Wasabato na kunena kwa lugha, hadi lini mtaishi katika uongo?

Cashman

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2018
Posts
3,333
Reaction score
5,845
Moja ya ishara iliyotajwa kuambatana na waaminio ni kusema kwa lugha mpya katikaMarko 16:17

Paulo akielezea hili, alisema katika 1 kor 14:2 "maana yeye anenaye kwa lugha hasemi na watu,bali husema na Mungu;maana hakuna asikiaye lakini anena mambo ya siri katika roho yake.

Nimekuwa nafuatilia kipindi cha Hope TV, katika mjadala wa kunena kwa lugha wanachotambua wasabato ni ile ya matendo ya mitume siku ya pentekoste pekee.Ambapo waumini waliongea lugha zilizoeleweka kwa mataifa mbali mbali.

Hata hivyo kwa uelewa wangu mdogo,biblia inabainisha kuwepo kwa namna mbili za kunena kwa lugha.

Hii namna ya pili ambayo mtu husema kwa lugha wasiyosikia wanadamu,ni namna ya maombi binafsi ambayo mtu anapaswa kufanya.

Mtu akiwa peke anaomba peke yake kwa akili,mawazo hutembea kwa kasi kubwa sana katika akili,hivyo anaweza kujikuta anapoteza mwelekeo wa kile anachokiomba kwa kuwa ni vigumu kuzuia wimbi la mawazo kutembea kwenye akili.

Ndio maana watu kama wakatoliki na waislam,wana aina ya maneno au sala wanazosisema kwa kurudia rudia wakiwa wana rozali au tasbihi.Hii huwasaidia kuzuia kasi ya mawazo mengine kuingilia sala zao.Kakini Mungu alitoa njia bora ya roho wake kuomba kwa ajili yetu kupitia kunena kwa lugha.

Kunena kwa lugha mpya, lugha ambayo hata wewe mwenyewe huifahamu, kumekusudiwa kukusaidia wewe binafsi kufikisha kilio chako kwa Mungu kwa kuwa kwa akili yako unaweza kuomba bila kugusa mambo ya msingi kabisa unayopaswa kuyaombea kwa Mungu.

Ni kama mtu anayemtumia wakili katika kesi yake kwa kuwa yeye hajui lugha za sheria mahakamani.

Wasabato mnapinga sana suala hili la kunena kwa lugha au hayo aliyoandika Paulo hayamo kwenye biblia mnazotumia?

---------------

Hao hawana Spiritual Awakening wanazidiwa mpaka na Buddha,siku zote ukitaka uende deep spiritual lazima uchant hata waabudu Shetani wanaijua hii siri ya kunena kwa Lugha na wanaitumia kufungua mageti ya ufahamu wa giza sembuse hao wanajiita waKristo na hawajui hiyo siri wanawezaje kua spiritual au wanetu chachi kwao wanapiga story na kuondoka?
 
Hata Mimi napinga,Kila siku hapa
Moja ya ishara iliyotajwa kuambatana na waaminio ni kusema kwa lugha mpya katikaMarko 16:17

Paulo akielezea hili, alisema katika 1 kor 14:2 "maana yeye anenaye kwa lugha hasemi na watu,bali husema na Mungu;maana hakuna asikiaye lakini anena mambo ya siri katika roho yake.

Nimekuwa nafuatilia kipindi cha Hope TV, katika mjadala wa kunena kwa lugha wanachotambua wasabato ni ile ya matendo ya mitume siku ya pentekoste pekee.Ambapo waumini waliongea lugha zilizoeleweka kwa mataifa mbali mbali.

Hata hivyo kwa uelewa wangu mdogo,biblia inabainisha kuwepo kwa namna mbili za kunena kwa lugha.

Hii namna ya pili ambayo mtu husema kwa lugha wasiyosikia wanadamu,ni namna ya maombi binafsi ambayo mtu anapaswa kufanya.

Mtu akiwa peke anaomba peke yake kwa akili,mawazo hutembea kwa kasi kubwa sana katika akili,hivyo anaweza kujikuta anapoteza mwelekeo wa kile anachokiomba kwa kuwa ni vigumu kuzuia wimbi la mawazo kutembea kwenye akili.

