Aliwataja wanahisa wa Kampuni ya Mwananchi Trust, ambayo ipo ndani ya Mwananchi Gold Company Ltd kuwa ni Umoja Entertainment, VNB, WM Holding inayomilikiwa na Yusuph Mushi, na CCM Trust Company.
Alisema katika Kampuni ya Mwananchi Trust, aliyekuwa na hisa nyingi ni Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilichokuwa na hisa 15.
Duh, Mbona siwaelewi?
Jamani Warioba aliwaita waandishi wa Habari ili awaeleze ufahamu wake kuhusu tuhuma zinazosemwasemwa mitaani na katika baadhi ya vyombo vya habari.
Sasa alichokisema ndicho alichokuwa tayari kukisema. Ndio maana anasema, kama kuna kushitakiwa yuko tayari kujibu mashitaka hayo wakati wowote.
Ndugu zangu, Jaji Warioba ni mtu makini sana. NI mtu anaefikiri kabla ya kusema. Na anasema kinachojitosheleza. Anapotaja Makampuni yenye uwekezaji katika hiyo MWANANCHI Gold anajua anachokisema. Kama unavyojua, Kampuni ina wamiliki wake, na wamiliki wanaweza kuwepo leo, kesho wakauza share zao. Hawezi kutaja tu moja kwa moja wamiliki wa hizo kampuni bila kuwa makini. Yeye kama Jaji anajua umuhimu wa kuhifadhi taarifa za watu (Kama Waziri Mkuu mstaafu, anaijua Katiba). Haikuwa nia yake kwenye kikao kile kisema majina ya watu wowote.
Pili ushiriki wake na Kampuni yake ameusema bayana. Kama unavyojua, Memorandum and Articles of Association za Kampuni yoyote huandaliwa na wana sheria. Kampuni yake ilipewa kazi ya kufanya hivyo, pamoja na ushauri mwingine wa kisheria endapo utahitajika wakati wowote kabla na baada ya kuanzishwa kwa Kampuni hiyo (hii ameisema vizuri katika taarifa hapo juu Sijaona mahali anaposema alikuwa mwendeshaji wa Kapuni hiyo (labda kama kuna mtu anaweza kunisaidia hilo).
Wakuu, nadhani mnajua pia kuwa Serikali imepewa mamlaka na Katiba kupitia Bunge kuanzisha Taasisi, na taratibu zimewekwa za kufanya hivyo. Serikali pia inaweza kuwa na wabia wengine (binafsi au Taasisi za serikali) katika kufikia matarajio ya uanzishwaji wa Taasisi hizo.
Nilidhani mngeshitushwa zaidi na taarifa ya kudidimizwa kwa MWANCHI GOLD ambayo inaelekea ilikuwa na nia ya kuhakikisha rasilimali (madini) yetu yanasafishwa hapa hapa nchini na kutuhakikishia kuwa hatuporwi mali hizo. Mimi kwangu ni jambo la kushtua sana kusikia serikali inakusudia kwa nguvu zote kuua shirika/Kampuni muhimu kama hiyo.
Kampuni ya Umoja inamilikiwa na familia ya Warioba, kampuni ya VMB inamilikiwa na familiaya Mahalu, kampuni ya YM inamilikiwa Yussuf Mushi, kampuni ya CCM Trust wenye hisa ni Warioba na Yussuf Mushi na si wadhamini wa CCM. Kazi kwenu
Kampuni ya Umoja inamilikiwa na familia ya Warioba, kampuni ya VMB inamilikiwa na familiaya Mahalu, kampuni ya YM inamilikiwa Yussuf Mushi, kampuni ya CCM Trust wenye hisa ni Warioba na Yussuf Mushi na si wadhamini wa CCM. Kazi kwenu
Warioba afichua siri nzito
• Aitaka serikali iharakishe kumpandisha kizimbani
na Happiness Katabazi
Tanzania Daima~Sauti ya Watu
Aliwataja wanahisa wa Kampuni ya Mwananchi Trust, ambayo ipo ndani ya Mwananchi Gold Company Ltd kuwa ni Umoja Entertainment, VNB, WM Holding inayomilikiwa na Yusuph Mushi, na CCM Trust Company.
Alisema katika Kampuni ya Mwananchi Trust, aliyekuwa na hisa nyingi ni Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilichokuwa na hisa 15.
Mwanakijiji said:a. Kampuni ya Nyalali, Warioba na Mahula (mmoja aliwahi kuwa Jaji Mkuu, mwingine Waziri Mkuu, na mwingine Balozi) inaweza vipi kufanya biashara na taasisi kama Benki Kuu bila kuwa na aina fulani ya insider information n.k? At that time ilikuwa ni muda gani tanu Nyalali atoke Ujaji Mkuu?
