#COVID19 Waraka wa wazi kwa Marais wetu Wastaafu kuhusiana na hali ya Corona nchini

Kwenu marais wetu Wastaafu, Mwinyi, Mkapa na rais Kikwete.

Kwa heshima na taadhima inafikirisha kuwaandikia waraka huu baada ya kuwa kwa dhati kabisa, njia nyingi zimejaribiwa kushauri, kuhimiza, kuomba, kuisihi nk ili kuwepo mtizamo tofauti kuhusiana na ugonjwa huu.

Nchi hii ni yetu sote kiasi kuwa kwa yeyote yule, awe mkubwa au mdogo kunyamaza kimya tu wakati ni wazi kuwa labda tunakoelekea sasa siko, siyo jambo ambalo tunaweza kulichagua kama moja ya uwezekano tena.

Waheshimiwa katika nyakati tofauti mmewahi kupokea hatamu za serikali na kuiongoza nchi hii pendwa kama watakavyo kuja na kutoka wengine kwa njia za amani. Siyo siri kuwa kama marais wastaafu nafasi yenu ya kulitumikia taifa hili ingalipo. Ni wazi kuwa, katu marehemu baba wa taifa (rip) asingelikubali kuliacha taifa hili ambalo limekuwa la kupigiwa mfano siku zote kuangamia.

Waheshimiwa, msiliache taifa hili kuangamia na ugonjwa huu huku mkiangalia tu. Mnayo nafasi ya kuliunganisha taifa hili kuwa moja ili kwa pamoja tukaishinda Corona kwa salama.

Shime waheshimiwa msilinyime taifa hili hekima wala busara zenu, ambazo kwa hakika zinahitajika sana kwa sasa labda kuliko kipindi kingine chochote kilichowahi kupita.

Kwa umoja wenu kama wananchi wa nchi hii au katika nafasi zenu ka mtanzania mmoja mmoja mnayo nafasi ya kushauriana na mheshimiwa rais kwa niaba yetu sisi wananchi.

Umoja wetu utokanao na kushawishiana kwa nguvu za hoja si hoja za nguvu utatuvusha katika vita hivi.

Kama watanzania tunastahili kuushinda ugonjwa huu kama jambo la dharura kweli kweli vinginevyo kama ilivyo wazi, maisha ya wengi wetu yako hatarini mno.

Mungu ibariki Tanzania. Mungu tujalie salama tunavyomuunga kupambana na ugonjwa huu.

Nawasilisha.
Mbona unahangaika kuomba watu waoteze maisha? Twambie kaya yako, ya jirani, ndugu, na rafiki wangapi una uhakika wameambukizwa au vifo kutokana na COVID-19.

Njia sahihi zinazohimizwa na wataalamu ni za kinga, hivyo basi wewe na wapendwa wako, msiache kuzingatia.

JIKINGE UMKINGE JIRANI

JILINDE UWALINDE UWAPENDAO
 
Mkuu hatuendi shule kutembea.

Maongezeko ya vifo wewe huyaoni na kuwa wewe huoni kuwa yako njiani na hatimaye yatakufikia tu?

Au wewe yote haya huyaoni mkuu?

Kwani yaliyowakuta wana makosa gani ambayo wewe huna? Hatuwezi kuwa na mkakati muafaka ukatuhakikishia usalama wetu sote?
 
Bado unaomba watu wafe ndoto zako zitimie? Utasubiri sana kama ambavyo huwezi kukikamata kivuli chako.

Kwanza korona ni kagonjwa kadogo. Pili mtu akizingatia ushauri wa kujikinga dhidi ya maambukizi hako kagonjwa hakaoni ndani.

JIKINGE UMKINGE JIRANI

JILINDE UWALINDE UWAPENDAO

KWA PAMOJA TANZANIA BILA KORONA INAWEZEKANA.

TIMIZA WAJIBU WAKO
 
Wewe ni zwazwa kuliko msukule. Unadhani kwa vile akili yako iko kwenye siasa basi kila mtu ni CCM au CHADEMA au chama fulani?

Au nyie ni mumiani mnaojipatia damu au nyama ya kula kwa kila mfu? Watu wa namna gani msiokuwa na chembe ya huruma nyie?

Huo uchadema unausomea wapi, msukule wahedi wee!
Wanaturudisha nyuma Sana hao watu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao wazee bado wanayo a Roll to Play, tena haswa Mkapa na Kikwete, kwani wao walihusika sana na mchakato wa kutuketea Magufuli.

Sasa kama Raisi Magufuli ni muungwana atawasikiliza hawa wazee, na watashauriana vizuri kwa manufaa ya nchi.