Ndio maana watu kama wakatoliki na waislam,wana aina ya maneno au sala wanazosisema kwa kurudia rudia wakiwa wana rozali au tasbihi.Hii huwasaidia kuzuia kasi ya mawazo mengine kuingilia sala zao.Kakini Mungu alitoa njia bora ya roho wake kuomba kwa ajili yetu kupitia kunena kwa lugha.

Kunena kwa lugha mpya, lugha ambayo hata wewe mwenyewe huifahamu, kumekusudiwa kukusaidia wewe binafsi kufikisha kilio chako kwa Mungu kwa kuwa kwa akili yako unaweza kuomba bila kugusa mambo ya msingi kabisa unayopaswa kuyaombea kwa Mungu.

Ni kama mtu anayemtumia wakili katika kesi yake kwa kuwa yeye hajui lugha za sheria mahakamani.

Wasabato mnapinga sana suala hili la kunena kwa lugha au hayo aliyoandika Paulo hayamo kwenye biblia mnazotumia?

Hata Mimi napinga,Kila siku hapa jirani Kuna kanisa lugha ni ileile shibhobho,shaggala shaggala, shibhobho ndio kunena huko!
 
Inapaswa tutambue mambo yafuatayo kuhusu kunena kwa lugha
1. Ni karama kutoka kwa Mungu, si kila mtu anapewa hii karama. Soma 1 Kor. 12:6:11
Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote.
Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana.
Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule;
mwingine imani katika Roho yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho yule mmoja;
na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha;
lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye.

2. Ni muhimu sana kuwepo na tafsiri katika kunena kwa lugha. Soma 1 Kor. 14:27–28
Kama mtu akinena kwa lugha, wanene wawili au watatu, si zaidi, tena zamu kwa zamu, na mmoja na afasiri.
Lakini asipokuwapo mwenye kufasiri na anyamaze katika kanisa; aseme na nafsi yake tena na Mungu.

3. Kunena kwa lugha kulihusisha lugha halisi za wanadamu. hii ni kwa reference ya Matendo 2 na pia Kunena kwa lugha kunaweza kuwa lugha isiyoeleweka kwa wasikilizaji, kulingana na 1 corinthians 14.

Nb. Biblia haifundishi kwamba kila Mkristo lazima anene kwa lugha, wala haifundishi kwamba kunena kwa lugha ndiko kunakothibitisha mtu amepokea Roho Mtakatifu. “Je! wote hunena kwa lugha?” (1 Kor. 12:30).
Muhimu zaidi ni kutoka 1 Wakorintho 14:28 Lakini ikiwa hakuna mwenye kufasiri, na anyamaze katika kanisa; aseme mwenyewe na Mungu.”
Hapa ndipo kuna uwazi kabisaa: kama hakuna mfasiri, mtu hapaswi kuendelea kunena kwa lugha hadharani mbele ya kusanyiko.
 
Hapa ndipo huwa naona kumbe mambo ya kiroho sio mepesi.Umeshindwaje kujibu hoja ya mstari wa Paulo unaosema anenaye kwa lugha haongei na binadamu bali Mungu?!Hata hiyo ya kutafsiri wanayofanya wasabato,ni kuhutubu sio kunena kwa lugha kunakozungumzwa hapo
 
Ni kweli kwamba 1 Korintho 14:2 inasema anayenena kwa lugha hasemi na wanadamu bali Mungu. Lakini hiyo haihalalishi kunena bila tafsiri mbele ya kanisa au mkutano. Paulo huyo huyo katika mistari 13, 27 na 28 anasema lugha itafsiriwe, na kama hakuna mfasiri, anayenena anyamaze katika kanisa. Kwa hiyo, suala si kwamba kunena kwa lugha hakuhitaji kueleweka kwa sababu ni kati ya mtu na Mungu; suala ni kwamba mbele ya kusanyiko, lazima kuwe na tafsiri ili kanisa lijengwe. Kama Paulo alivyoeleza.

