Wasafi Media na anguko la East Africa Radio

Wasafi Media na anguko la East Africa Radio

Hii wiki imeanza kwa kishindo upande wa Kiwanda cha media baada ya Wasafi Fm kufanya utambulisho wa watangazaji wa kipindi cha michezo cha Sport Arena, utambulisho uliojaa manjonjo na mbwe huku wakiwa wameacha vilio na mapengo kwenye baadhi ya vyombo vya habari,

Biashara ni Ushindani, eeeh ndio ushindani, naona yale yaliyofanyika kwa Clouds kuiba watangazaji wa EA Radio, na EFM kuiba kwa sasa naona yakitokea tena, issue kubwa ni dau, sehemu yoyote ukitangaza Dau mtu hufanya kwa kiwango cha juu sana plus taaluma na uzoefu,

Biashara ya media inabebwa na matangazo, matangazo nayo yanaangalia vipindi gani hupendwa na wasikilizaji, wasikilizaji nao huangalia kipindi kinaendeshwa na nani, ndiomaana tunaona wenye majina makubwa ndio wanufaika,

kuna watangazaji wadogo lakini wanauwezo mkubwa sana na wako mikoani au media kubwa Dar ila nafasi hawapewi, na kuna watangazaji wakubwa wanamajina ila maslah madogo sasa hapa ndio tunaona wenye upeo na biashara hucheza karata vizuri,

EA Radio kwenye usajili au nyakua nyakua, waliwapoteza Mammy Babby, Bantu, Kennedy, Sinyorita, na Ommy Crazy
hapo nyuma walishawapoteza Seba the warrior, Marygoreth Richard, nk
Mafuvu
pia walikosa kwa sababu zao binafsi

sasa kwenye usajili wa WASAFI fm katika kujitangaza na kujiboresha na kuteka hisia za watu, naona wafuatao wanaondoka,
Jr Junior, King Smash, Sam Misago pia kuna tetesi za watu wa team ya tv production kubebwa,

Hili litaleta anguko la pili baada ya lile la kwanza ambalo walipoteza sana mvuto kwa wasikilizaji na ikabaki ufanyaji wa kazi kwa mazoea bila initiative/strategy, pigo walilopigwa kuondoka Zembwela ni kubwa Supa Mix ndio basi tena, au wataendelea kuwazalishia watangazaji wazuri washindani wao..?
Ila zembwela kaniudhi kama alikuwa anataka nyongeza si angesema tu jamani
 
IPP kulinganisha na vitu vingine ni aibu kubwa sana,kimfumo unafuata sana maadili sio eti maarufu ndio urmtangazaji pale gamba lako sawa sio mala maarufu hawako hivyo kamwe.
 
Young talent ukiangalia kipindi cha Block89 wote wale ni young talent tena kuna Media zingine waliwaona hawafai ni makapi, kama Jonijo Times alikuwa kama yupoyupo, Calipso, Kissfm waliona hana jipya akaenda Lakefm, akaenda Times, mara Classic fm, hatimae wanaojua kujali wamemuona
aisee block 89 ni habari nyingine jamaa walianza slow ila sasa hivi ni moto
 
WASAFI wanaweza kununua watangazaji wote lakini hawawezi kununua wasilikizaji wote, mimi hata sioni sababu ya miluzi mingi kuwa imekuja kutingisha.
hivi huku mvomero wanapatikana masafa gani maana hii station naisikiliza tu hapa JF
 
Mimi pale EA RADIO hata aondoke nani, nitadumu kuwa msikilizaji wao.

Kuna vichwa mwanzo viliondoka bwana, achana na kina zembwela hawa.

Mwanzo mpaka nikawa nasema, nini hiki? Lakini mpaka leo EA RADIO wako imara.

DJ Mafuvu alipotoweka pale mjengoni, nikadhani pengo halitazibika, kumbe nilikuwa nadhani uongo, mpaka leo pengo lake limeshazibwa.

Haya, kuna yule dada aliyeko CLOUDS, nilidhani pengo lake halizibiki, lakini mpaka hapa pengo lake limezibwa, n.k n.k...
Ea Radio kile ni kiwanda, kila siku kinafyatua vichwa vipya.

Kwahiyo hao kina nani sijui wewe waache waende, lakini mimi na EA RADIO, Sijui aondoke nani pale ndipo niache kuisikiliza
Kwenye michezo kuna vichwa wamevichukua iringa ni hatari kina tigana lukinja ,EA radio ni kiwanda kile
 
Ivi ulichokiandika hata wewe mwenyewe ukiambiwa ukirudie kukikosoma utaelewa ulikuwa unamaanisha nini?
IPP kulinganisha na vitu vingine ni aibu kubwa sana,kimfumo unafuata sana maadili sio eti maarufu ndio urmtangazaji pale gamba lako sawa sio mala maarufu hawako hivyo kamwe.
 
Tangu nijue Wasafi wanaeneza sera za illuminat sina hamu hata ya kujua wanatangaza nini.
 
Akaondoka salama tukaona ohooooo....bwana akaja dullah tumesahau matatizo
Mimi pale EA RADIO hata aondoke nani, nitadumu kuwa msikilizaji wao.

Kuna vichwa mwanzo viliondoka bwana, achana na kina zembwela hawa.

Mwanzo mpaka nikawa nasema, nini hiki? Lakini mpaka leo EA RADIO wako imara.

DJ Mafuvu alipotoweka pale mjengoni, nikadhani pengo halitazibika, kumbe nilikuwa nadhani uongo, mpaka leo pengo lake limeshazibwa.

Haya, kuna yule dada aliyeko CLOUDS, nilidhani pengo lake halizibiki, lakini mpaka hapa pengo lake limezibwa, n.k n.k...
Ea Radio kile ni kiwanda, kila siku kinafyatua vichwa vipya.

Kwahiyo hao kina nani sijui wewe waache waende, lakini mimi na EA RADIO, Sijui aondoke nani pale ndipo niache kuisikiliza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom