Wasamaria:Fahamu chanzo chao na kwanini walikuwa hawachangamani na Wayahudi!

Wasamaria:Fahamu chanzo chao na kwanini walikuwa hawachangamani na Wayahudi!

ChamaDola

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2016
Posts
3,431
Reaction score
2,804
Wakuu,

Unapofungua Agano Jipya,hasa katika zile Injili Nne,utakutana na uadui kati ya Wayahudi dhidi ya Wasamaria!

Ila ushawahi jiuliza chanzo cha ukinzani huu? Basi twende sote tupate kujua!

Ukirudi nyuma kidogo katika Agano la Kale utakutana na Mfalme Suleiman!

Baada ya kuikinikia hekima aliyoiomba na kupewa na Mungu,Mungu aliamua kuugawa

ufalme katika vipande viwili hasimu:Ufalme wa Yuda upande wa Kusini na Israel upande wa kaskazini!

Kwa kuwa Mungu hakutaka kuutia doa ufalme wa Suleiman ili kutokuvunja agano lake

aliloliweka na Mfalme Daudi,basi kumrundia heshima Daudi,alisubiri Suleiman afe, ndipo auchane pawili ufalme kama adhabu dhidi ya uasi wa Suleimani kwa Mungu kwa kuleta

ibada ya shetani na miungu ya kigeni kupitia mamia ya wake wa kigeni aliyowaoa!

Punde, Suleiman alipovuta pumzi ya mwisho,Israeli ikachanwa katikati! Makabila kumi yakaasi na kujiunga na Jeroboam na akaanzisha ufalme wake,huku makao makuu yakiwa katika mji wa Samaria! Makabila mawili yakajiunga na kutengeneza ufalme wa Yuda yakiongozwa na Rehoboam mtoto mkubwa wa Mfalme Suleiman!


Pia kumbuka,kabila pekee lilikokuwa na mamlaka ya kutoa mfalme lilikuwa la Yuda! Ila cha ajabu,Jeqoboam alikuwa wa kabila la Ephraim! Dharau namba moja! Kama haitoshi Hekalu la Suleiman lilikuwa Yerusalem kule Yuda, kwahyo kila mwaka Wayahudi wa Samaria wafunge safari ya kuja hekaluni! Jambo hili likamkera Mfalme Jeroboam! Naye pasipo kumuomba Mungu ushauri,akaamua kujitengenezea ndama wawili,katika mji wa Betheli ili Wayahudi wa Samaria wasiende Yerusalem! Jambo hili lilimkera Mungu sana! Uadui uliendelea!


Ila ulikua zaidi mwaka 722 Kabla ya Kristo,baada ya ufalme kupinduliwa na maelfu ya

waisraeli wa Samaria kubebwa utumwani na jeshi la Wassyria! Na mfalme aliyeshinda, akaamua kuleta watu wa mataifa mbali kutoka katika makoloni yake toka Ninawi mpaka Babylon ili wautunze mji na kuilima ardhi! Lengo lake ilikuwa ni kuzima jitihada zote za Wayahudi wa Samaria kujitutumua tena ili kupinga utawala wake! Na pia kutoa somo kwa makoloni madogo kuwa yasithubutu kuleta fyokofyoko! Lakini cha ajabu,nchi ya Samaria ikaanza kuvamiwa na Simba wala watu!


Baada ya watu kusosiwa kwa muda mrefu na taarifa kumfikia mfalme wa Assyria,ikabidi kuhani wa Kiyahudi atafutwe! Baada ya upepelezi,ikaonekana Yahweh hajapendezwa na

miungu ya wakazi wapya wa Samaria,hivyo kuhani akatumwa kwenda Samaria ili

kuwafundisha watu amri za Yahweh!


Baada ya hali kutulia,mwaka 586 Kabla ya Kristo ufalme wa kusini nao ukaanguka kwa mkono wa Nebukadneza! Wayahudi wa Samaria hawakuwahi kurudi Samari,na huo ukawa mwisho wa hayo makabila kumi! Ila yale makabila mawili ya kusini,yalirudi chini ya uongozi wa Nehemia na Ezra! Kwahyo mbele ya Wayahudi,hawa wakazi wapya

wa Samaria,na baadaye katika Agano Jipya wakiitwa walikuwa ni Walowezi,nusu watu na wa mataifa! Walikuwa na haki zote za kuwachukia! Japo Kristo aliwatendea vizuri, kama yule mwanamke msamaria pale kisimani,mpaka hekalu linavunjwa mwaka 70

Baada ya Kristo "bifu" liliendelea!
 