Lakini issue sio Cirona pekee yake, hali ya nchii inavyoendeshwa pia linahitaji kuangaliwa kwa makini, mengi yasio pendeza yanatendeka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanaturudisha nyuma Sana hao watu

Sent using Jamii Forums mobile app

Sana tu. Ni ajabu mno kuwa wanachopata ni nini?

Nimejaribu kuongea na watu wengi na aina mbalimbali. Walio wengi na wenye akili zao hawakubaliani na status quo. Nani anaweza kumshauri Magufuli akatuelewa tunataka nini.

Ajabu na kweli hata marais wastaafu hawa misukule wanajaribu kufanya kila kitu wawa stifle wasifanye lolote!

They are driving us to the limit. wanachochea vurugu ambayo mwungwana yeyote hawezi kuitaka. Kwa upumbaav wao wanadhani wana msaidia mkuu kumbe wanamharibia sana tu.

Way forward pana haja ya kuwapuuza misukule vilivyo Usidhani wala kuwa wapo wengi. Wana fake ID nyingi wanazozifanyia kazi kwa shift 24x7.

Ni wale watu wasiojulikana. Watu walioshindwa. Hawana sera wala jipya. Wameapizwa kutetea juhudi no matter what (indeed hata kama wan***kwa). Wako humu ndani kuleta mitafaruku tusielewane wala kijinga mbele. Wemeapishwa hivyo hata kama kwa kufanya hivyo is to their own peril.

Nia yao ni kutunyamazisha. Hatutanyamaxa bali lazima tuwe na utaratibu wa kuwanyamazisha wao kuwapuuza. Ili wajue wazi kuwa tumewapuuza na hawana jipya.
 
Hao wazee bado wanayo a Roll to Play, tena haswa Mkapa na Kikwete, kwani wao walihusika sana na mchakato wa kutuketea Magufuli.

Sasa kama Raisi Magufuli ni muungwana atawasikiliza hawa wazee, na watashauriana vizuri kwa manufaa ya nchi.

Lakini issue sio Cirona pekee yake, hali ya nchii inavyoendeshwa pia linahitaji kuangaliwa kwa makini, mengi yasio pendeza yanatendeka.

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu nakubaliana nawe Ila tuwe na pa kuanzia. Dharura kubwa kwa sasa ni kwenye huu ugonjwa. Tupiganie uhai wetu kwanza. Mengine yatatafuata na kuwa na tija tu iwapo tutakuwa tuko hai.

Tufike kwanza daraja hili kwanza, tulivuke. Yuko wapi katibu sijui mwenyekiti wa taboa. Nina amini alikuwa na mengi aliyopenda yaboreshwe.

One thing at a time.

Wazee wastaafu hawa wanayo nafasi kubwa ya kufanikisha busara kutamalaki tukafanyia kazi yaliyo ya maana kwenye hali ya utulivu na amani.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Mkuu hatuendi shule kutembea.

Maongezeko ya vifo wewe huyaoni na kuwa wewe huoni kuwa yako njiani na hatimaye yatakufikia tu?

Au wewe yote haya huyaoni mkuu?

Kwani yaliyowakuta wana makosa gani ambayo wewe huna? Hatuwezi kuwa na mkakati muafaka ukatuhakikishia usalama wetu sote?

Hakuna asiyeogopa kifo. Kama kweli kuna maongezeko ya vifo, wananchi wasingeonekana wakiendesha maisha yao kama kawaida. Ukiibitisha mtaani kwako wangapi wamekufa na kufanya majirani mwogope na kujifungia ndani, nitaamini maneno yako. La acha uzushi.
 
Bila shaka kwa bandiko lako una maanisha hakuna vifo wala watu hawafi tena.

Kaza uzi hapo hapo.

Kikombe cha babu tokea Antananarivo kipo ndani ya nyumba uwe na hofu gani tena mkuu?

Chochea nyungu mwanamme.
 
Sasa wao watafanya nini? Washauri kuhusu nini labda? au watoe suluhu ipi? ukiona kimya jua na wao hawana majibu
Ni wanufaika wa mfumo hawawezi wazia we mwenye njaa, unafiki wa mtz ukimuona anapiga kelele au anamtetea mtz mwenzake ni sababu ya njaa
 
Hapana mkuu hawa wanaweza kuwa pekee wakombozi wetu kwa hali ya sasa.
Hata Nyerere angekuwepo asingefanya kitu angefunua mdomo angekuwa jela uhujumu uchumi au yamkute ya wasiojulikana
 
Huku mtaani watu wanasema hakuna maambukizi na serikali inamwagiwa sifa kwa kuishinda corona maana wanasema hakuna maambukizi mapya wala vifo. Wanasubiri wamuone PM kwenye luninga kusikia tarehe ya kufungua shule tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenu marais wetu Wastaafu, Mwinyi, Mkapa na rais Kikwete.

