Kaka Tuma asante kwa hoja nzuri na maridhawa, naamini umeusoma huu waraka, je unaweza kuscan na kuuweka hapa ili wote tuusome? nitashukuru, unaweza kumtumia Invisible ili aweke incase kama hutaweza.Kama hutaweza kwa sababau za security(kama zipo) je waraka una page ngapi na ni wa tarehe gani? na umekuwa addressed kwa nani?
Pili mimi sio Mkatoliki ila ni Mkristo, mbona naona unachanganya kati ya ukatoliki na ukristo maana wakristo ni wengi sana mkuu!
Mwisho, mbona hawa viongozi wa kikatoliki siwaelewi? maana walisema JK chaguo la Mungu, kwa nini wamemgeuka tena leo? ina maana Mungu anabadilika??
Kila mtu anayechanguliwa kuwa kiongozi kwa ridhaa ya watu wake kwa kawaida hutafsiriwa kuwa ni chaguo la Mungu. Kwa hiyo, kusema Kikwete ni 'chaguo la Mungu' kuna maana ya kuwa kachaguliwa kwa ridhaa ya Watanzaia (watu wake).
Ila sasa, kumchagua kiongozi na baadaye akadhoofika katika uongozi wake hakumfungi mtu aliyemchagua kumkosoa (walau ndivyo binadamu tulivyo). Mfano, sheikh akishasimikwa anakuwa amewekwa wakfu kwa kazi ya Mungu. Kama huyo sheikh akifanya udhaifu fulani katika maisha yake huwezi kuzuia watu waliomsimika kumkosoa (hivyo hivyo kwa mchungaji, padre, askofu, papa) etc.
Kuna Latin maxim kwamba Vox populi, vox dei (the voice of the people is the voice of God) - hii ina maana ya sauti elekezi na mambo mema.
Kwa hiyo, kurudiarudia tu kwamba Wakatoliki ndio waliosema hivyo, hakuna maana yoyote. Mbona viongozi tunawachagua halafu wanavurunda, kwa hiyo tusiwakosowe kwa vile tuliwachagua? Vilevile kuna watu tunaona wanafanya mambo mazuri na tunaweza kusema ni watu wema/watu wa Mungu. Je, siku wakibadilika na kutenda mabaya tusiwakosowe kwa vile tulishasema ni wema?
Mimi naona tunatumia tu msemo huu 'sauti ya Mungu' bila kujua maana yake na ndiyo maana tunadhani kusema 'Kikwete ni chaguo la Mungu' tunaona kama Mungu ndiye alikuja hapa Tanzania mwaka 2005 na kumchagua Jakaya Kikwete kuwa Rais wa Tanzania.
Mbona huwa tunasema sisi ni watoto wa Mungu? Kwa hiyo, tuelewe 'chaguo la Mungu' kama 'chaguo la watu' (ndiyo maana yake). Ni kama kusema tumeumbwa kwa mfano wa Mungu - siyo kwamba tuna sura ya Mungu (physical appearence) ila kwamba tuna thamani kubwa machoni pa Mungu na Mungu ametupa heshima, utu (dignity).
Kuna mtaalamu mmoja aliweza kutumia maneno yafuatayo katika kuelezea utukufu wa Mungu: 'God's glory is to be a human being fully alive!' Kwa maneno mengine, utukufu wa Mungu unadhihirika pale binadamu anapoishi kama anavyotakiwa kuishi na muumba wake - kutumia vipaji vyake vizuri, kuwapenda na kuwaheshimu wenzake na kufanya kazi kadiri ya uwezo wake (as best as he can).