Warioba: Wananchi tunaowaita Wanyonge ndio wenye nchi, Katiba ni kipaumbele hata kwenye marekebisho Bungeni

Kipengele kimojawapo cha katiba ni wabunge wa viti maalum. Katiba mpya inapaswa kuondokana na wabunge wote wasiochaguliwa na wananchi.

Katiba iliyopo inamtaka Spika kuwajibika kwa Rais. Katiba mpya inapaswa kuondoa takwa hilo na kulifanya bunge kuwa mhimili kamili unaojitegemea.

Cheo cha Spika wa bunge kilindwe hata kama ataondolewa uanachama wake.

Katibu wa bunge ambaye ni mtendaji mkuu wa bunge anapaswa kuteuliwa na Spika sio Rais kama ilivyo sasa.

Katiba mpya iondoe uwezo wa Rais kulivunja bunge katika mazingira yoyote yale.

Rais aondolewe uwezo wa kuitisha bunge wakati wowote.
Nchi ngumu hii,

Watu wanataka kubadili Katiba ambayo hata hawaifahamu...
 
Meneja wa hicho kipindi ITV ajiandae kupokea Amri kutoka juu.

Patamu hapa
 
Iwe tunaifahamu iwe hatuifahamu tunataka kudhibiti umagufulism
 
Harakati za Katiba Mpya zimefika patamu
 
Hapa ndipo ujinga wetu waTz ulipo mtu akitaja tu katiba ni lazima irekebishwe tayari wanamuamini.

Huyu warioba kaishi na hito katiba kwa muda mrefu na ameitumikia kwanini hakujiuzuru kuwa katiba haifai?..
Hawa wazee siyo wanafiki, kwa sababu walizunguka nchi nzima kukusanya maoni ya wananchi, na waliyaandika kama yalivyo, sidhani kama waliyachakachua
 
Watambambikia kesi chokochoko zake ni UCHOCHEZI wa kutaka kuleta vurugu nchini hivyo kupewa house arrest 24/7 au hata kutupwa lupango.

Hahaha patachimbika. Makonda aliyempiga Ngumi hayupo je Shaka ataweza?
 
Hapo ndio hata Mimi si-ulewi unafiki wa Hawa wazee wastaafu.Ukweli huu mlitakiwa muuseme mkiwa huko madarakani,Hapo ndo mngeonekana mashujaa.Kwa Sasa hata mkishauri hampewi kipaumbele na walio madarakani maana wanajua Hamna Tena uwezo wa kuwafanya lolote.Hata Sisi wananchi wa kawaida wenye uelewa,ushauri wenu hatuupi umuhimu maana mlitusaliti mlipokuwa na vyeo vyenu.
Hapa ndipo ujinga wetu waTz ulipo mtu akitaja tu katiba ni lazima irekebishwe tayari wanamuamini.

Huyu warioba kaishi na hito katiba kwa muda mrefu na ameitumikia kwanini hakujiuzuru kuwa katiba haifai?...
 
Hapa ndipo ujinga wetu waTz ulipo mtu akitaja tu katiba ni lazima irekebishwe tayari wanamuamini.

Huyu warioba kaishi na hito katiba kwa muda mrefu na ameitumikia kwanini hakujiuzuru kuwa katiba haifai?...
Uwe mpole. Hata nchi walizobadilisha katiba zao waliobadilisha katiba za zamani ni walewale walioapa kuzilinda katiba walizoapa kuzilinda na hawakuitwa wanafiki. Ni kwa sababu ya mabadiliko ya nyakati na uhitaji ndivyo vilivyowasukuma kuleta na kuridhia mabadiliko.
 
Hapa ndipo ujinga wetu waTz ulipo mtu akitaja tu katiba ni lazima irekebishwe tayari wanamuamini.

Huyu warioba kaishi na hito katiba kwa muda mrefu na ameitumikia kwanini hakujiuzuru kuwa katiba haifai?..
Acha kupanick dogo.
 
Reactions: BAK
Nchi ngumu hii,

Watu wanataka kubadili Katiba ambayo hata hawaifahamu
Hata hii iliyopo inafahamika na wachache. Kama issue ni kufahamika na wengi basi hata hii haifai.
 
Reactions: BAK
Wanafiki watupu walioweka mbele matumbo yao. Hawaoni mbali kwamba hili janga kubwa wanaloliruhusu liendelee nchini litavigusa hata vizazi vyao vijavyo. Nchi ina miaka 60 toka ipate huru, rasilimali chungu nzima lakini katika sekta zote hakuna chochote kile cha KUJIVUNIA.

Ni ubabaishaji tu, uhuni na janja janja huku kundi dogo ambalo halifiki hata 1% ya population likiwa mamilionea na mabilionea huku asilimia kubwa ikiishi katika ufukara wa kutisha kwa miaka nenda miaka rudi.

Baada ya shibe hadi kuvimbiwa wanatapikia wananchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…