Wasanii 10 wanaoongoza kwa pesa nchini India

mankachara

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2013
Posts
6,152
Reaction score
3,473
1) SHAHRUKH KHAN (UTAJIRI$600 Million)
Huyu ndie actor namba moja mwenye mkwanja mrefu kwa india, wenyewe wahindi wanamwita “THE KING OF BOLLYWOOD” . amezaliwa 2 November mwaka 1965 mjini New delhi, mkewe anaitwa Gauri Khan sliyemuoa mwaka 1991 na mpaka sasa ana watoto 3. Kama ni mtazamaji kidogo wa bollybood nafikiri utakua umeshawahi kumuona. Miongoni mwa movie zake kali ni My name is khan, Kuch Kuch Hota hai, Kal Ho Naa Ho, Devdas na kama unapenda kulia angalia Veer Zara lazima utatoka machozi. Sharuki sio wa kwanza kwa India tu bali pia ni actor wa pili mwenye mkwanja mrefu kwa dunia nzima akitangliwa na Jery Seinfeld


2) AMITABH BACHCHAN (UTAJIRI $400 Million)
Anaitwa Amitabh Harivansh Rai Shrivastava Bachchan, ni actor wa pili mwenye mkwanja mrefu kwa upande wa india, na pia ni actor wa 6 kwa dunia nzima. Amezaliwa October 11, 1942 katika mji uitwao Allahabad Nanda. Mkewe anaitwa Jaya Bhaduri Bachchani aliemuoa 1973. Amitabh ana watoto watatu tu na ameshapokea zawadi nyingi akiwa kama actor bora. Miongoni mwa movie alizoact ni Shalay, Zanjeer, Silsila, Paa, Bigg boss, who wants to be a millionair


3) SALMAN KHAN (UTAJIRI $200 Million)
licha ya kukutwa na kashfa nyingi pamoja na kufungwa jela kwa muda, Abdul Rashid Salim Salman Khan ni actor wa tatu mwenye mkwanja mwingi kwa india. Amezaliwa December 27, 1965 huko Indore nchini india. Ameact movie kama Sultan,Bajrangi Bhaijaan, Kick, Bodyguad na kama ni mtu wa mambo ya interlligencia ana movie inaitwa Ek Tha Tiger


4) AAMIR KHAN (UTAJIRI $185 Million)

Kama ni muangaliaji wa hizi bollybood nafkiri utakua umeshawahi kumuona huyu kiumbe na hata mimi pia namkubali sana maana movie zake nyingi zinaelezea kuhusu mabadiliko na challenge mbali mbali kuhusiana na elimu pamoja na mambo ya dini. Aamir Khan amezaliwa march 14, 1965 mji wa Mumbai nchini India. Amemuoa Reena Dutta 1986 na wakaachana na 2005 amemuoa Kiran Rao. Na mpaka sasa ana watoto watatu. Kwa ukweli movie zake ni challenge

Ana movie inayoitwa Pk inayoeleza juu ya uwepo wa mungu katika dini mbalimbali, movie nyengine inaitwa Laagan inaeleza jinsi waingereza walivokua wakiwatesa wahindi, kuna movie inaitwa Ghajini inaeleza mtu mwenye matatizo ya ubongo baada ya kupata majeraha na anasahau kila baada ya dakika 15, kuna movie inaitwa Dhoom 3 unaweza kuenjoy sana ukiiangalia, kuna nyengine inaintwann Taare Zameen Par inaeleza motto mwenye ugonjwa Fulani, movie hii imempatia fedha nyingi sana. Na kuna movie inaitwa 3 idiot, kama wewe ni motto wa college iangalie hii movie, utajifunza sana na natumai wengi mumeshaiangalia



5) AKSHAY KUMAR (UTAJIRI $100 Million)
Anaitwa Rsjiv Hsri Om Bhstia na umaarufu wake ni Akshay Kumar ni actor wa tano mwenye mkwanja mwingi kwa india. Amezaliwa September 9, 1967 huko Amritsar nchini india. Amemuoa Twinkle Khanna 2001 na ana watoto wawili, Ameact movie kama airlift, Baby, Rustom, gabbar is back


