Tetesi: Wasafiri wamekwama porini kwa siku tatu, wanahitaji msaada wa haraka

Wakati umefika sasa wenye makampuni ya mabasi kuanzisha huduma za vyakula vikavu, vinywaji na mahitaji mengine ya kibinadamu kama dawa nk kwenye mabasi yao kwa ajili ya dharura
 
Vichwa vya jf sometime havieleweki.

WASAIDIE KWANI WAO NDIO WAMELETA MAFURIKO??

Ukienda kushiriki mazishi ina maana wewe ndo umeua? Punguza mzaha. Watu wanahitaji kusaidiwa
 
Sio lazima lifike Tabora... bali sehemu yoyote ya karibu wanayoweza kupata msaada. Ni ushauri tu maana sijui jiografia ya maeneo hayo

Kutokujua geographia ya maeneo hayo ni tatizo. lakini naambiwa kuna mengine yamezuiliwa kwenye kijiji cha IPALE, hayaendelei kuelekea kwenye eneo la tukio. Na ninategemea pia mengine yanayotoka Chunya, yawezekana yamezuiliwa kuondoka kule. Tatizo ni hawa waliokwama porini hapo, ambapo hata walikotoka haparudiki.
 
Bado unakuwa haujatatua tatizo. Kuna wasafiri wengine hawana hela ya ziada. Mtu amekata tiketi anaenda kwao halafu anarudishwa ugenini ambako hana jamaa wala ndugu.
Bora nusu shari kuliko shari kamili. Bora upate msaada wa binadamu mwenzio usiyemjua kuliko kugeuzwa asusa na fisi mwenye njaa kali
 
Bora nusu shari kuliko shari kamili. Bora upate msaada wa binadamu mwenzio usiyemjua kuliko kugeuzwa asusa na fisi mwenye njaa kali

Serikali ililpeleka askari wenye silaha kwa ajili ya usalama. TUNAOMBA UHAI SASA WA HAWA WATU!.
 
Serikali ililpeleka askari wenye silaha kwa ajili ya usalama. TUNAOMBA UHAI SASA WA HAWA WATU!.
Nlitegemea hao waliopelekwa na silaha wangepelekwa na vyakula vya misaada, maji na madawa. Na usafiri uliowafikisha hao washika silaha ndo ungewabeba hao waliokwama.

Anyway ngoja tuendelee kuwaombea.
 
Poleni sana cha kusikitisha wahusika huwa wanalala kwenye issue kama hizi huku wakideal na sheria za mitandao
 
Bado unakuwa haujatatua tatizo. Kuna wasafiri wengine hawana hela ya ziada. Mtu amekata tiketi anaenda kwao halafu anarudishwa ugenini ambako hana jamaa wala ndugu.
Hekima,Umoja na Amani hizi ni ngao zetu....
Hapa ndo pa kuonesha huo umoja wetu,aliye kwenye hiyo hali asaidiwe na mwenyeji yeyote,natumaini kuna ambao Mbeya ndo nyumbani.
 
Mkuu sasa kama serikali itaweza kubeba madikodiko yote hayo (meaning itatumia usafiri fulani), si bora tu itumie usafiri huo huo kuokoa watu instead...

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…