kati yako waislamu.

MAPENDEKEZO: Nikiwa kama shabiki wako, ninakushauri ubadilishe haraka iwezekanavyo jina la wimbo YAHAYA na kutafuta jina lingine lolote lile. Katika kutafuta jina nakushauri utafute jina ambalo halihusiani na jina la dini yoyote kati ya ukristo na uislamu. Unaweza kutumia majina yanayo tumiwa na watu wa dini zote kama vile MAWAZO.
Ukibadilisha jina la wimbo wako, utajijengea heshima kubwa sana kwa mashabiki wako ambao ni waislamu na watachukulia hiyo kama heshima kwao.
Sina mengi ya kuongea zaidi ya hayo. Natumaini umenielewa.

NAKUTAKIA MAANDALIZI MEMA YA MAADHIMISHO YA MIAKA 13 YA LADYJAYDEE.

Mi nina wasiwasi we jina lako ni YAHAYA
 
Hay usomapo Lyrics za huu wimbo au uusikilizapo wimbo huu, replace jina la YAHAYA kwa jina la JOHN au JOSEPH....umeridhika? Username yako ni LIKUD...wale waasi/extremists wa Uturuki so tushajua behind ya ushauri wako. Kisheria hakuna hatimiliki ya jina moja kama hilo. Haya ushahara, kachukue posho yako kwa Ruge!!
 
Hata kama ni Yahya asiimbwe kisa dini? Namkumbuka Mario Abdallah Mgulunde...
 
Nakuoongezea na mengine Kassim na Isihaka. But

Mtoto Iddy .............Juma Nature ni muislamu na umetoka kipindi hicho hakuna vuguvugu la udini Tz.

Masudi ..............Msondo Ngoma/Sikinde: Asilimia kubwa ya waimbaji wakuu kwenye hizo bendi ni waislamu, waimbaji viongozi kwenye hizo bend pia ni waislamu/ nyimbo hizo zimetoka kipindi hicho hakukuwa na upepo wa udini Tz kama uliopo hivi sasa. Sasa hivi udini umewaingia sana watz kiasi huko mashuleni mwalimu wa dini moja akimpa adhabu ya viboko mwanafunzi wa dini nyingine, inaweza kutafsiriwa kama udini. Naamini kama Jide angekuwa muislamu, beef yake na Ruge ingeweza kutazamwa katika sura ya udini

Mkuu una uhakika gani mtunzi wa wimbo wa Yahaya sio MUISLAMU? Hebu acha hizo
 
Mleta uzi una tatizo kubwa sana la udini. Je, wafahamu kuwa kuna wakristu wengi tu wana wana majina ya kiislamu? Jina sio imani.
 
Yahaya akiwa tapeli na haeleweki eleweki haimaanishi waislam woote wapo ivyo, lengo la Jide ni kufikisha ujumbe na wala hakulenga dini.. Ni sawa na Juma Nature alivyoimba Mtoto Iddi, Offside Trick walivyoimba Ahmada, Nyimbo kama Mario nk.. Usifikirie sana dini coz zote zimeletwa na meli
 
yahaya unaishi wapi.....oooo yahaya.watu wadini kweli
 
wanatafuta sababu za kumwagia asidi jay dee!
 
Kaka umechanganyikiwa na kuvurugika kabisa! Unachofanya ni kujaribu kutulisha udini wako! Tanzania ina dini nyingi usitake kufanya watu wawe watumwa wa dini zao!!!!! Mbona kulikuwa na wimbo wa mtoto iddi na nyingine nyingi tu!!! Watu kaka wewe ndo wana akili za "Alshabab"! Fikra zako ni potofu...hazioni mbali zaidi ya udini na nina hakika wewe kabla ya kupanda daladala unamuuliza konda/dereva na abiria wengine kama ni waislamu au wakristo!:A S tongue:
 
Back
Top Bottom