Warioba: Wananchi tunaowaita Wanyonge ndio wenye nchi, Katiba ni kipaumbele hata kwenye marekebisho Bungeni

Hapa ndipo ujinga wetu waTz ulipo mtu akitaja tu katiba ni lazima irekebishwe tayari wanamuamini.

Huyu warioba kaishi na hito katiba kwa muda mrefu na ameitumikia kwanini hakujiuzuru kuwa katiba haifai?

Werema naye mnafiki tu kwani aliapa kuilinda katiba ileile mbaya,why?

Leo wanajifanya kukosoa katiba iliyopo ni wanafiki na viongozi wengi ni wanafiki ktk hili

Hapa kumekuwa na:

1. watu wanabambikizwa kesi,
2. watu wakishilikiliwa kutokana na kubambikiziwa kesi
3. watu wakishilikiliwa na hata kuachiwa kwa uonevu bila ya wahusika kuwajibika,
4. kuingiliwa kwa mihimili mingine ya kiutawala kiutendaji,
5. Nk nk

Bado wewe huoni umuhimu wa marekebisho bali unataka tukuamini wewe kuwa katiba haihitaji marekebisho?

Kwa mnafiki ni Warioba ila wewe?!
 
Aliyekuwa mwenyekiti wa Tume ya Katiba mpya Jaji Warioba amesema wananchi hawa wanaoitwa " Wanyonge" ndio wenye nchi.

Warioba amesema Rais Samia amesimama imara kwenye utendaji wake baada ya kifo cha hayati Magufuli na amekubali kushughulikia suala la katiba mpya.

Jaji Warioba amesema kuna mambo ya katiba ambayo yanaweza kupelekwa bungeni na kufanyiwa marekebisho kama ambavyo sheria ya mawasiliano inafanyiwa ammendmends mara kwa mara.

Cha ajabu tunaambiwa mawasiliano ni " kipaumbele" na sisi tunasema katiba ni kipaumbele.

Mahojiano ya Jaji Warioba yatarushwa jumatatu ITV kipindi dakika 45.

Source: ITV habari!

Nawasalimu kwa jina la JMT.

Wanazoziita ni chokochoko tutaelewana tu.
 
"... ni heri mkawapa wananchi katiba mpya wakati hawaihitaji kuliko kusubiri wakaidai". Haya maneno yamejaa busara na hekima nyingi sana japo sikumbuki yalitamkwa na nani.

Haaaaaa haaaaa nilisikia maneno haya yakitamkwa maeneo ya jalala kuu sijui siku hizi bado lipo au linehamishwa.
 
Hicho kipindi kwa kauli ya jana ya Rais, sidhani kama kitarushwa tena, maana labda ndo itakuwa moja ya ' chokochoko'..... itabidi vyombo vya habari viwe makini kuzungumzia hiyo issue ya katiba, maana naona inaonekana kama' chokochoko'..chonde vyombo vya habari msijepata matatizo katika kipindi kile aisee ....... kazi iendelee.
Meneja wa hicho kipindi ITV ajiandae kupokea Amri kutoka juu.

Patamu hapa
 
Aliyekuwa mwenyekiti wa Tume ya Katiba mpya Jaji Warioba amesema wananchi hawa wanaoitwa " Wanyonge" ndio wenye nchi.

Warioba amesema Rais Samia amesimama imara kwenye utendaji wake baada ya kifo cha hayati Magufuli na amekubali kushughulikia suala la katiba mpya.

Jaji Warioba amesema kuna mambo ya katiba ambayo yanaweza kupelekwa bungeni na kufanyiwa marekebisho kama ambavyo sheria ya mawasiliano inafanyiwa ammendmends mara kwa mara.

Cha ajabu tunaambiwa mawasiliano ni " kipaumbele" na sisi tunasema katiba ni kipaumbele.

Mahojiano ya Jaji Warioba yatarushwa jumatatu ITV kipindi dakika 45.

Source: ITV habari!

Nawasalimu kwa jina la JMT.
Wahuni ndio walimtuma Yule asiye na Radhi ya wazazi wake kumpiga huyu Mzee. RC wazamani wa DSM
 
Hicho kipindi kwa kauli ya jana ya Rais, sidhani kama kitarushwa tena, maana labda ndo itakuwa moja ya ' chokochoko'..... itabidi vyombo vya habari viwe makini kuzungumzia hiyo issue ya katiba, maana naona inaonekana kama' chokochoko'..chonde vyombo vya habari msijepata matatizo katika kipindi kile aisee ....... kazi iendelee.
mmeanza mambo yenu. acha hisia jana Rais hajasema chokochoko ni za nini
 
Hapa ndipo ujinga wetu waTz ulipo mtu akitaja tu katiba ni lazima irekebishwe tayari wanamuamini.

Huyu warioba kaishi na hito katiba kwa muda mrefu na ameitumikia kwanini hakujiuzuru kuwa katiba haifai?

Werema naye mnafiki tu kwani aliapa kuilinda katiba ileile mbaya,why?

Leo wanajifanya kukosoa katiba iliyopo ni wanafiki na viongozi wengi ni wanafiki ktk hili
Wamefanya kazi chini ya hiyo katiba na wanaona ina mapungufu makubwa na kuna haja yakuandikwa upya sasa unafiki wao uko wapi?.Uungwana ni kueleza mapungufu ya jambo lolote unaloliona haliko sawa,ata kama ukulisema jana leo nayo ni siku unaweza kulisema.
 
Nchi ngumu hii,

Watu wanataka kubadili Katiba ambayo hata hawaifahamu ,

Yaani hiyo wanayosema wanataka ibadilishwe ni wachache sana wanaoifahamu kwa mapana yake,

Na ndio hao wanaowadanganya kundi kubwa ambalo haliifahamu vyema.

Kelele za Katiba Mpya zimeanzia Chadema Sasa chadema ndio hao wanyonge??
Vip warioba naye anatafuta ulaji kupitia tume huru ya uchaguzi?
 
Haaaaaa haaaaa nilisikia maneno haya yakitamkwa maeneo ya jalala kuu sijui siku hizi bado lipo au linehamishwa.
... Roho wa hekima na maarifa aliyemwongoza hapo mwanzo kuyatamka yale maneno, siku hizi alishamtoka; kinywani halimtoki neno ila upotoshaji wa yale yale aliyoyaamini na kutuaminisha mwanzoni!
 
Nchi ngumu hii,

Watu wanataka kubadili Katiba ambayo hata hawaifahamu ,

Yaani hiyo wanayosema wanataka ibadilishwe ni wachache sana wanaoifahamu kwa mapana yake,

Na ndio hao wanaowadanganya kundi kubwa ambalo haliifahamu vyema.

Kelele za Katiba Mpya zimeanzia Chadema Sasa chadema ndio hao wanyonge??
Mawazo haya ya kijinga ndiyo yanayosababisha chokochoko kutoka kwa uma.
 
Afadhali ya Warioba na Werema Wanauthubutu wa KUSEMA KATIBA MPYA ni MUHIMU kuliko KABUDI,POLEPOLE na KIGWANGALA wanaosifia KATIBA ILIYOPO
Alafu hayo Mataga yanajifanya yanaijua Nchi na CCM kuliko Warioba na Jaji Werema.
 
Wanafiki ni nyie mnaotetea uozo. Ukitaka kujua wewe ni mnafiki, kesho Samia akisema katiba mpya inakuja, utaandamana kumuunga mkono! Ndio unafiki wako huo. Njaa inakusumbua.

Back
Top Bottom