Wasafi Media bado inawahitaji Jonijoo na Mtiga Abdallah

Wasafi Media bado inawahitaji Jonijoo na Mtiga Abdallah

Kweli anayo ,lakini ninachomkubali huwa anayafanyia Kazi mapungufu yake na kuimprove .Zamani nilikuwa hata kumsikiliza siwezi nikawa nina dhana ya kuwa watu wenye uwezo mdogo wa kuchambua mambo ndio wanaoweza kumsikiliza na kushangaa watu wakimsifia ila nimeona video zake za karibuni amejigahidi sana.
kwahiyo unadhani jamal anatosha kufanya kazi zote mbili haitaji msaada
 
Wana wanampa sifa nyingi sana Jamal April sometimes anazingua kutuletea story za upuuzi kuelezea maisha ya peponi, mara jehanam kupoje mambo ya dhahania dhahania yanakera sana. watu tunataka mambo yalioExist, mambo reality
Watu wanaofuatilia hizo story ni vilaza fulani tu hivi..

Mtu na akili yako huwezi kushabikia hizi story za kusadikika kwenye hizi simulizi uchwara.
 
Watu wanaofuatilia hizo story ni vilaza fulani tu hivi..

Mtu na akili yako huwezi kushabikia hizi story za kusadikika kwenye hizi simulizi uchwara.
Lazima uchague sio kila kitu cha kusikiliza, mimi nafutilia zaidi stori zinazohusu maisha ya watu mule mfano Bob,Dube,Bruce viongozi nk coz najua inakuwa ngumu kukuta chai ila hayo matukio uchwara naishia kusoma heading tu.
 
wasafi walimuondoa kwa kumchafua hiyo ndo sifa ya wasafi wanakuchafua kuwa wewe mlevi, jeuri na unatumia mihadarati ..

sasa itakuwa ngum sana mtiga kurudi wasafi media
sio kwamba ni ngumu, haiwezekani,kabisa kurudi pale ,nyie ndio mnaangaika tu kumlilia arudi
 
Ndugu mwandishi wa huu uzi sidhani kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa Wasafi media. Ndio nasema kwamba wewe sio mfuatiliaji kwasababu zifuatazo:
1. Kwanza inaonekana unazungumzia hisia binafsi na maoni tu ya kwako binafsi na wala sio kwamba unawasemea watu wote.

2. Block 89 unayoizungumzia kuwa ilikuwa poa sana, kuna wenzako waliikataa na kusema ni kipindi kibovu na kilikuwa kwenye bad timing. Japo hapa nakiri kwamba binafsi nilikipenda sana hiki kipindi. Ila unaposema pia kwamba mtu anaweza kuacha kusikiliza Clouds XXL kwasababu ya block 89 sio kweli kwasababu vipindi hivi vilikuwa muda tofauti.

3. Mtiga na Jonijoo: nakubali na kuheshimu mchango wao kwa wasafi Media na pia nikiri ubora wao walipokuwa wasafi Media. Lakini unajua kwa sasa wako wapi na wanafanya nini? [emoji1] Mpaka hapo utagundua pia kwamba Wasafi Media pia ilikuwa inawabeba. Kwa mfano huyu Mtiga alikuwa mwanafunzi wa Jamal, aliandikiwa stori na kuelekezwa pia jinsi ya kuzisoma. Kipaji chake kikubwa ni sauti yake nzuri [emoji91]

4. Wasafi Media kumtegemea Zuchu na Diamond [emoji1][emoji91] Ni kweli kwanza Diamond ni msanii anayezungumziwa zaidi Tanzania na nje ya Tanzania na suala la kumzungumzia halikwepeki. Hakuna namna....ndio maana hata Media zilizokuwa na tofauti naye zimerudi zenyewe na zinapiga nyimbo zake. Zuchu ni dhahabu, nyimbo kali, kipaji na ubunifu wake unamfanya kuwa mmoja wasanii bora kabisa wa kike kwa Tanzania na Afrika kwa sasa. Utaachaje kumzungumzia?

5. Wasafi TV: Africa Is watching. Hii ina maana kwamba maudhui na mtazamo mzima umebadilika na hivyo lazima ilenge kuhudumia Africa nzima.
 
shida sio Jamal kufanya vitu viwili. ila kufanya vitu viwili kwa wakati moja kuna athari kubwa mfano jamal leo hii ana mvuto katika usimuliaji maana yake anataka kuandika pia anatka kusimulia hatima yake anakuta kuna kimoja anaharibu .

Jamal binadam kama binadamu wengine anatakiwa afanye kitu kimoja kwenye media yoyote lazima kuwa na mgawano wa majukumu .

Sio mtu moja huyo huyo awe producer, awe dj pia awe Radio presenter
Hakuna tatizo hapa. Kama kazi inafanyika vizuri sioni shida iko wapi kwasababu kazini pia huwa inatokea unapokuwa na majukumu ya ziada lazima ulipwe kwa majukumu hayo. Na kuna watangazaji wengi ambao pia ni producers wa show zao na wala sio tatizo. Na kwa kukusaidia, anayeandika jambo ndio ana hisia za kweli na lile jambo kuliko msimuliaji
 
Jonijo,Jamal na Abdallah Mtiga sisi wa Shinganga vijiji tunaomba muwapositi picha zao tuwajue.

Wabeja sana bhaghosha[emoji120]
 
Back
Top Bottom