Kwa heshima na taadhima inafikirisha kuwaandikia waraka huu baada ya kuwa kwa dhati kabisa, njia nyingi zimejaribiwa kushauri, kuhimiza, kuomba, kuisihi nk ili kuwepo mtizamo tofauti kuhusiana na ugonjwa huu.

Nchi hii ni yetu sote kiasi kuwa kwa yeyote yule, awe mkubwa au mdogo kunyamaza kimya tu wakati ni wazi kuwa labda tunakoelekea sasa siko, siyo jambo ambalo tunaweza kulichagua kama moja ya uwezekano tena.

Waheshimiwa katika nyakati tofauti mmewahi kupokea hatamu za serikali na kuiongoza nchi hii pendwa kama watakavyo kuja na kutoka wengine kwa njia za amani. Siyo siri kuwa kama marais wastaafu nafasi yenu ya kulitumikia taifa hili ingalipo. Ni wazi kuwa, katu marehemu baba wa taifa (rip) asingelikubali kuliacha taifa hili ambalo limekuwa la kupigiwa mfano siku zote kuangamia.

Waheshimiwa, msiliache taifa hili kuangamia na ugonjwa huu huku mkiangalia tu. Mnayo nafasi ya kuliunganisha taifa hili kuwa moja ili kwa pamoja tukaishinda Corona kwa salama.

Shime waheshimiwa msilinyime taifa hili hekima wala busara zenu, ambazo kwa hakika zinahitajika sana kwa sasa labda kuliko kipindi kingine chochote kilichowahi kupita.

Kwa umoja wenu kama wananchi wa nchi hii au katika nafasi zenu ka mtanzania mmoja mmoja mnayo nafasi ya kushauriana na mheshimiwa rais kwa niaba yetu sisi wananchi.

Umoja wetu utokanao na kushawishiana kwa nguvu za hoja si hoja za nguvu utatuvusha katika vita hivi.

Kama watanzania tunastahili kuushinda ugonjwa huu kama jambo la dharura kweli kweli vinginevyo kama ilivyo wazi, maisha ya wengi wetu yako hatarini mno.

Mungu ibariki Tanzania. Mungu tujalie salama tunavyomuunga kupambana na ugonjwa huu.

Nawasilisha.
Wanaogopa kufilisiwa mali zao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata Nyerere angekuwepo asingefanya kitu angefunua mdomo angekuwa jela uhujumu uchumi au yamkute ya wasiojulikana

Nyerere (rip) alikuwa tofauti. Yule alikuwa really baba wa taifa.

Kwake Tanzania na Africa ilikuwa vyote hakuwa na mzaha.

Huyo alikuwa mwana halisi wa nchi hii hakuwa na mfano apumzike kwa amani.
 
Wanaogopa kufilisiwa mali zao

Sent using Jamii Forums mobile app

Hawa wanaweza kuwa waokozi wetu pekee waliobakia.

Ingependeza kama wote wasiopendezwa na hatua zinazochukuliwa bila kujali vyama tukaunganisha nguvu kuonana na marais wastaafu hawa kwa majadiliano.

Hili si la kisiasa hata kidogo.

Ni suala halusi la kizalendo.

Uzalendo hauna chama!
 
Labda Kama wangepigwa njaa.TISS wangekuwa smart yaani kujali nchi kuliko mtu yasingekuwapo haya
 
wazee wa watu kila wakipiga simu wanaambiwa wawasilishe ushauri wao kimaandishi. haaa haaa
 
Hawa wazee si wajinga kiasi cha kushabikia haya tunayo yaona.

Wenye mawazo tofauti toka madhehebu ya dini, vyama vya siasa, asasi za kiraia nk wangeweza ku spear head hili.

Starting point to seek audience na hawa former presidents. Kushauriana na ili kuona namna ya kushauriana na mtukufu rais kwa mstakabala tofauti.

Kuvunjika kwa koleo si mwisho wa uhunzi.
 
wazee wa watu kila wakipiga simu wanaambiwa wawasilishe ushauri wao kimaandishi. haaa haaa

Mwalimu (rest in peace) kwenye mambo nyeti kama haya alizoea kusema: "haya ni yetu siyo ya rais. Kama yeye hataki kuelewa tutayapeleka kwa wananchi". Mwisho wa kumnukuu.

Huyu ni kiongozi wetu hawezi kukataa kusikiliza. Apewe confidence kujua there's no malice. Tunachotaka Corona kuondoshwa nchini.

Kwa pamoja tuweke mkakati unaota na ambao utatupa matokeo tunayo yahitaji.

Afahamu hii siyo siasa ni suala la life and death.
 
Back
Top Bottom