Ndugu zangu, niaandika habari hii kwa uchungu nikiomba, kwa yeyeote atakayeisoma, afikishe habari hizi kwa wahusika ili hatua za haraka za uokozi zichukuliwe.
Kuna habari kwamba barabara inayotoka chunya kwenda manyoni imekatika na wasafiri wamekwama hapo porini maeneo ya ipole kwa siku tatu sasa.
Wito wangu ninaomba sana serikali iokoe hawa binadamu. pamoja na kuwapelekea askari wenye silaha (jambo ambalo ni jema), wawapelekee haraka huduma za kibinadamu. hawa watu watakufa porini.
Tunaomba chombo chochote chenye wepesi, kipeleke haraka chakula kama mikate white and brown, biscuits za sukari na zisizo na sukari, juice za sukari na zisizo, maji ya kunywa, huduma ya kwanza, dawa za kuzuia kuumwa na mbu, hata mablanketi ya kujifunika usiku ukizingatia pia njia hiyo huwa na tsetse flies.
Ombi lingine, kwa jinsi hali ya miuondo mbinu ilivyo kwa sasa, serikali ifanye juhudi za haraka za kutoa taarifa mapema pale kunapokuwa na barabara haipitiki ili watu wasiende kukwama maporini na kuhatarisha maisha. hii pia itasaidia watu kupanga route sahihi za kufika wanakotaka kwenda.
Habari nilizozipata ni kwamba daraja limekatika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na hivyo hakuna uwezekano wa gari kupita ama kutoka manyoni kwenda chunya, ama kutoka chunya kwenda manyoni.
Habari zilizonifikia ni kwamba kuna abiria wamekwama hapo porini tangu juzi. ni porini ambapo hakuna duka, hakuna huduma za mpesa, hakuna hoteli wala huduma ya chakula, hakuna huduma ya afya hata duka la dawa, hakuna maji salama, hakuna hata kijiji kinachoweza kutoa msaada kwa hawa binadamu.
Nimeambiwa kwamba serikali ya mkoa wa tabora walikwenda ku survey eneo la tukio. wakati wanajiandaa kujenga daraja, ama kufanya utaratibu wa kuwezesha mahala pale papitike, wamepeleka askari kulinda usalama. hili ni jema, lakini naomba sana uhai wa hao binadamu uangaliwe.