Wasafi Media Mtegoni. Diamond, Kusaga wavurugana

Wasafi Media Mtegoni. Diamond, Kusaga wavurugana

Hili suala binafsi nilikuwa nalifahamu tangu 2011 wakati nafanya kazi kwenye media house. Wengi wenu humu JF hamjui mambo mengi sana ya mjini. Mmesoma ila mambo ya town mko nyuma sana.
Kusema nilifanya kazi, alikua/ni rafiki yangu, nimesomea hayo mambo nk ni weak defending points.

Yaani kisa wewe ulikua kwenye media house basi tukuamini??
Haya kuna mdau hapo kafanya research tcra nae anataka tumuamini!!
Leta hoja sio mimi ni nani, ukizingatia jf yenyewe hatujuani.
 
I View attachment 2930478
Hii habari ni ya mda sana mleta uzi Sasa[emoji276][emoji276]
Sasa Mkuu, huyo Ali Kiba hajazungukwa na watu? Na huyo Dullah Planet hajazungukwa na watu pia mpaka hii habari iwe siri?
BTW sijui hata kama Chapo amewahi kuandika hilo, na hakuna nilikosema hii ni breaking news.

Habari moja itaripotiwa na vyombo vingi, kinachotofautisha ni aina/namna ya kuripoti.

Halafu habari yangu imebeba details lukuki, sio habari ya Media ya Ali pekee.
 

Wakurugenzi wa Wasafi Media, Joseph Kusaga na Naseeb Abdul ‘Diamond Platinumz’ wanaripotiwa kukosa maelewano kati yao juu ya uendeshaji wa media hiyo inayomilikiwa na wawili hao.

Chanzo ni TRA
Diamond ambaye amekuwa akitafutwa na maafisa kodi kwa muda mrefu, huku yeye akitumia 'janja janja' kuwakwepa, maafisa kodi hao wamehamishia majeshi kwa Joseph Kusaga.

Joseph Kusaga ambaye majukumu ya uendeshaji amemwachia Diamond, amekuwa akimpigia simu mara nyingi bila mafanikio.
Hivyo Diamond anawakwepa maafisa kodi, na huku simu za Kusaga pia hapokei.

Kusaga achoshwa na mabifu ya Diamond!
Inaarifiwa kuwa Kusaga amekuwa akilalamika mara nyingi juu ya mabifu ya Diamond na watu wengi ambayo yanaikwamisha Wasafi Media kukua.

Wakati anaanzisha media hiyo 2016, alikuwa na malengo makubwa ya kuikuza kuwa kubwa pengine kuizidi Clouds Media ambayo ni mali ya familia yao. Hivyo kupitia umaarufu wa Diamond alitegemea kuvuna wasikilizaji kutoka kila pembe ya nchi jambo ambalo kwa kiasi kikubwa limefanikiwa ila kikwazo kikiwa ugomvi wa Diamond na watu wengi ambao wengi hutumia mabifu hayo kama fursa ya kuikwamisha Wasafi Media.

Kusaga amgeukia Ali Kiba…
Habari za uhakika ni kwamba mastermind huyo wa biashara za vyombo vya habari na nyinginezo lukuki, ameelekeza nguvu zake kwa hasimu wa Diamond, Ali Kiba.

Wawili hao (Kusaga na Ali) wapo kwenye hatua za mwisho kukamilisha masuala muhimu likiwemo jina rasmi la kutumika kuitambulisha Media hiyo.

Kupitia chanzo changu makini nimefanikiwa kunasa jina linalopewa kipaumbele, Kings Media (Kings TV & Kings FM).

Pia watangazaji ambao tayari wameshawekwa kwenye list ni Abdallah Ambua ‘Dullah Planet’ aliyeng’oka EATV na EA Radio hivi karibuni, pamoja na Khalid Mohamed ‘TID’.

Kusaga na utajiri wa frequencies!
Kwa wafuatiliaji wa masuala ya media hasa radio, watakuwa wanafahamu ya kwamba hivi sasa hakuna frequency mpya hapa jijini Dar Es Salaam.

Yaani kwamba ukitaka kuanzisha redio huwezi kupata mawimbi ya kukuwezesha kusikilizwa Dar, labda ununue (frequency) ambayo inamilikiwa na wengine kisha uibadilishe kuwa redio yako.

