Swala la sound ni tatizo sana Tanzania na watu hawawekezi kabisa kwenye sound zaidi ya kiki..mfano ukienda kuangalia ile show ya Dr Dre na Snop juzi kule Marekani aiseee ni lazima mtu atakubaliana na wewe wenzetu wamewekeza...kazi ya watanzania ni kununua spika tuu na vipaza sauti tuu
Lakini tumekuwa tukiwasingizia sana masound engineer lakini tujiulize ile sauti ya zuchu na yale makelele yake na kukoroma kule kweli kulihiitaji saound engineer?
Wasanii wetu live wanaimba vibaya sana yani uwezi amini kama ni huyu aliyeimba wimbo unao tamba!
Mbona kuna wasanii waliimba vyema?
Mfano Q chillah,Kassim Mganga na Mboso? Kwani s
Kwa hiyo kabla ya kuanza kuuliza kuhusu sound engineer tujiulize tuna wasanii wa aina gani? Wanao uwezo wa kuimba live? Wemezoea?
Zuchu hii ni show yake ya pili jukwaa hili hili na anafunikwa na watu wa aina ile ile na ni wale wale.....