Kwa mtazamo wangu, ukisoma Wakorintho wa kwanza 14 yote. Naona inaeleza wazi kabisa hasa mstari wa 28 kuhusu maelekezo ya Paulo kuhusu kunena kwa lugha.
 
wanenaji wote wanasema maneno yale tu halafu wanakwambia ni lugha mpya,,, lakini wameiakariri.... ina maana hakuna cha roho mtakatifu anayeongea nao ila ni kitu walichokariri na wanajilazimisha kuamini kuna kitu nje ya wao ndo kinahusika na huko kupotoka..

mimi siyo msabato maana siamini kuwa Ellen G. White ni Nabii..
 
Ishi kusudi la MUNGU!
 
Moja ya ishara iliyotajwa kuambatana na waaminio ni kusema kwa lugha mpya katikaMarko 16:17

Paulo akielezea hili, alisema katika 1 kor 14:2 "maana yeye anenaye kwa lugha hasemi na watu,bali husema na Mungu;maana hakuna asikiaye lakini anena mambo ya siri katika roho yake.

Nimekuwa nafuatilia kipindi cha Hope TV, katika mjadala wa kunena kwa lugha wanachotambua wasabato ni ile ya matendo ya mitume siku ya pentekoste pekee.Ambapo waumini waliongea lugha zilizoeleweka kwa mataifa mbali mbali.

Hata hivyo kwa uelewa wangu mdogo,biblia inabainisha kuwepo kwa namna mbili za kunena kwa lugha.

Hii namna ya pili ambayo mtu husema kwa lugha wasiyosikia wanadamu,ni namna ya maombi binafsi ambayo mtu anapaswa kufanya.

Mtu akiwa peke anaomba peke yake kwa akili,mawazo hutembea kwa kasi kubwa sana katika akili,hivyo anaweza kujikuta anapoteza mwelekeo wa kile anachokiomba kwa kuwa ni vigumu kuzuia wimbi la mawazo kutembea kwenye akili.

Ndio maana watu kama wakatoliki na waislam,wana aina ya maneno au sala wanazosisema kwa kurudia rudia wakiwa wana rozali au tasbihi.Hii huwasaidia kuzuia kasi ya mawazo mengine kuingilia sala zao.Kakini Mungu alitoa njia bora ya roho wake kuomba kwa ajili yetu kupitia kunena kwa lugha.

Kunena kwa lugha mpya, lugha ambayo hata wewe mwenyewe huifahamu, kumekusudiwa kukusaidia wewe binafsi kufikisha kilio chako kwa Mungu kwa kuwa kwa akili yako unaweza kuomba bila kugusa mambo ya msingi kabisa unayopaswa kuyaombea kwa Mungu.

Ni kama mtu anayemtumia wakili katika kesi yake kwa kuwa yeye hajui lugha za sheria mahakamani.

Wasabato mnapinga sana suala hili la kunena kwa lugha au hayo aliyoandika Paulo hayamo kwenye biblia mnazotumia?

---------------
USIPOTOSHE WATU WEWE NENO LIPO WAZI KWA WANAONENA KWA LUGHA NA UTAPELI HUO WA KUNENA AMBAO MUNGU AMEUZUIA SOMA

1 Wakorintho 14:23 Haya! Ikiwa kanisa lote limekusanyika pamoja, na wote wanene kwa lugha, kisha ikawa wameingia watu wajinga au wasioamini, je! Hawatasema ya kwamba mna wazimu?

kisha soma hapa
1 Wakorintho 14:27-33
27 Kama mtu akinena kwa lugha, wanene wawili au watatu, si zaidi, tena zamu kwa zamu, na mmoja na afasiri.

28 Lakini asipokuwapo mwenye kufasiri na anyamaze katika kanisa; aseme na nafsi yake tena na Mungu.

29 Na manabii wanene wawili, au watatu, na wengine wapambanue.

30 Lakini mwingine aliyeketi akifunuliwa neno, yule wa kwanza na anyamaze.

31 Kwa maana ninyi nyote mwaweza kuhutubu mmoja mmoja, ili wote wapate kujifunza, na wote wafarijiwe.

32 Na roho za manabii huwatii manabii.

33 Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani; vile vile kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu.
 
Back
Top Bottom