Warioba:Tanganyika ina shutumiwa kwa kuvaa koti la Muungano na kufanya Tanzania ndiyo Tanganyika

Warioba:Tanganyika ina shutumiwa kwa kuvaa koti la Muungano na kufanya Tanzania ndiyo Tanganyika

Kilasi Mkuu

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2013
Posts
2,325
Reaction score
723
Mzee Warioba amesema zipo shutuma kwamba Tanganyika ilijivua na kuvaa koti jipya la muungano ambalo hapana shaka Tanzania bara kuonekana kufaidi matunda ya muungano kuliko Wazanzibari hata kupelekea Tanzania kuonekana ndiyo ile Tanganyika iliyo kufa.

Hali hiyo ndiyo inayofanya ongezeko la kero za muungano.Kwa maneno yake Wazanzibari wanaona ni ujanja tu ulitumika kuinyang'anya mamlaka yake Zanzibar nakisha kuiua kabisa na labda ndiyo chanzo cha hali duni za maisha ya Wazanzibari.

Wangetamani wajiunge na umoja wa nchi kama OIC unaojumuisha nchi za kiislamu hatua ambayo ingebadili kipato chao lakini haiwezekani kwakuwa koti linavaliwa Bara kwa mgongo wa muungano.

amesema tume yake ime angalia options nyingi ili kuondosha Muonekano huo lakini imeshindwa kupata balikurejesha pendekezo la kwenye rasimu ya kwanza la serikali tatu.

Ame chukua muda mrefu hadi kuchosha kuelezea hilo naona baaba ya kuhisi ccm wasinge taka hata kusikia serikali tatu.Kwakweli ameonyesha kuwa Wazanzibari walikuw wanataka kitu kingine siyo serikali mbili tena kitu ambacho ni mwiba kwa ccm.

Na hadhani kama wangetaka serikali moja kwani hiyo ni kuimeza kabisa Zanzibar.amesema zaidi ya 60%ya Watanzania Bara walitaka tatu hali kadhalika huko Zanzibar.

Nakiasi kikubwa Zanzibar walitaka muungano wa mkataba.

Tupo katika takuli kubwa wa kuu hali ndiyo hiyo
 
Siyo kushutumiwa ni ukweli usiopingika kuwa serikali ya Tanzania ndio hiyo hiyo serikali ya Tanganyika anayebisha aje na ushahidi.
 
Naunga mkono serikali tatu Na huo muungano sioni faida zake uvunjwe tu
Unachotaka kueleza hapa nini. Haiwezekani uunge mkono serikali 3 at the same time usitake muungano. Tunaounga mkono serikali 3 tunahitaji muungano, ila tunataka uwe modified kuondoa au kupunguza kero.

Wewe kama huungi mkono muungano basi hii katiba ya Jaji warioba haikuhusu maana ni katiba ya muungano.

Wewe unachotakiwa kudai ni kuvunja muungano na kutaka kila nchi iandae katiba yake kivyake.

Nina mashaka kama unajua nini kinaendelea.
 
Unachotaka kueleza hapa nini. Haiwezekani uunge mkono serikali 3 at the same time usitake muungano. Tunaounga mkono serikali 3 tunahitaji muungano, ila tunataka uwe modified kuondoa au kupunguza kero.

Wewe kama huungi mkono muungano basi hii katiba ya Jaji warioba haikuhusu maana ni katiba ya muungano.

Wewe unachotakiwa kudai ni kuvunja muungano na kutaka kila nchi iandae katiba yake kivyake.

Nina mashaka kama unajua nini kinaendelea.
Umeishawahi kaa na wazanzibari mkaongea kuhusu muungano ukasikiliza maoni yao?
 
Naunga mkono serikali tatu, hata hao wabunge wa bunge la katiba wawe wasikivu na waelewa.

Binafsi namkubali mbunge wangu Mnyika najua hatapindisha hoja hii kwa kuwa wananchi wake wa ubungo tumemtuma akapitishe serikali tatu.

Je mbunge wako ni msikivu kama wangu wa ubungo? ?
 
Naunga mkono serikali tatu Na huo muungano sioni faida zake uvunjwe tu

What kind of an opinion is this? Plastic brains!

chris-jestina-na-wadau-wengine-wakikusanya-misaada-mbalimbali.jpg
 
At this point, the question is not if the union will collapse, the question is when will the union collapse.

Kizazi kilichouenzi muungano kinaisha, na hata watu wa bara, ambao mara nyingi ndio wamekuwa watetezi sana wa muungano, wanaanza kujiuliza, hivi is this union really worth all the trouble?

Mimi nilishasema siku nyingi. Ipigwe kura ya maoni, ili muungano uendelee iwe lazima upate simple majority both sides.

Ukipata hiyo simple majority, serikali inapata mandate ya watu, na yeyote atakayerudia habari za kuvunja muungano achukuliwe hatua.

Ukikosa hiyo simple majority, uvunjwe, na tuanze Balkanization yetu vizuri.
 
Naunga mkono serikali tatu Na huo muungano sioni faida zake uvunjwe tu


tunazunguka sana ila suluhisho ni serikali moja na znz iwe mkoa rasmi au muungano uvunjwe tukutane EAC,kwa hali hii matatizo yatajirudia tena na znz wataendelea kulalamika wanataka mamlaka kamili
 
Naunga mkono serikali tatu Na huo muungano sioni faida zake uvunjwe tu
Lukosi watu walikuwa wanakubeza kumbe pia ni mzalendo, hapo pia nakuunga mkono. Japo kuwa umerudi ccm labda kwa faida ya biashara zako, lakini bado unaonyesha kuwa una damu ya mageuzi(revolution) ila huja pata chama kinacho kulidhisha. Hata hivyo kwa sasa bado nitasema kuwa unadamu ya cdm, ccm unaiunga mkono ili biashara zako ziende vizuri. Najua baadae utarudi tu.
 
Marais 3!!!!!! what a nice chance to become a president one day
 
Tutakuwa viziri mjini hapa kwa ving'ora vya misafara ya maraisi wa 3.....sasa wakiwa watembezi kama huyu bado watakuwa wanagongana angani

Ha ha ha ha ha aaa,Mkuu unanivunja mbavu hapa,mmoja tu tuliambiwa tutakula nyasi,sasa watutu Si tutaambiwa tujile wenyewe!
 
Tatizo hakuna kiongozi jasiri anayetaka muungano uvunjikie kwenye uongozi wake. Tumebaki na wadhaifu ambao agenda yao (zao) ni kurithisha watoto wao watawale.
 
Naunga mkono serikali tatu Na huo muungano sioni faida zake uvunjwe tu
Duhm kazi kwelikweli! sasa umeongea nini?

Unapounga mkono serikali tatu maana yake unaunga mkono na serikali ya tatu ya Muungano wa shirikisho lenye Tanganyika na Zanzibar.

Halafu unasema muungano huoni faida yake na uvunjwe! Sasa kauli yako ya kwanza inamaanisha nini?

Try to shake your head before use!
 
Back
Top Bottom