Wakuu,
Unapofungua Agano Jipya,hasa
katika zile Injili Nne,utakutana na
uadui kati ya Wayahudi dhidi ya
Wasamaria!
Ila ushawahi jiuliza chanzo cha
ukinzani huu?
Basi twende sote tupate kujua!
Ukirudi nyuma kidogo katika
Agano la Kale utakutana na
Mfalme Suleiman!
Baada ya kuikinikia hekima
aliyoiomba na kupewa na
Mungu,Mungu aliamua kuugawa
ufalme katika vipande viwili
hasimu:Ufalme wa Yuda upande
wa Kusini na Israel upande wa
kaskazini!
Kwa kuwa Mungu hakutaka
kuutia doa ufalme wa Suleiman ili
kutokuvunja agano lake
aliloliweka na Mfalme Daudi,basi
kumrundia heshima
Daudi,alisubiri Suleiman
afe,ndipo auchane pawili ufalme
kama adhabu dhidi ya uasi wa
Suleimani kwa Mungu kwa kuleta
ibada ya shetani na miungu ya
kigeni kupitia mamia ya wake wa
kigeni aliyowaoa!
Punde,Suleiman alipovuta pumzi
ya mwisho,Israeli ikachanwa
katikati!
Makabila kumi yakaasi na
kujiunga na Jeroboam na
akaanzisha ufalme wake,huku
makao makuu yakiwa katika mji
wa Samaria!
Makabila mawili yakajiunga na
kutengeneza ufalme wa Yuda
yakiongozwa na Rehoboam
mtoto mkubwa wa Mfalme
Suleiman!
Pia kumbuka,kabila pekee
lilikokuwa na mamlaka ya kutoa
mfalme lilikuwa la Yuda!
Ila cha ajabu,Jeqoboam alikuwa
wa kabila la Ephraim!
Dharau namba moja!
Kama haitoshi Hekalu la Suleiman
lilikuwa Yerusalem kule
Yuda,kwahyo kila mwaka
Wayahudi wa Samaria wafunge
safari ya kuja hekaluni!
Jambo hili likamkela Mfalme
Jeroboam!
Naye pasipo kumuomba Mungu
ushauli,akaamua kujitengenezea
ndama wawili,katika mji wa
Betheli ili Wayahudi wa Samaria
wasiende Yerusalem!
Jambo hili lilimkera Mungu sana!
Uadui uliendelea!
Ila ulikua zaidi mwaka 722 Kabla
ya Kristo,baada ya ufalme
kupinduliwa na maelfu ya
waisraeli wa Samaria kubebwa
utumwani na jeshi la Wassyria!
Na mfalme aliyeshinda,akaamua
kuleta watu wa mataifa mbali
kutoka katika makoloni yake toka
Ninawi mpaka Babylon ili
wautunze mji na kuilima ardhi!
Lengo lake ilikuwa ni kuzima
jitihada zote za Wayahudi wa
Samaria kujitutumua tena ili
kupinga utawala wake!
Na pia kutoa somo kwa makoloni
madogo kuwa yasithubutu
kuleta fyokofyoko!
Lakini cha ajabu,nchi ya Samaria
ikaanza kuvamiwa na Simba wala
watu!
Baada ya watu kusosiwa kwa
muda mrefu na taarifa kumfikia
mfalme wa Assyria,ikabidi kuhani
wa Kiyahudi atafutwe!
Baada ya upepelezi,ikaonekana
Yahweh hajapendezwa na
miungu ya wakazi wapya wa
Samaria,hivyo kuhani akatumwa
kwenda Samaria ili
kuwafundisha watu amri za
Yahweh!
Baada ya hali kutulia,mwaka 586
Kabla ya Kristo ufalme wa kusini
nao ukaanguka kwa mkono wa
Nebukadneza!
Wayahudi wa Samaria
hawakuwahi kurudi Samari,na
huo ukawa mwisho wa hayo
makabila kumi!
Ila yale makabila mawili ya
kusini,yalirudi chini ya uongozi
wa Nehemia na Ezra!
Kwahyo mbele ya
Wayahudi,hawa wakazi wapya
wa Samaria,na baadaye katika
Agano Jipya wakiitwa walikuwa
ni Walowezi,nusu watu na wa
mataifa!
Walikuwa na haki zote za
kuwachukia!
Japo Kristo aliwatendea
vizuri,kama yule mwanamke
msamaria pale kisimani,mpaka
hekalu linavunjwa mwaka 70
Baada ya Kristo "bifu" liliendelea!