Nami Nakubali Kuwa Sokoine Na Julius Kidogo Na Salim....ingawa Hakukaa Sana...warioba Hapana..........
Not so sure lakini nasikia ni mmoja wa waliochangia kididimiza TTCL...na kufacilitate ile deal ya kiini macho ya Celltel (Zain/Airtel) ndani ya TTCL
Je Watanzania tutamkumbuka kwa kipi?
Kwangu mie the best PM bado ni Edo Sokoine...huyu nafikiri alifanya kazi yake kwa kufuata sheria, bila makeke...pia inaelekea aliondoka na heshima zake. ndiyo maana hana uwoga kuizungumzia rushwa au kuwanyooshea kidole wala rushwa...najua kwa Tanzania si rahisi kukuta mwanasiasa asiye na mawaa, lakini kwa standards zetu, Sinde Warioba anaelekea kuwa msafi.NB:..IS HE THE BEST PRIME MINISTER WE HAVE EVER HAD?
Tanzania hii ni Mwalimu Nyerere pekee ambaye ni Waziri Mkuu aliyepata kuwa rais. MaPM wengine wote hawakufanikiwa sijui ni kwa nini.By the way, napenda kufahamu sana ilikuwaje Mwinyi hakumteua tena awamu iliyofuata? Badala yake akamteua Jumanne Malacela?Huwa najiuliza kwa nini huyu Warioba hakuendelea kuwa waziri mkuu wa mzee Ruksa kwa kipindi cha miaka 10.Anaongea vitu vinaeleweka kuhusu Muafaka kuliko Babu wa Kilwa na Mgosi,Je Ruksa aliogopa kuwa huenda angeweza kugombea Urais awamu ambayo ilifuata kama kawaida ya wanaomaliza uwaziri mkuu hugombea U rais?Huyu jamaa ndo waziri wa kwanza kuundiwa wizara hii ya TAMISEMI ambayo iliundwa kipindi cha Ruksa.Hata kupata ubunge kule Bunda mkoani Mara kipindi fulani ilikuwa mbinde maana waliendeshana na Stephen Wassira alipokuwa amehamia NCCR-MAGEUZI.Naona baada ya kukosa U waziri mkuu kipindi cha pili,mambo yalimwendea kombo sana ktk duru za siasa.Hiki kichwa bado tunakihitaji kwa maendeleo ya Taifa hili