Wajanja wa mjini wamezihodhi, akiwemo Joseph Kusaga ambaye anaarifiwa kuwa nazo kwa idadi ambayo haifahamiki.

Kupitia chanzo changu nyeti,

Nifah.
Crown FM nigga
 
FM frequency inaanzia 87.5 hadi 108.0 na inajumla ya ya frequencies 101

Mpaka sasa Dar kuna frequency chini ya 50 zinazotumika na vituo mbali mbali vya Fm radio

Frequency hazinunuliwi kama njugu kusema utazinunua tu uziweke ndani zikae tu utakavyo

Utapewa frequency baada ya kuwa umetimiza masharti na vigezo vyote vya kuwa na Fm radio..... yaani umekamilisha mitambo na kila kitu ndio unaomba, nasio unakwenda na tai yako tu unajza form unapewa frequency

Serikali inatambua limitation ya frequency hairuhusu unakwenda tu na form zako unajaza unapewa

Dar bado frequency zipo, zinazo tumika ni chini ya frequency 50
 
FM frequency inaanzia 87.5 hadi 108.0 na inajumla ya ya frequencies 101

Mpaka sasa Dar kuna frequency chini ya 50 zinazotumika na vituo mbali mbali vya Fm radio

Frequency hazinunuliwi kama njugu kusema utazinunua tu uziweke ndani zikae tu utakavyo

Utapewa frequency baada ya kuwa umetimiza masharti na vigezo vyote vya kuwa na Fm radio..... yaani umekamilisha mitambo na kila kitu ndio unaomba, nasio unakwenda na tai yako tu unajza form unapewa frequency

Serikali inatambua limitation ya frequency hairuhusu unakwenda tu na form zako unajaza unapewa

Dar bado frequency zipo, zinazo tumika ni chini ya frequency 50
Haya masuala ya mtu kumiliki frequency kusaga mwenyewe alishawahi kuliongelea hili suala
 
Nina chanzo nyeti mnooo, mpaka nawaandikia hapa mnatakiwa muondoe shaka.
Hii habari ninayo wiki nzima sasa, mimi na chanzo tulishauriana tuitoe katika siku sahihi, ndio leo.

Shukrani za dhati kwa chanzo changu.
Acha kujipaisha basi we taarifa umeileta juzi jna redio inzinduliwa bado unaiita hyo taarifa ni nyeti
 
hiyo habari Mange aliandika now ni mwaka inaenda na alikuwa anaupdate kila mara ,wewe unakuja kuandika siku 1 kabla ya uzinduzi.
we bibi cheupe uko serious kweli?
Ndio unaniambia wewe kama Mange alikuwa anasema mimi wala sina habari.

Halafu kwani akisema Mange ndio wengine hatutakiwi kusema tena?
Okay, nimeandika. Wewe kinachokuuma ni nini?
 
Daah...! Ila hapo ndio nimekwama. Umesema Diamond hapokei simu za kusaga mara wako wote tena mahala?. Sasa simu za nini kama wanaonana?.

Kuna upande umeongea kiushabiki mno. Kwa kumponda Diamond.

Kwa namna hiyo unatuamisha kuna mengi ya uongo kwenye uongo kwenye hii habari ili tuamini Mond anazingua.

Kuna Jambo moja vijana wa kitanzania wana wivu sana na kijana mwenzao akifanikiwa. Nimeona vijana wengi bongo wanamchukia Mond bila sbb za msingi. Utasikia anaringa. Kisa tu amefanikiwa.

Kwa akili ya Mond + management yake sidhani kama anaweza kuzinguana na TRA kiasi cha kuwakimbia. Ni mara nyingi nimesikia amezinguana na TRA,bado ni kile kile ni wivu tu wanamsakama hata kupita ile taratibu za kawaida.

Nianavyo kwa huyu dogo Diamond watapoteza tu muda kumshusha. Vinginevyo waungane nae. Yule dogo akili kubwa. Yule dogo yuko mbali sana.
Tuwaunge mkono vijana wenzetu waliofanikiwa. Ama tuungane nao.
Ukishakua mfanyabiashara mkubwa kukwaluzana na TRA ni given. Kwa sababu Tanzania hii hakuna mtu analipa kodi 100%
 
Back
Top Bottom