Aliyekuwa mwenyekiti wa Tume ya Katiba mpya Jaji Warioba amesema wananchi hawa wanaoitwa " Wanyonge" ndio wenye nchi.
Warioba amesema Rais Samia amesimama imara kwenye utendaji wake baada ya kifo cha hayati Magufuli na amekubali kushughulikia suala la katiba mpya.
Jaji Warioba amesema kuna mambo ya katiba ambayo yanaweza kupelekwa bungeni na kufanyiwa marekebisho kama ambavyo sheria ya mawasiliano inafanyiwa ammendmends mara kwa mara.
Cha ajabu tunaambiwa mawasiliano ni " kipaumbele" na sisi tunasema katiba ni kipaumbele.
Mahojiano ya Jaji Warioba yatarushwa jumatatu ITV kipindi dakika 45.
Chanzo: ITV habari
Nawasalimu kwa jina la JMT.
Kwanza kuna swali moja la kuuliza. Unapokuwa madarakani unaweza ukawa unakuja kwa nia njema kabisa ya kupigania haki za wananchi na sio maslahi binafsi na kulinda serikali hata kama inakosea.
Kwa maneno hayo sasa. Tujiulize, ni wangapi ambao wanaweza kuweka kipaumbele shida za wananchi na kuweza ku sacrifice hata uhai wake. Tunajua kupigania haki ni jambo linalohitaji ujasiri sana. Ili uwe kiongozi bora katika hili ni lazima pia usiwe mlafi wa pesa na uroho wa madaraka, pia unahitaji kua na mindset ya mwanafalsafa.
Kwa mfano tunawalaumu sana viongozi/wanasiasa juu ya uwajibikaji. Lakini ukweli mchungu kwa dunia ya sasa viongozi ni wafanyabiashara. Na siku zote mfanya biashara atafanya chochote hata kudiriki kudanganya wananchi ilimradi lengo lake litimie. Hawa huwa hawana uchungu na jamii wanazotoka, huwa ni waoga wa kupoteza mali na pesa kwa ajili ya kupambana dhidi ya matatizo ya nchi.
Kiongozi wa aina hii, huwa anahakikisha anacheza karata yake kwa umakini sana akiwa madarakani au nyazfa yoyote ya uongozi.
Sisi wananchi tunabaki kulia mara ooh mbona mbunge fulani anajua tuna matatizo fulani wilayani lakini haongei. Anaweza asiongee kwa sababu kwake ni rahisi kuishi vizuri aki defend serikali kuliko ku defend wananchi. So wanachofanya wanaaangalia sehemu yenye influence ya power. Kama kusifia raisi kutamfanya maisha yake yawe mazuri na salama atasifia sana hata kama ni ujinga.
Ndo maana tunasema kwa dunia ya sasa 2021 tuna wafanya biashara wengi sana kwenye nyazifa za uongozi kuliko wazalendo na viongozi wa kweli. Sifa kuu ya mfanyabiashara ni kufanya chochote kinachomwezesha kupata hela na usalama wa maisha yake sio ya wananchi.
Sasa solution ya hii mambo ni nn wakuu? South afrika imetuonesha ni kiasi gani kuna wafanya biashara wengi kuliko viongozi. Kuna swala la kujifunza hapa kama nchi.