Wasabato Yesu Kristo ni Alfa na Omega, Mnadai alianza kufanya upelekezi wa matendo yetu miaka ya 1860's, haingii akilini, mnamshushia hadhi yake!

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
3,585
Reaction score
8,106
Moderator naomba mada hii isiunganishwe kwingineko


Wadau hamjamboni nyote?

Nimekuja tena na hoja kuwa Yesu Kristo ni Alfa na Omega na amekabidhiwa mamlaka yote haitaji kufanya upelekezi kujua dhambi anazozifanya mwanadamu!

Ndiyo yeye ndiye mwenye mamlaka makuu na uwezo wake haufananishwi na kiumbe yeyote yule hivyo haitaji kufanya mchakato wa kupelekeza kama vile yeye ni mwanadamu ili kujua kama tumetenda mema au mabaya.

Bwana wetu Yesu Kristo haitaji hata kuweka kumbukumbu ya matendo yetu bali uwezo wa kipekee alio nao automatically unatunza kumbukumbu zote za matendo yetu!

Kudai kuwa eti mwaka fulani ndiyo alianza kufanya upelekezi basi huko ni kumfananisha yeye na viongozi wa idara za ujasusi za FBI au CIA, wapo vizuri kwenye faninhiyo ila wanasalia kuwa wanadamu!

Bwana wetu Yesu Kristo wetu anajua kila kitu tunachokifanya hata kabla ya kufanya

Niwatakie siku njema
 
Nikiwa Rais wa nchi kitu cha kwanza nitakachokifanya ni kupiga marufuku dini zote, dini zimefanya watu wamekuwa wajinga sana hata awe na degree ni kazi bure.
 

Ufunuo 20:12​

Kisha nikawaona watu wakubwa na wadogo, wamesimama mbele ya kiti cha enzi, na vitabu vikafunguliwa. Halafu kitabu kingine, yaani kitabu cha uhai, kikafunguliwa pia. Wafu wakahukumiwa kadiri ya matendo yao, kama ilivyoandikwa ndani ya vitabu hivyo.

basi ukatae hili kwamba vitabu vilifunuliwa kutafuta kumbukumbu humo
 
Mimi huwa najiuliza, sasa ilikuwaje yesu akafanyiwa tohara( kutairiwa) wakati yeye ndyo bwana, walimfanyia hivyo kwa lengo gani?
 
Kwa uelewa wako unadhani kuwa hivyo ni Vitabu vilivyotajwa hapo ni sawa na vile unavyotumia ukiwa darasani kwenye shule zetu za kata?
 
Mkuu soma kitabu "The Great Controversy" au "Pambano Kuu" kwa kiswahili kitakusaidia sana. Nimekiambatanisha hapa kwa ajili ya wokovu wako. Maswali yako mengi kuhusu Wasabato yatapungua mkuu.
 

Attachments

Mkuu soma kitabu "The Great Controversy" au "Pambano Kuu" kwa kiswahili kitakusaidia sana. Nimekiambatanisha hapa kwa ajili ya wokovu wako. Maswali yako mengi kuhusu Wasabato yatapungua mkuu.
Hicho kitabu cha nini hasa? Ingalikuwa vema ukanukuu maandiko ya Biblia badala ya mapokeo au Itikadi za kidini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…