Wasaidizi Samia Suluhu waomba AFCON iahirishwe hadi 2028

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,132
Reaction score
64,416
Ndo maana CAF hawataki Serikali kujihusisha na Mpira.

Wasaidizi wa anayejiita Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, waomba AFCON iahirishwe hadi 2028.

Wanadai Viwanja na maandalizi hayatakuwa yamekamilika. Wanadai eti Kenya itakuwa kwenye Uchaguzi Mkuu kwamba kunaweza kukatokea Vurugu.

Kwanini waseme Kenya Kutatokea Vurugu?

Aliyekula nyama ya binadamu haachi.

Timu ya ukaguzi kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwa sasa ipo Tanzania na inatarajia kufanya kikao kuhusu maandalizi ya michuano hiyo.
 
Prof mhongo alifeli mara nyingi tu
Kuwa mke wa tatu ni kukosa maadili, unajua maana ya maadili!?..no wonder gt wamekimbia JF
 
Mpira ni burudani. Katika hali ya kawaida, hakuna burudani kwa mtu anayeomboleza. Watanzania bado wanaomboleza, hata miili tu ya ndugu zao ambao waliuawa na watawala haramu haijapatikana! Kuna furaha gani kuingia kwenye burudani tukiwa kwenye mazingira ya namna hiyo? Michezo ya AFCON iendelee kwa mataifa yaliyopo katika furaha. Hapa kwetu, hapana. Wakilazimisha, wataaibika, maana hata watakaoenda huko uwanjani, ni hawa machawa wachache sana, itakuwa aibu ya mwaka, timu zikicheza zikiwa na mashabiki wageni bila ya wananchi wenyeji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…