Wakati wa Mwalimu Julius Nyerere kulikuwa na 'compulsory primary school education' (kila mtoto - Mkristo au asiwe Mkristo alitakiwa aende shule). Pili, kulikuwa na 'compulsory national service' (kila mhitimu wa elimu ya sekondari alitakiwa aende Jeshi la Kujenga Taifa). Kutoka huko, kila aliyefaulu vizuri aliweza kuendelea chuo kikuu au vyuo vya ufundi au pia kurudi nyumbani kuendelea na ufugaji, kilimo au biashara (kujiajiri).
Mimi nimesoma enzi hizo na dini haikuwa issue hata kidogo. Kama ilitokea Waislamu waliwazuia watoto wao kusoma ni tatizo lao wenyewe. Sehemu (Mtaa) ninakoishi wengi ni Waislamu. Nyumba ninayoishi ina baraza kubwa na watoto wengi wanacheza pale kuanzia saa moja asubuhi hadi saa 5 usiku. Yaani ni kero sana!
Hii inasema kitu gani? Kwamba hawaendi shule! Na wale wanaoenda, wakirudi badala ya kufanya homework, wanaenda madrassa. Hivyo, badala ya kuelekeza nguvu sehemu moja, unakuta watoto hawapati muda mzuri wa kufanya mazoezi ya shuleni. Matokeo yake ni kushindwa kwenye mitihani yao. Je, haya yanafanywa na Wakristo?
Hebu angalia wazazi wa Kikristo wanafanyaje: mtoto anaenda shule, akirudi anasimamiwa afanye homework baada ya kupumzika, akimaliza ndipo anaruhusiwa acheze (na ikiwezekana kama bado hajaelewa vizuri anapelekwa tuition). Kwa hiyo, mwamko wa kusoma uko zaidi kwa watoto kutoka familia za Kikristo au dini zingine kuliko ilivyo kwa watoto kutoka familia za Kiislamu.