Duh, Mbona siwaelewi?
Jamani Warioba aliwaita waandishi wa Habari ili awaeleze ufahamu wake kuhusu tuhuma zinazosemwasemwa mitaani na katika baadhi ya vyombo vya habari.
Sasa alichokisema ndicho alichokuwa tayari kukisema. Ndio maana anasema, kama kuna kushitakiwa yuko tayari kujibu mashitaka hayo wakati wowote.
Ndugu zangu, Jaji Warioba ni mtu makini sana. NI mtu anaefikiri kabla ya kusema. Na anasema kinachojitosheleza. Anapotaja Makampuni yenye uwekezaji katika hiyo MWANANCHI Gold anajua anachokisema. Kama unavyojua, Kampuni ina wamiliki wake, na wamiliki wanaweza kuwepo leo, kesho wakauza share zao. Hawezi kutaja tu moja kwa moja wamiliki wa hizo kampuni bila kuwa makini. Yeye kama Jaji anajua umuhimu wa kuhifadhi taarifa za watu (Kama Waziri Mkuu mstaafu, anaijua Katiba). Haikuwa nia yake kwenye kikao kile kisema majina ya watu wowote.
Pili ushiriki wake na Kampuni yake ameusema bayana. Kama unavyojua, Memorandum and Articles of Association za Kampuni yoyote huandaliwa na wana sheria. Kampuni yake ilipewa kazi ya kufanya hivyo, pamoja na ushauri mwingine wa kisheria endapo utahitajika wakati wowote kabla na baada ya kuanzishwa kwa Kampuni hiyo (hii ameisema vizuri katika taarifa hapo juu Sijaona mahali anaposema alikuwa mwendeshaji wa Kapuni hiyo (labda kama kuna mtu anaweza kunisaidia hilo).
Wakuu, nadhani mnajua pia kuwa Serikali imepewa mamlaka na Katiba kupitia Bunge kuanzisha Taasisi, na taratibu zimewekwa za kufanya hivyo. Serikali pia inaweza kuwa na wabia wengine (binafsi au Taasisi za serikali) katika kufikia matarajio ya uanzishwaji wa Taasisi hizo.
Nilidhani mngeshitushwa zaidi na taarifa ya kudidimizwa kwa MWANCHI GOLD ambayo inaelekea ilikuwa na nia ya kuhakikisha rasilimali (madini) yetu yanasafishwa hapa hapa nchini na kutuhakikishia kuwa hatuporwi mali hizo. Mimi kwangu ni jambo la kushtua sana kusikia serikali inakusudia kwa nguvu zote kuua shirika/Kampuni muhimu kama hiyo.