#COVID19 Waraka wa wazi kwa Marais wetu Wastaafu kuhusiana na hali ya Corona nchini

#COVID19 Waraka wa wazi kwa Marais wetu Wastaafu kuhusiana na hali ya Corona nchini

Hawa wazee si wajinga kiasi cha kushabikia haya tunayo yaona.

Wenye mawazo tofauti toka madhehebu ya dini, vyama vya siasa, asasi za kiraia nk wangeweza ku spear head hili.

Starting point to seek audience na hawa former presidents. Kushauriana na ili kuona namna ya kushauriana na mtukufu rais kwa mstakabala tofauti.

Kuvunjika kwa koleo si mwisho wa uhunzi.
Unafiki wa tz jadi yetu we uoni hata vioy wa dini wako kimya wanaogopa kufungiwa makanisa yao na misikiti yao wanaogopa watakula wapi,Kenya viongozi ya dini wako smart awaabudu chama au mtu wanasimamia kweli wala awawaogopi wahuni yajapo maslai ya watu
 
Usitegemee kupata ushauri au msaada kwa mtu aliyeshiba hasa mtz
 
Unafiki wa tz jadi yetu we uoni hata vioy wa dini wako kimya wanaogopa kufungiwa makanisa yao na misikiti yao wanaogopa watakula wapi,Kenya viongozi ya dini wako smart awaabudu chama au mtu wanasimamia kweli wala awawaogopi wahuni yajapo maslai ya watu

Mkuu si wote. Wapo viongozi wa dini ambao wako vizuri sana tu. Si kama ambavyo wale uchwara uchwara walivyo.

Ukiwachanganya wote kwenye pakacha moja haitakuwa sawa.

Kumbuka wanasema njia ile iendayo kuzimuni ni pana.
 
Mkuu si wote. Wapo viongozi wa dini ambao wako vizuri sana tu kama ambavyo na wale uchwara uchwara wapo.

Kumbuka wanasema njia ile iendayo kuzimuni ni pana.
Labda wale wenye usajili wa kudumu msajili Hana ubavu wa kuyafuta
 
.....and two and half months later one of those you addressed in this thread is no longer with us! and the cause of his death is still SIRI KALI!

Kwenu marais wetu Wastaafu, Mwinyi, Mkapa na rais Kikwete.

Kwa heshima na taadhima inafikirisha kuwaandikia waraka huu baada ya kuwa kwa dhati kabisa, njia nyingi zimejaribiwa kushauri, kuhimiza, kuomba, kuisihi nk ili kuwepo mtizamo tofauti kuhusiana na ugonjwa huu.

Nchi hii ni yetu sote kiasi kuwa kwa yeyote yule, awe mkubwa au mdogo kunyamaza kimya tu wakati ni wazi kuwa labda tunakoelekea sasa siko, siyo jambo ambalo tunaweza kulichagua kama moja ya uwezekano tena.

Waheshimiwa katika nyakati tofauti mmewahi kupokea hatamu za serikali na kuiongoza nchi hii pendwa kama watakavyo kuja na kutoka wengine kwa njia za amani. Siyo siri kuwa kama marais wastaafu nafasi yenu ya kulitumikia taifa hili ingalipo. Ni wazi kuwa, katu marehemu baba wa taifa (rip) asingelikubali kuliacha taifa hili ambalo limekuwa la kupigiwa mfano siku zote kuangamia.

Waheshimiwa, msiliache taifa hili kuangamia na ugonjwa huu huku mkiangalia tu. Mnayo nafasi ya kuliunganisha taifa hili kuwa moja ili kwa pamoja tukaishinda Corona kwa salama.

Shime waheshimiwa msilinyime taifa hili hekima wala busara zenu, ambazo kwa hakika zinahitajika sana kwa sasa labda kuliko kipindi kingine chochote kilichowahi kupita.

Kwa umoja wenu kama wananchi wa nchi hii au katika nafasi zenu ka mtanzania mmoja mmoja mnayo nafasi ya kushauriana na mheshimiwa rais kwa niaba yetu sisi wananchi.

Umoja wetu utokanao na kushawishiana kwa nguvu za hoja si hoja za nguvu utatuvusha katika vita hivi.

Kama watanzania tunastahili kuushinda ugonjwa huu kama jambo la dharura kweli kweli vinginevyo kama ilivyo wazi, maisha ya wengi wetu yako hatarini mno.

Mungu ibariki Tanzania. Mungu tujalie salama tunavyomuunga kupambana na ugonjwa huu.

Nawasilisha.
 
.....and two and half months later one of those you addressed in this thread is no longer with us! and the cause of his death is still SIRI KALI!

I wish mzee wa Msoga sees this before time times him.

Long live mzee wa Msoga. Macho na matumaini yetu kwako.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Ahaaaaa. Mental disorders ahaaaa. Mimi sina mengi.

Shida sana mkuu. Bahati mbaya ni kuwa watu wa namna hiyo ndiyo manahodha wanaotuongozea chombo.

Pana ka wimbo kanasema:

"dereva,
akiwa shetani,
mwisho wake,
mwisho ni mauti."

Apumzike kwa amani rais Mkapa.

One down, two to go.
 
Hatuombi mabaya lakini corona haichagui nyazifa ya mtu,Tunapopaza sauti ni kwa maslahi ya nchi na raisi akiwemo.

Mzaha mzaha siku moja mkulu hata kama amejificha Chato ila hata yeye hili janga linaweza kumpata jambo ambalo ni hatari kwani fununu zilizopo anamaradhi ya moyo kitu ambacho huu ugonjwa ukiupata ni ngumu sana kukuacha salama.

Ni kweli tunahitaji kodi ya mapato ila atambue corona haichagui kiongozi.

Kuchukua hatua ni jambo la msingi sana.

Wengi zaidi watanusuriwa kwa kuamua kuanza kuchukua hatua.

Hili si suala la kufanyiwa mzaha.
 
Kwenye red yalikuwa sehemu ya uzi huu May 8, 2020:

IMG_20210320_200255_723.jpg

Mzee Kikwette unayo nafasi ya kuliokoa taifa hili.

Better late than never!
 
Hatuombi mabaya lakini corona haichagui nyazifa ya mtu,Tunapopaza sauti ni kwa maslahi ya nchi na raisi akiwemo.

Mzaha mzaha siku moja mkulu hata kama amejificha Chato ila hata yeye hili janga linaweza kumpata jambo ambalo ni hatari kwani fununu zilizopo anamaradhi ya moyo kitu ambacho huu ugonjwa ukiupata ni ngumu sana kukuacha salama.

Ni kweli tunahitaji kodi ya mapato ila atambue corona haichagui kiongozi.

Mkuu uliona mbali sana, ila sikio la kufa halisikii dawa.

Hiiiiii bagosha!
 
Back
Top Bottom