Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Huko nchini Brazil Influencers wawili wameripotiwa kufariki dunia baada ya kukataa kuvaa Jaketi za kuokoa maisha walipokuwa kwenye boti ya mwendo kasi iliyozama pwani ya Brazil. Walikataa kuvaa jaketi hizo kwa sababu hawakutaka kuharibu mwonekano wao kwenye picha walizokuwa wakipiga kwa ajili ya ku-post kwenye mitandao ya kijamii.
Aline Tamara Moreira de Amorim (37) na Beatriz Tavares da Silva Faria (27), walipuuza kuvaa jaketi hizo za kuokoa maisha wakati walipokuwa wakirudi ufukweni kutoka kwenye party ya kifahari kwenye boti hiyo.
Boti hiyo, iliyokuwa na watu wengi kupita kiasi, ilipinduka baada ya mawimbi makali eneo la "Koo la Shetani" kwenye Mto Iguazu, kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari vya huko.
Kamishna wa Polisi wa Sao Vicente, Marcos Alexandra Alfino, alisema kuwa baadhi ya abiria hawakutaka kuvaa jaketi kwa sababu walikuwa wakipiga selfie.
Soma: Pia:
+ Brazil: Ndege yanye abiria 62 yapata ajali mjini Sao Paulo, hakuna aliyenusurika
+ Brazil: Mahakama Kuu kupiga Kura ya kuamua kama X (Twitter) inastahili kufungiwa