Wasafiri Tanzania wananyanyasika sana na kuibiwa wakiwa safarini

Wasafiri Tanzania wananyanyasika sana na kuibiwa wakiwa safarini

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
2,268
Reaction score
7,119
Wizi unaanzia kwa maajanti wa mabasi ambao hupandisha nauli hovyo.

Hawana nauli ambazo ni standardized. Utakuta basi moja kila mtu amelipa nauli tofauti japokuwa wanaenda sehemu moja.

Wakati wa kula chakula. Madereva na makomdakta wanawapeleka abilia kwenye sehemu ambazo ndio kuna wizi na uporaji mkubwa.

Mtu anauziwa wali kiduchu na nyama moja na mfupa usio na nyama kwa sh 6000 za kitanzania.

Huu ni wizi mkubwa sana kwa abiria na jambo ambalo sio jema.
 
ha ha ha
na bado Hormuz haijafunguliwa
 
Ni kweli aisee tunapigwa sana hasa kwenye vyakula.
 
Back
Top Bottom