Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Kipengele kimojawapo cha katiba ni wabunge wa viti maalum. Katiba mpya inapaswa kuondokana na wabunge wote wasiochaguliwa na wananchi.
Katiba iliyopo inamtaka Spika kuwajibika kwa Rais. Katiba mpya inapaswa kuondoa takwa hilo na kulifanya bunge kuwa mhimili kamili unaojitegemea.
Cheo cha Spika wa bunge kilindwe hata kama ataondolewa uanachama wake.
Katibu wa bunge ambaye ni mtendaji mkuu wa bunge anapaswa kuteuliwa na Spika sio Rais kama ilivyo sasa.
Katiba mpya iondoe uwezo wa Rais kulivunja bunge katika mazingira yoyote yale.
Rais aondolewe uwezo wa kuitisha bunge wakati wowote.

Nchi ngumu hii,
Watu wanataka kubadili Katiba ambayo hata hawaifahamu...