Wasaidizi wa Rais Samia warekebishe makosa aliyofanya katika mahojiano na BBC, vinginevyo ataonekana siyo muungwana

Yaani wewe jolojolo yaani huyo mwanamke uwezo mdogo uwezo wa kujieleza Hana kweli kila kitu madawa hospitalini utafikiri hata hayo madawa yapo ,,, msimruhusu tena kuhojiwa na mwandishi yeyote mbona Magu alikuwa mwoga kuhojiwa na vyombo hivi vya kimagharibi sabb alihofia kukosea ,, mama anajifanya mjuaji hata uwezo wake mdogo sana
 
Kwani yeye anasemaje ameomba msaada wa kurekebisha rais hamywi bia anajua kila kitu
 
Mbona tunaambiwa nchi inaongoza kwa rasilimali Africa nzima
Sawa inaongoza, je inatunufaisha kwa kiwango tunachokihitaji? Jibu ni hapana kwa sababu wengi wanataka kuzitumia rasilimali zetu kujinufaisha wao zaidi. Mfano Bandari ya Bagamoyo hadi sasa mradi umekwama kwa sababu masharti ya mwekezaji yanalenga kujinufaisha Yeye zaidi
 
Kinachotakiwa ni kuwaondoa waliompotosha kwenye nafasi zao.
Hilo ni zaidi ya kuomba radhi kwe wenye akili.
Hata kama ni washirika wake wa kutegemewa sana, aweza kubadili vyeo vyao ili kuongeza ufanisi na pia kuonesha kutoridhika na yaliyotokea.
Nyakati za kutumia ubabe wa wazi bila akili zimepita.
Washauri lazima wawe na uwezo wa kutumia akili nyingi na nguvu kidogo ili mambo yaende.
 
Wengi wa kina nani acha propaganda na uongo wa kitoto, bunge wabunge wote ni waccm, rais wa ccm wanashindwa nin kupitisha Sheria zitakazolinda rasilimali na kuinufaiha nchi
 
..mtu yeyote MUUNGWANA huwa anaomba radhi pale anapokosea.

..Na anayeomba radhi ni mtu anayejiamini na JASIRI kuliko yule asiyeomba radhi.

..Mtu mgumu kuomba radhi naamini ni dhaifu mwenye inferiority complex.

 
Ila kwa mwanamke kuwa mwongo au katili na dikteta uchwara haipendezi...

Mama aombe tu radhi, tutamsamehe bila shaka...

Mwanamke kuwa mwongo haileti picha nzuri...!!
 
Hakuna mwomba msamaha hapo yaani mara hii mmesahau namna uchaguzi wa wenye viti wa mitaa ulivyoendeshwa? hicho alichokisema ndicho kiujazacho moyo wake jamani .

Sent from my SM-A307FN using JamiiForums mobile app
 
Mkwere aliitwa majina yote, Mkapa aliitwa majina yote, Mwinyi aliitwa majina yote na Magufuli pia, nini kitakuwa cha ajabu kwa Samia?
 
Nahisi big [emoji102] hana hadhi ya kuendesha hata kino tumepigwa mchana kweupe Kuna siku moja tutamkumbka mwamba flan hivi kwa vitendo si maneno
 
Mkwere aliitwa majina yote, Mkapa aliitwa majina yote, Mwinyi aliitwa majina yote na Magufuli pia, nini kitakuwa cha ajabu kwa Samia?

..Waswahili wana msemo " bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi. "
 
Kazi ya Urais kwa nchi zetu za "Afrika" si kazi ya uungwana, Rais haombi msamaha....kiufupi raia hawana mamlaka ya kuombwa msamaha na Rais wao kwa sababu hawana mamlaka ya kuamua kumpa au kumnyang'anya nafasi ya Urais!
..Maraisi wa wenzetu wanaomba msamaha.

 
Nimefedheheshwa sana na interview ile, inatupunguzia credibility kama nchi
 
Nguvu ya MAOMBI watu wamefunga wanasali

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Alishasema yeye ni Rais hakosei
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…