WARIOBA na rekodi yake akiwa Waziri Mkuu

WARIOBA na rekodi yake akiwa Waziri Mkuu

mzee wetu Warioba Mungu ampe rehema maana si madogo aliyofanya bali ni mengi sana tutazidi kupokea mapendekezo na njia mbalimbali ulizotumia hta watawala wetu natakiwa kuinga mambo muhimu wa sio dhambi.
 
Mhe Jaji Joseph Sinde Warioba alipata kuwa Mwanasheria mkuu na baadae Waziri mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais. Kwa muda mrefu amekuwa akijitokeza kwenye vyombo vya habari, Jee ana kipi cha kujivunia (legacy) kwamba katika uongozi wake watanzania wanaweza kumkumbuka kwayo. Mimi namwona ni mchumia tumbo tuu kupitia siasa...
Yapo machache ni aibu kwake
1.Mwananchi Gold Mine...
2.Visasi dhidi ya wabaya wake hususan Kiula alipokuwa mwenyekiti Tume ya Rushwa...
3. Kiongozi mlevi na mvuta sigara...

Lengeri
 
I don't know much about Warioba but this much I know, Warioba si mlevi, anakunywa wine socially tu. Na kuhusu sigara ( na hata unywaji/ ulevi) sie tukichagua kiongozi hatuchagui Papa wa kanisa katoliki. Na kwenye katiba hatukatazwi kunywa au kuvuta sigara.

Ukienda viwanja vingine mwanamme kama hunywi watu wanaweza kukushangaa, kwa hiyo hili swala ni subjective na as long as halijaingilia utendaji sioni umuhimu wake.

Maswali 1 na 2 yanaweza kuwa na hoja.
 
Warioba ana mengi ya kujivunia katika uongozi wake.

Kwanza kabisa suala la Mwananchi Gold Mine limetumiwa vibaya dhidi yake. Lengo lilikuwa ni kujenga kiwanda cha kusafisha dhahabu ndani ya Tanzania badala ya kuisafirisha nje kama inavyofanyika hivi sasa lakini utawala wa sasa ukapinga kwa sababu walikuwa na maslahi maalumu katika dhahabu inayosafirishwa nje. Hilo moja.

Pili, Warioba alishiriki sana katika uanzishaji wa mikataba ya Law of the Sea katika Umoja wa mataifa.

Kuhusu Kiula anayestahili kulaumiwa zaidi ni Mkapa ndiye aliyemfungulia kesi. Haikuwa kisasi kwa sababu Warioba hakuwa na mvutano wowote na Kiula. Na mwisho, haya mambo ya uvutaji sigara au kunywa bia ni personal. Hayahusiana vyovyote vile na utendaji kazi na legacy.

Na kabla sijasahau, wakati akiwa mwanasheria mkuu alimnusuru Nyerere katika skendo la kisheria pale alipomteua Chediel Mgonja kuwa mkuu wa mkoa huku akiwa amepigwa marufuku kutogombea uchaguzi kwa miaka mitano. Uamuzi huo ulitangazwa Warioba akiwa New York ikabidi aahirishe safari na kurudi na kumwambia Nyerere kuwa amemchagua Mgonja kwa makosa.

Kama una kisa na Warioba tafuta jingine.
 
Hao ndo kundi la wale wanaonesha mbwembwe wakiwa nje ya system,huyu jamaa alivuliwa ubunge wa bunda na mzee wasira kwa tuhuma za rushwa mahakaman
 
Back
Top Bottom