Lady Whistledown
JF-Expert Member
- Aug 2, 2021
- 1,147
- 2,008
Mapema wiki hii, imetrend habari imuhusuyo aliyekuwa Rapa Maarufu nchini Kenya, Colonel Mustafa baada ya kuonekana akifanya kazi za Ujenzi.
Katika mahojiano rapa huyo alikiri kuwa amelazimika kuingia mzigoni ili apate fedha za kumtibia Mama yake aliye mgonjwa wa Saratani. Wakenya wenye roho safi walijitolea kumchangia huku wengine wakipinga kwa kuhoji inakuwaje mtu mwenye uwezo wa kupata Ksh. 950,000 kwa mwezi kushindwa kuweka akiba?
Maswali ni Je, wanajua kuwa kuna dharura? Ugonjwa, ajali au kufilisika? Matukio kama hayo kama huna akiba utajua hujui, yaani hata kama kuna ndugu wa kukusaidia watachoka na cha moto utakiona.
Sasa basi ni vyema Maselebrity wetu kujifunza na kuchukua hatua kutokana na hili. Hii iwe tahadhari kwa wanamuziki na watu maarufu wa Tanzania kuwa makini na tabia zao za matumizi na mipango ya kifedha kwa ajili ya siku zijazo.
Na ili kuepuka kusimangwa wakati wa kuchangiwa ni muhimu kuzingatia yafuatayo:-
Weka akiba ya sehemu ya mapato yako kwa ajili ya matukio yasiyotarajiwa, dharura, na kustaafu. Hii inaweza kufanikiwa kwa kuwekeza, kuanzisha akaunti ya akiba, au hata kununua bima. Hautaimba au kuigiza milele, na kuna wakati soko lako kama brand linashuka, huu ndo wakati wa kutumia akiba huku ukisikilizia mishe zingine
Epukeni matumizi makubwa kwa matumizi yasiyo ya lazima na weka kipaumbele cha matumizi yako kwenye mambo muhimu zaidi. Mambo ya Kidimbwi kila Jumapili, sjui Elements kupop Moet na Kuletewa Henessy na Vitaa mpunguze
Wekeza katika biashara au sekta nyingine, au hata kujaribu fani ya uigizaji au fani nyingine zinazohusiana.
Tafuta ushauri wa kitaalam wa kifedha: Ni muhimu kutafuta ushauri wa kitaalam kutoka kwa washauri wa kifedha, wahasibu, au mawakili. Wataalam hawa wanaweza kukusaidia kufanya maamuzi sahihi na kukuelekeza kuelekea utulivu wa kifedha. Wengi wenu hata wana sheria hamna
Usipozingatia yanaweza yakakutokea yaliyomtokea Colonel au makubwa zaidi, halafu muanze kulia kulia Tanzania haiwathamini wanamuziki na wasanii wakongwe
Mwenye masikio na asikie