Warere Beach Resort: Zainab Oladehinde alikubaliana na mlinzi kufanya mapenzi. Alitaka tumlipe fidia USD 10,000

Wewe ingekuwa mlinzi ungekataa?hebu tuanzie hapo so ungeona Ndio fursa wewe?
 
Kukubali ama kukataa, hakubadilishi ukweli wowote. Wanaolala na watoto underage kwa sababu ya kushawishiwa na watoto hao, mwishoe ula mvua ya miaka 30 jela. Ushawishi wa mtoto hauwezi kuwa ushahidi wa kumtetea mtu anayelala na mtoto mdogo kisheria. Hivyo hivyo, ushawishi wa mteja wa hoteli, hauwezi kuwa utetezi wa mlinzi anayevunja maadali ya kazi yake. Kama hauna akili ya kuona hilo basi 🙌
Wewe ingekuwa mlinzi ungekataa?hebu tuanzie hapo so ungeona Ndio fursa wewe?
 
Wacha niwe Sina tu akili,but I can't buy this
 
Acheni kudhalilisha utalii toka lini mtalii akatoka Nigeria.
Nigerian ni watafuta fursa
Hakuna matajiri kwa Afrika kama wanigeria asikudanye mtu

Kule kuna ma dangote kibao

Kule ukifika ukitaka kubadilisha pesa dereva taxi anafungua buti ana maburungutu ya minoti kibao ya dollar ,euro'pound na Naira anakubadilishia chap chap

Kule ukipanda daladala usitarajie kuna kibaka atakukwapulia pesa hata mwanae vipi
 
Bila shaka unabisha kitu ambacho huna uelewa nacho.
 
Mmmhm NO! usiwakuze, population ya Nigeria Ni kubwa,matajiri Ni wengi ndio na maskini Ni wengi pia,vibaka wezi na matapeli wapo kibao maana hata Nigeria wao wana Shida ya ajira so kusema huwezi kwapuliwa sio kweli anything can happen.
 

Hii pia ni nigeria
 
Sasa ujanja wa upigaji wametoa wapi kina huspup
 
Kila sehemu yenye matajiri.maskini wapo pia

Mfano Kenya kuna wenye pesa wengi kuliko Tanzania lakini kuna asilimia ya malofa hasa Nairobi
Unaumwa wewe kenya kuna matajiri kuliko bongo? Taarifa zako haziko sawa
 
Nimeona press ya Polisi, naanza kuwa na Imani kwamba tumedhamiria kuilinda Tanzania; hatuwezi kutumia billion kuandaa royal tour then kiumbe Mmoja anayetafuta followers atuhujumu.

Kwa hili tunapaswa kuungana pamoja, alikaa kimya mwaka mzima Leo amemwona Rais yupo USA anaibuka na story. Na hapa ndipo utabaini kwanini ubalozi wake ulimpuuza?

Tusimame imara tusiyumbe Dunia inatufuatilia; tutoke adharani tumwambie atume Mawakili wake waje kutafuta haki la sivyo tuwasiliane na nchi yake aeleze Dola elfu Kumi alizokataliwa kupewa alozitaka za kazi gani?

Huyu amenifanya nisimame imara Sana , tunaonewa Sana Kwa serikali kushindwa kumtetea wawekezaji. Tusimamie haki
 
Kwa hiyo tumefikia stage ya kuwahukumu watu kwa kuwaangalia usoni?

Level ya upumbavu wetu ndo imefika hapa?

Nimetoa solution kwamba justice ipatikane kwa vyombo vya sheria kufanya kazi yake ili mwisho wa siku tujue tatizo liko wapi na litatuliwe. Haki itendendeke.

Hivi mnadhani hiyo solution yenu ya kipumbavu ya kufunika hizi Allegations kwa maneno kama Zanzibar is safe ndio italimaliza hili tatizo lililotokea? Tunaonekana kituko kwenye nchi watu.

Aiseeee hili sakata limeexpose upumbavu uliojaa kwenye vichwa vya watanzania wengi sana. Including wewe.

Hatujasahau enzi watu wanatekwa mlikuwa mnasema wamejiteka.

Watu wanapigwa wanavunjwa miguu mlikuwa mnasema walikuwa wamelewa wakadondoka wakavunjika.

Mpaka ishu ya lisu mlisema aliamua kupigwa risasi ili kutafuta kiki.

Naomba mtu asinihubirie suala la kufunika hili eti kwa kigezo cha uzalendo.

Siwezi upumbavu mimi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…