Nadhani hoja yako ina matege kidogo, SIO KAMA WASAMARIA WALIKUWA HAWACHANGAMANI NA WAYAHUDI, usahihi ni Kuwa WAYAHUDI WALIKUWA HAWACHANGAMANI NA YOYOTE ASIYE MYAHUDI

Wayahudi walikuwa na Amri ya kumpenda jirani yako, na Jirani wa Myahudi ni Myahudi na sio mtu yoyote yule awe Myunani, mwarabu, Msamaria nk, (Ushahidi wa maandiko upo, soma injili yako vizuri),kwa Myahudi hata kama next door yuko Yoyote asiye Myahudi huyo sio jirani, jirani ni myahudi aliye hata mita 100, na hili ilitokana na Imani tofauti walizokuwa nazo watu waliokuwa wakiishi pamoja na Wayahudi

Yesu ndio aliyekuja kuwafundisha Wayahudi kuwa Jirani sio kabila au imani moja- Yesu aliibadirisha Sheria ya kimwili na kuifanya ya Kiroho, Ukisoma habari za wanyanganyi Waliomkaba Myahudi na kumjeruhi utaona Wayahudi wenzie (Wanasheria-Walawi, Mahakimu-Kadhi) walishindwa kumsaidia, na Alipofika Msamaria alimsaida so Yesu akawauliza Jirani ni nani?, na hapo Wayahudi wakapata concept ya Sheria za Kiroho zaidi ya za Kimwili

Hata Yesu alipokutana na mwanamke Msamaria pale Kisimani kwa Yakobo, alimwambia sisi (Wasamalia) hatuchangamani na Wayahudi iweje wewe uniombe maji? (yaani Myahudi hawezi kamwe kuomba msaada kwa Wasamali au kwa Yoyote asiye Myahudi- ilikuwa ni Sheria yao) Mwisho akamwambia wote Wayahudi, Wasamaria na wengineo wataabudu Mungu mmoja katika roho na Kweli

Kifupi Wayahudi ndio walikuwa na Sheria ya kuwabagua wasio Wayahudi
 
tajiri wa mwanza la hasha,hiyo uisemayo,inawahusu waisraeli wa kusini katika ufalme wa Yuda,baada ya kurudi toka utumwani!
Upande wa kaskazini,yaani Samaria hawakurudi toka utumwani kabisa!
 
Kituko nimeuelewa ukosoaji,na hoja ni kama hiyo uliyoandika,labda kama umenisoma vibaya!
 
Kituko nimeuelewa ukosoaji,na hoja ni kama hiyo uliyoandika,labda kama umenisoma vibaya!

Tatizo kichwa cha Thread yako ndio kina shida, wewe umemaanisha kuwa Wasamaria ndio walikuwa hawachangamani na Wayahudi, lakini huo sio ukweli, Ukweli ni kuwa Wayahudi ndio walikuwa Hawachangamani na Wasamaria , Badirisha Kichwa cha uzi wako
 
Tatizo kichwa cha Thread yako ndio kina shida, wewe umemaanisha kuwa Wasamaria ndio walikuwa hawachangamani na Wayahudi, lakini huo sio ukweli, Ukweli ni kuwa Wayahudi ndio walikuwa Hawachangamani na Wasamaria , Badirisha Kichwa cha uzi wako

Kama maji hayachangamani na mafuta nitakuwa nimekosea nikisema mafuta hayachangamani na maji???

Au "kiuswaziuswazi" ni sawa ila kibiblia sio sawa?
 
Kama maji hayachangamani na mafuta nitakuwa nimekosea nikisema mafuta hayachangamani na maji???

Au "kiuswaziuswazi" ni sawa ila kibiblia sio sawa?

Haina uhusiano na hilo aliloliandika mtoa maada, Wayahudi walikuwa wakiishi kwa kutumia Sheria Torati, na wao walikuwa na Mungu wao ambaye alikuwa ni tofauti na Mungu wa Mataifa mengine, Hivyo wao KWENYE SHERIA ZAO NDIO WALIOAMBIWA WASICHANGAMANE NA WATU WENGINE, YESU ALIKUJA KUZIBADIRISHA HIZO SHERIA ZA KIMWILI NA KUZIFANYA KUWA ZA KIROHO
 
Mtoa mada hebu tueleze injili kwa nini ziko nne?na yesu alipewa moja tu ?

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Haina uhusiano na hilo aliloliandika mtoa maada, Wayahudi walikuwa wakiishi kwa kutumia Sheria Torati, na wao walikuwa na Mungu wao ambaye alikuwa ni tofauti na Mungu wa Mataifa mengine, Hivyo wao KWENYE SHERIA ZAO NDIO WALIOAMBIWA WASICHANGAMANE NA WATU WENGINE, YESU ALIKUJA KUZIBADIRISHA HIZO SHERIA ZA KIMWILI NA KUZIFANYA KUWA ZA KIROHO

Unaweza kunisaidia sehemu yoyote ya Torati inayoonesha Wayahudi wasichangamane kabisa na mataifa/makabila mengine yasiyoabudu Mungu wao? Niko interested kujifunza hapa zaidi
 
Mtoa mada hebu tueleze injili kwa nini ziko nne?na yesu alipewa moja tu ?

