Tetesi: Wasafiri wamekwama porini kwa siku tatu, wanahitaji msaada wa haraka

Hekima,Umoja na Amani hizi ni ngao zetu....
Hapa ndo pa kuonesha huo umoja wetu,aliye kwenye hiyo hali asaidiwe na mwenyeji yeyote,natumaini kuna ambao Mbeya ndo nyumbani.
Kweli mkuu ila miongoni wapo wageni. Ni bora kukaa eneo la tukio walau unaweza kusaidiwa kirahisi kuliko kurudishwa mjini kusikokuwa na jamaa vinginevyo kama ni mwanaume unaweza kuolewa.
 
Gari ligeuze lirudi lilikotoka au hakuna pa kugeuzia?
 
Hao abiria hawana simu?hawana ndugu wa kuwapigia ili wawasaidie kutoa taarifa kunako husika?wamiliki wa mabasi yaliokwama huko kwanini hawatoi taarifa za kuomba msaada wa kunusuru mabasi yao na abiria wao au wameamua kuyatelekeza?kama hii taarifa ni ya kweli basi kutakuwa kuna uzembe mkubwa sana hasa kwa mamlaka zinazohusika na utoaji wa misaada ya dharura kama watakuwa wamepata taarifa...
 
Gari ligeuze lirudi lilikotoka au hakuna pa kugeuzia?
Mwenye gari anawaza mafuta aliyotumia na atakayotumia kuwarudisha atalipa nani maana kwa sheria za Sumatra abiria hawakufikishwa wanakokwenda nauli wanarejeshewa.
 
je hawawezi kurudi walipotoka kama wanakoenda hakuendeki. Nyoosha maelezo
 
weka picha
 
Hii ni yalini maana niliona Habari Kama hii juzi sehemu nilijibu ili tuweze kufikisha taarifa sahihi
 
Kuna hatari yakuzaliana hapo... Kisha kesi ziletwe kwa Rais wa Dathilamu

Ndugu yangu, watu wanakufa kwa njaa na kiu, na pengine kwa maradhi halafu wewe unaleta masuala ya mizaha! Tafadhali bwana. Hapa si mahala pake.
 
je hawawezi kurudi walipotoka kama wanakoenda hakuendeki. Nyoosha maelezo

Bila matengenezo hawawezi kuenda mbele wala kurudi nyuma. Wamekwama porini. Na hakuna mtu atapenda kukaa katika hali hatarishi kama ile kama kuna suluhu.
 

Taarifa hii ni ya kweli. Madreva na abiria wao wote wako porini.
Ndugu zao ni pamoja na mimi na wewe. Nidyo sababu tunapiga yowe hapa kuhitaji msaada wa haraka.
 
Mkuu sasa kama serikali itaweza kubeba madikodiko yote hayo (meaning itatumia usafiri fulani), si bora tu itumie usafiri huo huo kuokoa watu instead...

Unajua vikosi vya uokoaji vina namna yingi ya kufanya. Wanaweza kuwatupia hivyo vifurushi kwa Helicopter wakati matengenezo ya njia yanaendelea. Hayo si madiko diko. Ni suala la kuokoa uhai wa binadamu. Wako wengi na afya zao zinatofautiana..

Si suala la mizaha hili. Na mimi huwa sina mizaha linapokuja suala la maisha ya binadamu.
 
Nlitegemea hao waliopelekwa na silaha wangepelekwa na vyakula vya misaada, maji na madawa. Na usafiri uliowafikisha hao washika silaha ndo ungewabeba hao waliokwama.

Anyway ngoja tuendelee kuwaombea.

Nilitamani iwe hivyo pia. Nilitamani viongozi wetu wawe na uelewa wa kuchambua huduma na misaada inayohitajika kulinganan na tukio. Tukio la kukwama porini linahitaji huduma ya ulinzi na afya pia. Sijui kwa kweli kwa nini hawakuliona hili.
 
Serikali haijaleta mvua so hatuwezi kuwasadia,halafu hao wanatoka mbeya,hawakumchagua malaika wa Lucifa ni halali yao wakipate moto,ingekuwa wa kanda ya ziwa wangeokolewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…