Hakuna binadamu aliye mkamilifu. Rais SSH alifanya makosa kwa kutoa kauli zisizo "sahihi" ktk interview yake na Salum Kikeke wa BBC.
Hilo siyo jambo geni kumtokea kiongozi yeyote yule. Kinachofanyika ktk mazingira kama hayo ni kiongozi mwenyewe, au wasaidizi wake, kujitokeza kuomba RADHI na kurekebisha makosa yaliyojitokeza.
Nashangaa kwanini mpaka sasa hivi hakuna mtu wa IKULU aliyejitokeza kurekebisha kauli alizotoa Rais. Ukimya huu wa Rais SSH, pamoja wasaidizi wake, unaweza kuleta hisia kwamba Rais hakukosea kibidamu, bali alifanya makusudi au alidhamiria kutoa majibu yale.
Zaidi ya kuharibu taswira ya Rais na kuporomosha heshima yake, hali hiyo inatoa mwanya kwa Rais kuitwa majina mabaya yenye kumvunjia heshima.
Hivi kweli Rais SSH ameridhika na majibu aliyotoa kwa BBC? Je, wasaidizi wake wanadhani Rais ametenda sawa, na kwa kukaa kimya wanamtendea haki Rais?
Nawasihi wasaidizi wa Rais wajitokeze kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza, na kuwaomba RADHI wananchi.
cc Richard, Nguruvi3 , Pascal Mayalla, Sesten Zakazaka