Wewe kama mtaalamu wa hayo masomo ulitakiwa utoe ufafanuzi wa kina badala ya kutaja terminologies na classmates wako.
Mimi kama kilaza wa mambo ya radio frequency ngoja nieleze kwa kutumia ukilaza wangu. Radio frequencies kwa Tanzania nadhani zitakuwa zinaanza palepale ambapo sehemu nyingi duniani huwa zinaanza. Kuanzia 88.0MHz hadi 108.0MHz.
Sasa kati ya hizo frequency modulation (FM) radio stations, inabidi kuwepo na space ya 0.2MHz kuzuia kuingiliana kwa sauti maana frequency mfano redio ikiwa 89.7 unaweza isikia kwa kelele ukiweka 89.6 au 89.8, isingekuwa wanaacha nafasi kidogo basi redio zisingekuwa zinasikika vizuri mwenye transmitters kubwa ndio anasikika na mwingine anakuwa na noise. Hii issue hutumika kwenye jamming tukienda mambo ya usalama.
Na kuna sababu kwanini redio kongwe na kubwa kubwa zote zina frequencies chini ya 92MHz, alafu redio uchwara zile za sijui nani mkusanya sadaka ziko kwenye 102 na kupanda.
Therefore, nashawishika kuamini kuna watu walinunua frequencies za mwanzo nzurinzuri wakakaa nazo ilimradi wanazilipia TCRA. Hilo suala la kukosa mapato ni la TRA. Btw hii ni banana republic lolote linawezekana.
Hakuna mtu ataanzisha redio kubwa alafu frequency iwe 107.8, atabidi abanane na hawa 88, 89 uko. Na ndipo ataenda kununua kwa waliohodhi.
Alafu kukusanya umbea wa uhakika kwa vyanzo tofauti nadhani ni kazi sana. Badala ya kuja kuattack mleta taarifa kwamba muongo ingefaa expert wa fani yake aje na maelezo ya kushiba kujazia au kukosoa hoja. Badala yake mnachambua vipointi mnamuita mtu mwongo na wala hakuwa na intention ya kuongopa.