Wasafi Tv wanachosha na Tv Yao

Wasafi Tv wanachosha na Tv Yao

Lavit

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2011
Posts
14,834
Reaction score
32,522
Wakuu mara kadhaa nimejaribu kuangalia hii tv na imeishia kunichosha tu...

Kwa kifupi nilitegemea itakuwa tv ambayo italeta mapinduzi katika sekta ya burudani lakini imekuwa tofauti kabisa...

Hawa jamaa muda wote wanapiga manyimbo yao, ukiwasha tu channel yao unakutana na lavalava, hujakaa kidogo mara kwangwaru, hazijapita dakika mbili Rayvan huyu hapa.. Umeenda bafuni umerudi utamkuta diamond.. Yan ni rotation hiyo kila siku na muda wote... Utakuta wimbo mmoja unapigwa hata mara 30 kwa siku...

Hawa jamaa inabidi wajirekebishe vinginevyo watakimbiwa sana na watazamaji, maana walichokuwa wanakipinga kwenye media nyingine ndicho wanachofanya wengine...
 
Nilishaacha kuiangalia mkuu, hawa wamefeli mapema kabisa
Kutokuangalia ww haimanishi kuwa wamefeli, TCRA peke yao wanaoweza wakatoa takwimu zakuonyesha wasilikilizaji, kupitia hiyo takwimu ndiyo itakayoonyesha either wamefeli au kufaulu na usichokipenda ww usikitie hila. Huu ni ulimwengu wa demokrasia, usichokipenda kipenda ww, Kuna watu wanavipenda kutoka moyoni.
 
Last edited:
Nyimbo zao hazichezwi kwenye machanel mengine,embu tuwaacheni wapoze machungu yao.
 
Tv bado ni mpya haina vipindi kwa sasa tofauti ya refresh na kungwi...ila baadae itakua na vipindi hadi hizo nyimbo utaman kuziona ila hutoziona
 
Wakuu mara kadhaa nimejaribu kuangalia hii tv na imeishia kunichosha tu...

Kwa kifupi nilitegemea itakuwa tv ambayo italeta mapinduzi katika sekta ya burudani lakini imekuwa tofauti kabisa...

Hawa jamaa muda wote wanapiga manyimbo yao, ukiwasha tu channel yao unakutana na lavalava, hujakaa kidogo mara kwangwaru, hazijapita dakika mbili Rayvan huyu hapa.. Umeenda bafuni umerudi utamkuta diamond.. Yan ni rotation hiyo kila siku na muda wote... Utakuta wimbo mmoja unapigwa hata mara 30 kwa siku...

Hawa jamaa inabidi wajirekebishe vinginevyo watakimbiwa sana na watazamaji, maana walichokuwa wanakipinga kwenye media nyingine ndicho wanachofanya wengine...
Watazamaji wakimbie kwenda wapi ?
 
Hizo ndio nyimbo zinazo tamba kwa sasa unataka wapige nyimbo gani na bado hawajaruhusiwa kufanya kitu kingine chochote zaidi ya mziki unataka nini? By the way Mtu una Instagram,una JAMII forum,una Twitter,una Facebook na Unabandle unataka TV/Radio /Gazeti vya nini
 
Back
Top Bottom