Habari wadau? Leo nilifika kwenye eneo lililochangamka ghafla kwa usafiri wa mabasi ya kwenda nje ya Dar es Salaam, pale Shekilango-Ubungo.
Safari yangu pale ilikuwa kusafirisha mzigo kwenda mkoa mmoja uliyopo Kanda ya Ziwa.
Nikiwa naendelea kuhudumiwa, nilishangaa namna mabasi yalivyo mengi na mazuri tena ya kisasa na jinsi mahali pale palivyochangamka kwa sasa.
Nilipomaliza kilichonipeleka, ndipo nikaanza kuwauliza baadhi ya wasafiri kwa siku hiyo na waliyokwishasafiri au kusafirisha mizigo ambao walikuwa tayari kuongea na mimi, kwamba ni kampuni gani ya mabasi inatoa huduma kwa wateja (customer care) nzuri kuliko nyingine.
Lengo langu lilikuwa kupata Top Ten tu. Na maswali yangu yalilenga huduma bora na siyo mabasi bora au mazuri.
Nilizingatia:
1. Mapokezi kwa abiria.
2. Kauli za wahudumu kwa abiria au wateja.
3. Uzingatiaji muda wa basi kuondoka.
4. Usalama wa mizigo inayopakiwa kwenda mikoani.
5. Ukarimu wa wahudumu kwa abiria njiani.
6. Kumchukulia abiria ule msemo wa 'mteja ni mfalme' nk.
Baada ya kuongea na abiria hao sanjari na wasafirishaji mizigo wanaotumia mabasi hayo, nikapata Top Ten yangu na idadi ya abiria waliyoyataja mabasi hayo ikiwa kwenye mabano:
1. Shabiby Line (watu 18).
2. BM Coach (watu 15).
3. Abood Bus (watu 14).
4. ABC Coach (watu 12).
5. Ester (watu 11).
6. Kimbinyiko (watu 9).
7. Ratco (watu 8).
8. Tahmeed (watu 8).
9. Ally's (watu 6).
10. Tilisho Safari (watu 6).
Kwa idadi ya mabasi ya kwenda mikoani kutokea Dar ilivyo, hawa 10 nawapa hongera yao.