WARIOBA na rekodi yake akiwa Waziri Mkuu

WARIOBA na rekodi yake akiwa Waziri Mkuu

Nami Nakubali Kuwa Sokoine Na Julius Kidogo Na Salim....ingawa Hakukaa Sana...warioba Hapana..........

Dah! Sasa huyu mzee tunayemwita Simba Wa Vita je? Kwa sababu hio nickname nzito hio....yeye ana nafasi gani? Au labda kwa sababu alianza career yake kama actor,hatumuoni serious? kwi..kwi...kwi!
 
Simba wa Vita alikuwa "Yes Man" wa Nyerere tu.Sokoine alikuwa an overzealous ideologue. Warioba is an intellectual more adept at conducting studies ,writing reports and playing the eldery statesman part but he was probably the best of the bunch, regardless of the fact he was trumped up by Butiama as a Nyerere button on the remote control aimed at Mwinyi.

Problem is if you go by rule of law as opposed to "rule of politics" (as coined by FMES) in bongo, you end up looking irrelevant to the CCM stalwarts who value party dominance than country, exactly like the Warioba predicament now .
 
Kwa jinsi unavyomkumbuka Edward Ngoyay Lowasa, reverse ya kumbukumbu zako zitamfit Warioba
 
Kwa kuchapwa viboko kijijini kwao Ikizu kwa kushindwa kujenga kwao huku akijenga nyumbani na kwao mke wake.
 
Not so sure lakini nasikia ni mmoja wa waliochangia kididimiza TTCL...na kufacilitate ile deal ya kiini macho ya Celltel (Zain/Airtel) ndani ya TTCL
 
Hivi ni yule bwana ambaye zama zile akiwania ubunge alimwekea zengwe kijana mpinzani wake hadi akapigwa transfer ya chapchap toka jimboni.
Au ndiye aliyekuwa akilia mbwamwitu mbwamwitu eti serikali inataka kumkamata kuhusiana na kampuni tata yakusafisha madini ikimhusisha yeye Nyalali akina Mahalu na kampuni ya Kiitaliano.
Na kesi ya kijana wake & CO. wa manispaa ya Kinondoni kuhusiana na ugawaji viwanja kinyume na taratibu iliishaje?
In short kwa hawa si rahisi kuwatofautisha, mjini wanasema ni haohao waliokunywa uji wa mgonjwa na mgonjwa akafariki.
 
Not so sure lakini nasikia ni mmoja wa waliochangia kididimiza TTCL...na kufacilitate ile deal ya kiini macho ya Celltel (Zain/Airtel) ndani ya TTCL


Hivi bado si mjumbe huyu kwenye ile bodi ya Airtel?.
 
Atakumbukwa kwa kuwa kiongozi wa ngazi mbalimbali kubwa nchini bila kuhusishwa na ufisadi, pamoja na kwamba hakuna kumbukumbu nzuri ya jinsi uongozi wake ulivyokuwa mzuri kwa taifa.
 
Namkumbuka kama mmoja aliyesimama kuishauri serikali kukaa na CUF wakati wa Mkapa na kuwa wakitaka wanaweza kuepusha mauji yaliyokuwa yanaenda kutokea Zanzibar- hii ni kabla ya yale maandamano - serikali haikumsikiliza na kweli wananchi wakapoteza maisha halafu serikali ikakubali kufanya lilelile walilokataa- Kukaa na CUF

Kwa hili nilimkubali kwa ujasiri na maono yake
 
Jaji Warioba yuko juu sana, ila ukweli ni kwambam uovu unavuma sana zaidi ya wema.
Angekuwa ametenda uovu jina lake lingekuwa kubwa sana kwa uovu wake, lakini kwa kuwa si muovu jina lake limebakoi liki play low profile
 
Nadhani hakuwa mbaya sana ndio maana hata hajulikani sawasawa, ila kwa kuwa ni wa chama cha magamba ndio maana kikombe hiki hakimuepuki.
 
Warioba hajawahi kuwa jaji wa mahakama za Tanzania. Anaitwa Jaji kwa heshima ya kuwa mjumbe wa kimataifa wa Dodi inayosikiliza kesi zinazohusu sheria za kimataifa za baharini. Wajumbe wa bodi hiyo wana hadhi ya Ujaji. Ni mtaalamu wa kimataifa wa sheria za bahari
 
Je Watanzania tutamkumbuka kwa kipi?

... kwa kumtafutia mwanawe CHEO kwa kutumia kila aina ya mbinu ambazo ni pamoja na kumharibia ndugu yake na rafiki wa karibu! Sijui Kippi ataukwaa lini huo UDC
 
Angekuwepo Mwl Nyerere akaulizwa hili swali,
Asingilijibu, angebinua binua mdomo wake, alafu akaangalia angalia watu wa pembeni yake
alafu angecheka saaaana.

Nadhani angeeleweka
 
Ni mzee na anaheshimika sana,lakini nimepekua historia ya uongozi wake kisiasa sijaona legacy yake kwa nafasi kubwa aliyokuwa nayo huyu Mzee.

WanaJF naomba kujua ya huyu Mzee katika Taifa letu.
 
..huyu nafikiri alifanya kazi yake kwa kufuata sheria, bila makeke...pia inaelekea aliondoka na heshima zake. ndiyo maana hana uwoga kuizungumzia rushwa au kuwanyooshea kidole wala rushwa...najua kwa Tanzania si rahisi kukuta mwanasiasa asiye na mawaa, lakini kwa standards zetu, Sinde Warioba anaelekea kuwa msafi.NB:..IS HE THE BEST PRIME MINISTER WE HAVE EVER HAD?
Kwangu mie the best PM bado ni Edo Sokoine.
 
Huwa najiuliza kwa nini huyu Warioba hakuendelea kuwa waziri mkuu wa mzee Ruksa kwa kipindi cha miaka 10.Anaongea vitu vinaeleweka kuhusu Muafaka kuliko Babu wa Kilwa na Mgosi,Je Ruksa aliogopa kuwa huenda angeweza kugombea Urais awamu ambayo ilifuata kama kawaida ya wanaomaliza uwaziri mkuu hugombea U rais?Huyu jamaa ndo waziri wa kwanza kuundiwa wizara hii ya TAMISEMI ambayo iliundwa kipindi cha Ruksa.Hata kupata ubunge kule Bunda mkoani Mara kipindi fulani ilikuwa mbinde maana waliendeshana na Stephen Wassira alipokuwa amehamia NCCR-MAGEUZI.Naona baada ya kukosa U waziri mkuu kipindi cha pili,mambo yalimwendea kombo sana ktk duru za siasa.Hiki kichwa bado tunakihitaji kwa maendeleo ya Taifa hili
Tanzania hii ni Mwalimu Nyerere pekee ambaye ni Waziri Mkuu aliyepata kuwa rais. MaPM wengine wote hawakufanikiwa sijui ni kwa nini.By the way, napenda kufahamu sana ilikuwaje Mwinyi hakumteua tena awamu iliyofuata? Badala yake akamteua Jumanne Malacela?
 
Back
Top Bottom