mito mingi
Senior Member
- Dec 21, 2014
- 196
- 108
Huyo namba moja hataree sana
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
kawa mzuri kweli naweza kumpata?
Hahaa!! Wema kukosekana haiingii akilini lakini hawezi kuwa top kama issue ni East Africa!!Nadhani Sepenga anatakiwa kuwa kama Godfather wao, maana ni balaa yule mtoto hakauki hata humu JF
Ameeeen!! Hebu niwekee ile Aya ambayo huku kitaa tunaipenda sana pale unapoishiwa sound za kuimbisha-- kuna maneno yasemayo "aombae upewa na abishae ufunguliwa!"Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu,Kwa paa na kwa ayala wa porini, Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe.
Wimbo uliobora 2:7
Okay basi iwe ni list ya wakaa uchi sio ya wanaoandikwa sana maana baada ya Oscar Lupita aliandikwa sana
Every Socialite ni maarufu in one way or another but sio maarufu wote ni socialites! Kwa mtazamo wangu Lupita isn't socialite but Wema is! Lupita is just a celebrity. Kwanza socialites wote duniani wana sifa moja inayowaunganisha-- ni attention seekers na wapo tayari kufanya lolote ili mradi tu wapate attention hususani za media!Kama mtu maarufu...
AhsanteEvery Socialite ni maarufu in one way or another but sio maarufu wote ni socialites! Kwa mtazamo wangu Lupita isn't socialite but Wema is! Lupita is just a celebrity. Kwanza socialites wote duniani wana sifa moja inayowaunganisha-- ni attention seekers na wapo tayari kufanya lolote ili mradi tu wapate attention hususani za media!
Hata hivyo ukiwaambia wanatafuta attention ya media, majority watakujibu "sitafuti attention za media bali media zinanitafuta mimi!"
Inaweza ikawa mara ya kwanza kusikia neno”Socialite”,au pengine umeshawahi kusikia mtu akizielezea sifa za mtu kwa kumuita “Socialite person”,ila kwa kifupi “Socialite” ni neno la kingereza linalomwelezea mtu mwenye sifa nyingi ila baadhi ya sifa hizo ni pamoja na kuzungumziwa kwenye vyombo habari mara kwa mara,nguvu ya fedha,kuonekana kwenye matamasha na event mbalimbali za burudani,kujihusisha na masuala ya kijamii ect.Kwa kuzingatia sifa hizo hii hapa ni top ten socialite girls wanazungumziwa na kuandamwa zaidi na vyombo vya habari Afrika mashariki.
10:Hamissa Mobeto
Mrembo huyu ni mwanamitindo aliejipatia umaarufu kwa muda mfupi kwa kuonekana kwenye video kadhaa za mastaa wa bongo fleva kama “Your Mine” ya mwanamuziki Quick Racka na kupelekea watu wengi hasa magazeti ya udaku kumfatilia.
![]()
9:Gigy money
Gigiy Money amejipatia umaarufu kwa miezi ya karibuni kwani licha kupiga picha zanazoonyesha maungo yake,ameonekana kwenye video nyingi za bongo fleva,baadhi ya video hizo ni “I get high” ya rapper Godzila, na”Shika adabu yako”ya Ney wa mitego,mbali kuonekana kwenye video hizo Gigy money ametajwa mara kadhaa kwenye headline za magazeti ya udaku akidaiwa kutoka kimapenzi na baadhi ya mastaa wa muziki.
![]()
8:Vanessa Chittle
Mrembo huyu ambae pia ana kipaji cha muziki,amekua akihost shows mbalimbali jijini Nairobi.Baada ya picha zake za utupu kuvuja kwenye mitandao ya kijamii nchini Kenya alipata umaarufu na kufanya watu wengi hasa magazeti yaudaku kuanza kumfatilia.
![]()
7:Risper Faith
Mrembo huyu mwenye shepu matata,amekua kwenye headline za magazeti ya udaku na mitandao ya kijamii nchini Kenya kwa skendo za kutoka kimapenzi na watu maarufu,mbalina skendo hizo Risper amekua akidai kuwa yeye ni mkirsto na anaamini Yesu ameokoa maisha yake.
![]()
6:Judith Heard
Mbali na kuonekana kwenye video ya Jose Chamilion inayofahamika kama “Vumilia”,mrembo huyu kutoka Uganda nimwanamitindo wa kimataifa na mjasiriamali ambae amekua kwenye headline za vyombo vya habari na mitandao ya kijamii nchini Uganda akidaiwa kutoka kimapenzi na vijana aliowazidi umri
![]()
5:Vera sidika
Mrembo huyu alijipatia umaarufu mara baada ya kuonekana kwenye video inayofahamika kama”You Guy”ya kundi lamuziki la P-Unit iliyotoka mwaka 2012,mbali na video hiyo pia alionekana kwenye video inayofahamika kama “Carry Go” ya Nigerian musician Davido aliyomshirikisha D-Black,licha ya kutokeakwenye video hizo Queen V kama anavyojiita ameonekana kwenye season one ya reality show inayofahamika kama “Nairobi Diaries”.
![]()
4:Huddae Monroe
Mrembo huyu kutoka Kenya alijipatia umaarufu zaidi mwaka 2015 aliposhiriki kwenye shindano la “Big Brother Africa”,ingawa hakushinda ila Huddah ameendelea kubaki kwenye headline za media houses,magazeti ya udaku na mitandao ya kijamii akiwa na skendo za kutoka kimapenzi na watu maarufu na mastaa wa muziki nchini Kenya.
![]()
3:Agness Masogange
Mrembo huyu mwenye shepu inayowatoa wanaume udenda,ameonekana kwenye video kadhaa za bongo fleva kama “Masogange” ya Belle 9 ambayo ilimpatiajina analolitumia mpaka leo,pia alionekana kwenye video inayofahamika kama “Msambinugwa” ya Tunda man f.t Ally Kiba.mbali na kuonekana mara kadhaa kwenye events za burudani,mrembo huyu aliingia kwenye headline za media houses Tanzania na nnje ya nchi mwaka 2013,alipokamatwa na polisi nchini Afrika Kusini akidaiwa kusafirisha kiasi kikubwa cha madawa yakulevya aina ya “Crystal
![]()
2:Zari hassan
Mrembo huyu licha ya kuwa mama wa watoto wanne,watatu wa kiume na wa kike “Princess Tiffa”aliezaa na Mogul Bongofleva star,Diamond Platnumz,ni mfanyabiashara anaemiliki magari kadhaa ya kifahari na nyumba katika nchiza Uganda na Afrika kusini,mahusiano yake na Diamond yamezidi kumfanya afatiliwe na kuzungumziwa mara kwa mara kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
![]()
1:Corazon Hassan
Mrembo huyu msomi aliehitimu masomoya sheria katika chuo kikuu cha Nairobi nchini Kenya,ni mwanamitindo aliejipatia umaarufu mara baada ya picha zake za utupu kuvuja kwenye mitandao ya kijamii,kama ilivyo kwa warembo wenzake Carazon amewahi kutokea kwenye kurasa za mbele za magazeti ya udaku nchini Kenya akihusishwa na za kutoka kimapenzi na watu maarufu na mastaa wa muziki nchini Kenya na kumfanya azidi kuandamwa na mapaparazi kila kukicha.
![]()
Teamtz.com