Hata Mimi napinga,Kila siku hapa jirani Kuna kanisa lugha ni ileile shibhobho,shaggala shaggala, shibhobho ndio kunena huko!Moja ya ishara iliyotajwa kuambatana na waaminio ni kusema kwa lugha mpya katikaMarko 16:17
Paulo akielezea hili, alisema katika 1 kor 14:2 "maana yeye anenaye kwa lugha hasemi na watu,bali husema na Mungu;maana hakuna asikiaye lakini anena mambo ya siri katika roho yake.
Nimekuwa nafuatilia kipindi cha Hope TV, katika mjadala wa kunena kwa lugha wanachotambua wasabato ni ile ya matendo ya mitume siku ya pentekoste pekee.Ambapo waumini waliongea lugha zilizoeleweka kwa mataifa mbali mbali.
Hata hivyo kwa uelewa wangu mdogo,biblia inabainisha kuwepo kwa namna mbili za kunena kwa lugha.
Hii namna ya pili ambayo mtu husema kwa lugha wasiyosikia wanadamu,ni namna ya maombi binafsi ambayo mtu anapaswa kufanya.
Mtu akiwa peke anaomba peke yake kwa akili,mawazo hutembea kwa kasi kubwa sana katika akili,hivyo anaweza kujikuta anapoteza mwelekeo wa kile anachokiomba kwa kuwa ni vigumu kuzuia wimbi la mawazo kutembea kwenye akili.
Ndio maana watu kama wakatoliki na waislam,wana aina ya maneno au sala wanazosisema kwa kurudia rudia wakiwa wana rozali au tasbihi.Hii huwasaidia kuzuia kasi ya mawazo mengine kuingilia sala zao.Kakini Mungu alitoa njia bora ya roho wake kuomba kwa ajili yetu kupitia kunena kwa lugha.
Kunena kwa lugha mpya, lugha ambayo hata wewe mwenyewe huifahamu, kumekusudiwa kukusaidia wewe binafsi kufikisha kilio chako kwa Mungu kwa kuwa kwa akili yako unaweza kuomba bila kugusa mambo ya msingi kabisa unayopaswa kuyaombea kwa Mungu.
Ni kama mtu anayemtumia wakili katika kesi yake kwa kuwa yeye hajui lugha za sheria mahakamani.
Wasabato mnapinga sana suala hili la kunena kwa lugha au hayo aliyoandika Paulo hayamo kwenye biblia mnazotumia?
Hapa ndipo huwa naona kumbe mambo ya kiroho sio mepesi.Umeshindwaje kujibu hoja ya mstari wa Paulo unaosema anenaye kwa lugha haongei na binadamu bali Mungu?!Hata hiyo ya kutafsiri wanayofanya wasabato,ni kuhutubu sio kunena kwa lugha kunakozungumzwa hapoInapaswa tutambue mambo yafuatayo kuhusu kunena kwa lugha
1. Ni karama kutoka kwa Mungu, si kila mtu anapewa hii karama. Soma 1 Kor. 12:6:11
Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote.
Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana.
Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule;
mwingine imani katika Roho yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho yule mmoja;
na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha;
lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye.
2. Ni muhimu sana kuwepo na tafsiri katika kunena kwa lugha. Soma 1 Kor. 14:27–28
Kama mtu akinena kwa lugha, wanene wawili au watatu, si zaidi, tena zamu kwa zamu, na mmoja na afasiri.
Lakini asipokuwapo mwenye kufasiri na anyamaze katika kanisa; aseme na nafsi yake tena na Mungu.
3. Kunena kwa lugha kulihusisha lugha halisi za wanadamu. hii ni kwa reference ya Matendo 2 na pia Kunena kwa lugha kunaweza kuwa lugha isiyoeleweka kwa wasikilizaji, kulingana na 1 corinthians 14.
Nb. Biblia haifundishi kwamba kila Mkristo lazima anene kwa lugha, wala haifundishi kwamba kunena kwa lugha ndiko kunakothibitisha mtu amepokea Roho Mtakatifu. “Je! wote hunena kwa lugha?” (1 Kor. 12:30).
Muhimu zaidi ni kutoka 1 Wakorintho 14:28 Lakini ikiwa hakuna mwenye kufasiri, na anyamaze katika kanisa; aseme mwenyewe na Mungu.”
Hapa ndipo kuna uwazi kabisaa: kama hakuna mfasiri, mtu hapaswi kuendelea kunena kwa lugha hadharani mbele ya kusanyiko.
MaranathaYESU anakuja!
Ishi kusudi la MUNGU!wanenaji wote wanasema maneno yale tu halafu wanakwambia ni lugha mpya,,, lakini wameiakariri.... ina maana hakuna cha roho mtakatifu anayeongea nao ila ni kitu walichokariri na wanajilazimisha kuamini kuna kitu nje ya wao ndo kinahusika na huko kupotoka..
mimi siyo msabato maana siamini kuwa Ellen G. White ni Nabii..
USIPOTOSHE WATU WEWE NENO LIPO WAZI KWA WANAONENA KWA LUGHA NA UTAPELI HUO WA KUNENA AMBAO MUNGU AMEUZUIA SOMAMoja ya ishara iliyotajwa kuambatana na waaminio ni kusema kwa lugha mpya katikaMarko 16:17
Paulo akielezea hili, alisema katika 1 kor 14:2 "maana yeye anenaye kwa lugha hasemi na watu,bali husema na Mungu;maana hakuna asikiaye lakini anena mambo ya siri katika roho yake.
Nimekuwa nafuatilia kipindi cha Hope TV, katika mjadala wa kunena kwa lugha wanachotambua wasabato ni ile ya matendo ya mitume siku ya pentekoste pekee.Ambapo waumini waliongea lugha zilizoeleweka kwa mataifa mbali mbali.
Hata hivyo kwa uelewa wangu mdogo,biblia inabainisha kuwepo kwa namna mbili za kunena kwa lugha.
Hii namna ya pili ambayo mtu husema kwa lugha wasiyosikia wanadamu,ni namna ya maombi binafsi ambayo mtu anapaswa kufanya.
Mtu akiwa peke anaomba peke yake kwa akili,mawazo hutembea kwa kasi kubwa sana katika akili,hivyo anaweza kujikuta anapoteza mwelekeo wa kile anachokiomba kwa kuwa ni vigumu kuzuia wimbi la mawazo kutembea kwenye akili.
Ndio maana watu kama wakatoliki na waislam,wana aina ya maneno au sala wanazosisema kwa kurudia rudia wakiwa wana rozali au tasbihi.Hii huwasaidia kuzuia kasi ya mawazo mengine kuingilia sala zao.Kakini Mungu alitoa njia bora ya roho wake kuomba kwa ajili yetu kupitia kunena kwa lugha.
Kunena kwa lugha mpya, lugha ambayo hata wewe mwenyewe huifahamu, kumekusudiwa kukusaidia wewe binafsi kufikisha kilio chako kwa Mungu kwa kuwa kwa akili yako unaweza kuomba bila kugusa mambo ya msingi kabisa unayopaswa kuyaombea kwa Mungu.
Ni kama mtu anayemtumia wakili katika kesi yake kwa kuwa yeye hajui lugha za sheria mahakamani.
Wasabato mnapinga sana suala hili la kunena kwa lugha au hayo aliyoandika Paulo hayamo kwenye biblia mnazotumia?
---------------