Post sent using JamiiForums mobile app

Hivi ni injili ziko NNE au ni Vitabu vya Injili viko Vinne (kumaanisha vimeandikwa na watu wa4 tofauti) lakini Injili ni moja?
 
Itakuwaje iandikwe na watu wanne na kila moja ina utofauti na nyengine? Iliyo kuwa sawa ni ipi ?

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Tusikuvunje moyo umu ila jitahidi kusoma kwa bidii sana biblia maana unaonekana unapenda kujifunza na kushare na wenzako.

Pili jitahidi pia kujenga hoja wakati unaandika pia kichwa kiendane na main body ili kuleta kitu murua zaid ya hiki.

Napenda sana kusoma mambo kama hayo.

Wayahudi walikuwa watu pekee walioteuliwa na Mungu mwenyewe kuwa kama taifa teule la kumuwakilisha Mungu duniani kwa kutenda na shika kanuni za mbinguni.

Uteuzi huu uliwakilishwa na tohara yaani kila myahudi ni lazma atahiriwe na hii ni baada tu ya mtoto kuzaliwa akifikisha umri flani bas anatimiza agano la kuwa myahudi kwa kutahiriwa.

Kwa dhana hio basi kukawa na hali flani ya wayahudi kujiona wao kuwa ni bora zaidi ya wengine.

Kwahiyo si kwa wasamaria tu bali ilikuwa ni kwa kila ambaye hakuwa myahudi walijiwekea mipaka kuwa hawaruhusiwi kuchangamana nao.

Hili lilikuwa ni tatzo na ndio maana kristo anapokutana na mwanamke msamaria kisimani anamwambia nipe maji ninywe si kama yesu hakujua sheria ya kutochangamana bali alikuwa anaonyesha kuwa hakuna cha myahudi wala myunani wala mpagani bali wote baba yetu ni mmoja Mungu wa mbinguni hivyo alikuja kuvunja huo ukuta ambao wayahudi waliujenga dhidi ya mataifa yasio ya kiyahudi.
Asante mtoa mada.
 
Unaweza kunisaidia sehemu yoyote ya Torati inayoonesha Wayahudi wasichangamane kabisa na mataifa/makabila mengine yasiyoabudu Mungu wao? Niko interested kujifunza hapa zaidi

Sura ziko nyingi sana kaka, we soma Agano la Kale utaelewa:

Mfano

Kumbukumbu la Torati 7
1 Bwana, Mungu wako, atakapokutia katika nchi uendayo kuimiliki, atakapoyang'oa mataifa mengi watoke mbele yako, Mhiti, na Mgirgashi, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi, mataifa saba makubwa yenye nguvu kukupita wewe;
2 wakati Bwana, Mungu wako, atakapowatoa mbele yako, nawe utawapiga; wakati huo ndipo uwaondoe kabisa; usifanye agano nao, wala kuwahurumia; wala usioane nao;
3 binti yako usimpe mwanawe mume, wala usimtwalie mwanao mume binti yake.
4 Kwa kuwa atamkengeusha mwanao mume asinifuate, ili wapate kuabudu miungu mingine; ndipo itakapowaka hasira ya Bwana juu yenu, naye atakuangamiza upesi.
5 Lakini watendeni hivi; zivunjeni madhabahu zao zibomosheni nguzo zao, yakateni maashera yao, ziteketezeni kwa moto sanamu zao za kuchonga.
6 Kwa maana wewe u taifa takatifu kwa Bwana, Mungu wako; Bwana Mungu wako, amekuchagua kuwa watu wake hasa, zaidi ya mataifa yote walioko juu ya uso wa nchi.
7 .....
16 Nawe angamiza mataifa yote atakayokupa Bwana, Mungu wako; jicho lako lisiwahurumie, wala usiitumikie miungu yao; kwani litakuwa ni mtego kwako jambo hilo.

Kumbukumbu la Torati 20

16 Lakini katika miji ya mataifa haya akupayo Bwana, Mungu wako, kuwa urithi, usihifadhi kuwa hai kitu cho chote kipumzikacho;
17 lakini uwaangamize kabisa, Mhiti, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi, kama alivyokuamuru Bwana, Mungu wako;
18 wasije wakawafunza kufanya mfano wa machukizo yao yote, waliyoifanyia miungu yao; hivyo itakuwa ni makosa juu ya Bwana, Mungu wenu.

 
Watu wanapenda na kujua historia ya Wayahudi na Wasamaria walioishi miaka maelfu na maelfu mbali huko, lakini ukiwauliza historia ya Mwanamalundi, Kinjekitile, Mkwawa au David Kidaha Makwaia walioishi takriban miaka mia moja iliyopita kwetu hawaijui.

Hili ni jambo la aibu.

Ndiyo maana inakuwa rahisi kutuaminisha kwamba sisi si watu kamili.
 
Back
Top Bottom