6) HRITHIK ROSHAN (UTAJIRI $70 million)



7) RANBIR KAPOOR (UTAJIRI $66 Million)



8) SANJAY DUTT (UTAJIRI $55 Million)



9) JOHN ABRAHAM (UTAJIRI $55 Million)


10) SAIF ALI KHAN (UTAJIRI $40 Million)
 
karibuni wapenzi mliokua mnaangalia bila ya kujua nani yuko juu huko india
 
Shahrukh Khan hana mpinzani.
Jamani huyu baba nampenda mnooo!
Wapi Sunil Shety?Sun Deo?
Mimi sio mfuatiliaji wa movie za kihindi sana.
Ukipata wasaa tuandalie list ya Wakorea mkuu...
Asante.
 
PK-India highest grossing film of all time (US$120 million)................
Sequal yoyote ya Batman box office ikifanya hivyo ni flop....Anyway,I think most of those actors' wealthy is overrated.
 
Mkuu uko vizuri na unafuatilia sana hivi vitu,na hawa jamaa wa India wanapiga pesa ndefu sana tena kimya kimya. Japo hapo ukija kidunia imeshakuwa si hivyo tena orodha hii hapa Top 10 Richest Actors in 2016 – Real Net Worth - The Gazette Review
 
Shahrukh Khan hana mpinzani.
Jamani huyu baba nampenda mnooo!
Wapi Sunil Shety?Sun Deo?
Mimi sio mfuatiliaji wa movie za kihindi sana.
Ukipata wasaa tuandalie list ya Wakorea mkuu...
Asante.
Asante sana, nitaanda ili kuwaelewesha wapenzi wa korea drama na action movie
 
Mkuu uko vizuri na unafuatilia sana hivi vitu,na hawa jamaa wa India wanapiga pesa ndefu sana tena kimya kimya. Japo hapo ukija kidunia imeshakuwa si hivyo tena orodha hii hapa Top 10 Richest Actors in 2016 – Real Net Worth - The Gazette Review
Wahindi wanapenda utamaduni wao, wanaenda tengeneza film new york, london lakini unakuta wanaeleza utamaduni wao ule ule, management zao ziko vizuri katika kuhakikisha wanatoa film itakayomfanya mtazamaji aifahamu hata kama haina subtittle
 
Vipi kuhusu Govinda?
ingawa govinda ametamba kwa muda wake, na amekua maarufu kwa movie kama Saajan chale sasural, Naseeb, Hero No. 1, Hum. Kwa kipindi kirefu hajahit sana kwenye game
 
Huyu Sanjay Dutt kaanza haya mambo muda mrefu sana mbona hana mafanikio?
 
karibuni wapenzi mliokua mnaangalia bila ya kujua nani yuko juu huko india
King Khan apart from Bolywood richest movie star pia ni msanii no 2 kwa utajiri Kidunia!
Pia Aamir Khan ameazaliwa 1975
Nawapenda sana wahindi hapa naangalia tamthilia ya kihindi inayoiywa KRISHNADAS!!
 
SRK a.k.a fundi, my name is khan ndo filamu bora kuwahi kuitazama ikifuatiwa na raaz 3 ya emran hashmi
 
Teh binamu tukae tu nyumba moja, unafatilia tamthilia zao zeeworld?
hahaaa!tutaenjoy balaa!
AZAM hawana Zee TV,wana Colors,Star plus,Star gold na nk.Ila enzi hzo tuna DSTV kihome home nlikua naangaliaga sana tamthilia zao!
 
Jamani movie ya FAN mie ndo movie yangu ninayoitazama hata mata 4 kwa siku.
Shahrukh Khan ni nyoko aiseee......
hii fan ameigiza na nani? za kwake nazipenda zote hasahasa my name is khana, billu barber.. dah nyingi mno
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…