Mashtaka yatakuwa kujiandikisha kama wao ni CCM Trust wakati CCM haikuwapa ruhusa hiyo. CCM kama ingetaka kuwa na hisa au trust wangeweza kufanya kwa namna tofauti. Aulizwe Makalla kama wanaitambua CCM Trust Company ya kina Warioba na Mushi. I bet my last nickel kwamba CCM watawaruka!
Kwa sababu sidhani kama watapata dondoo za kikao chochote kilichounda au kuidhinisha CCM trust kufanya kazi na Mwananchi Gold.
".... serikali ilikuja kwenye ofisi yetu ya uwakili ya Nyalali, Warioba & Mahalu Law Associates ili tuisaidie kuipatia huduma ya kisheria kabla na baada ya kuundwa kwa kampuni hiyo."
PUBLIC PROCUREMENT ACT 2004-21
Sect 44 (1), 66 (1), 67 (4), 63 (1), 56 (1)
Duties of procuring entities
44.-(1) Notwithstanding anything to the contrary contained in any written law, where any expenditure is to be incurred on any procurement of goods, works or services, it shall be the duty in respect of a head of expenditure to ensure that such procurement of goods, works or services is in accordance with the procedures prescribed by or under this Act or Regulations.
66.-( 1 ) The tender board … shall receive tenders using procedures set out in the Regulations made under this Act.
67.-( 4) The procuring entity shall prepare a detailed report on the evaluation and comparison of tenders, setting out the specific reasons on which its recommendations for the award of each contract are based.
63.-( 1) The procuring entity shall use the appropriate standard model tender documents specified in the Regulations for the procurement in question…shall be worded so as to permit and encourage competition and such documents shall set forth clearly and precisely all the information necessary for a prospective tenderer...
Records, Information and Notices
56.-( 1 ) Each procuring entity and each approving authority shall maintain a record of procurement proceedings in which each is involved, including decisions taken and the reasons for it and such record shall be kept for a period of not less than five years
.......hata kwenye hiyo namba {1} bado Warioba ana maswali mengi ya kujibu:...
{1}Jaji Warioba alihusika kupitia kampuni yake kutoa ushauri wa kuanzisha mwananchi.Mpaka hapo sina tatizo na mzee wetu Warioba kwasababu hiyo ni kazi yake.
Naona kuwa Waryoba yuko matatani kabisa, na sidhani kama atakwepa. Ninaanza kuelewa kwa nini alikuwa akitetea watu wasimsakame Mkapa. Inaelekea Mkapa alimgawia kitu hiki ili anyamaze asiendelee kupiga kelele kuhusu ile ripoti yake ya rushwa halafu akaibugia bila hata kunawa mikono. Mkapa alikuwa na namna ya kuwanyamazisha wanasiasa wa aina yake kama akina Mzindakaya, na nadhani alitumia njia hiyo hiyo kumnyamazisha huyu Waryoba, lakini sasa atakuwa amekalia makaa ya moto.
Najaribu kufikiri jinsi gani Bwana Nalaila Kiula, George Mlingwa na Bwana Stephen Wassira (mgomvi wake wa kisiasa kwa kiti cha Bunda) watakavyofurahi kumwona jamaa akipelekwa keko!!
maelezo yake yamejikanganya sana halafu mtu ukipitia rekodi zilizoko kuhusiana na sakata hilo ndipo unagundua kuwa Mzee yuko matatani. Iweje kweli serikali "iiombe" kampuni yake binafsi ya sheria "kusaidia" uanzishaji wa kampuni hiyo ambayo baadaye ilipewa fedha na benki kuu katika "utaratibu usio wa kisheria" na baadaye kampuni hiyo inayeyuka bila kulipa fedha za umma kinyume cha sheria?
Halafu basi baada ya serikali "kumwomba" atoe huo ushauri wa kisheria kuisaidia kampuni hiyo mpya, inakuwaje kampuni hiyo iliyoanzishwa kwa maelekezo ya serikali inakuwa na wabia ambao ni makampuni ya watu binafsi tu, na tena mwenyekiti wa bodi yake akiwa ni yeye huyo huyo Waryoba?
Maswali ya kutatanisha yanazidi kuwa mengi, ngoja mimi niwahi kiti pale kisutu kusudi niweze kumsikiliza mzee wa sheria akijitetea.
Warioba?? former prime minister? mwanasheria mahiri?
Si mramba huyu au Yona, pia sijaona bado alipojichanganya wapi, labda nisaidie!