Warithi wa Manara

Warithi wa Manara

Klabu ya Simba imewatambulisha Mwijaku na Kay Mziwanda kuwa wahasishaji wapya wa klabu hiyo, kazi aliyokuwa akiifanya aliyekuwa Msemaji wa klabu hiyo Haji Manara.

View attachment 1981932

Umewapokeaje wahamasishaji hawa?

Binafsi sina neno ila nina swali moja tuu, je hawa wana mikataba?
Watajua wenyewe kama wana mikataba au wanajitolea
 
Hakuna mhamasishaji hapo. Sana sana ni watu wakuzungumza maneno ya shombi kwa timu pinzani.

Lakini Simba ilishatoka huko kwenye mambo ya Kiswahili kwanini yanajirudia tena?
 
Yule lunatic anasema apigwe mawe au atatembea uchi, mpira umevamiwa
 
Mkuu watu wengi wanachanganya hafisa habari wa team na muhamasishaji wa team.
Kuamini maneno yangu ona kichwa cha habari cha mleta mada na michango ya wadau utaamini maneno yangu.
Duh.... Basi sawa.... [emoji1787]
 
Klabu ya Simba imewatambulisha Mwijaku na Kay Mziwanda kuwa wahasishaji wapya wa klabu hiyo, kazi aliyokuwa akiifanya aliyekuwa Msemaji wa klabu hiyo Haji Manara.

View attachment 1981932

Umewapokeaje wahamasishaji hawa?

Binafsi sina neno ila nina swali moja tuu, je hawa wana mikataba?
Wachambaji wa club, mpira wetu una safari ndefu.
 
Mgamasishaji wa Simba kaweka nia kutembea uchi mchana kweupe naamini mashabiki wa klabu mtamuunga mkono mutembee kwa pamoja
 
Bora hata wangewapa hawa masela hilo jukumu la uhamasishaji
IMG_20211022_053510.jpg
 
Mhamasishaji atatembea uchi na mashabiki inabidi wahamasike watembee uchi kweupee
 
Back
Top Bottom