Wasanii na Celebrities wa Bongo mjifunze kupitia Colonel Mustafa, maana suala la akiba ni Kitendawili kwenu

Wasanii na Celebrities wa Bongo mjifunze kupitia Colonel Mustafa, maana suala la akiba ni Kitendawili kwenu

Attachments

  • mustafa.jpg
    mustafa.jpg
    7.5 KB · Views: 5
anaitwa Maryana na wimbo ule mkali mpaka leo
Huyu demu alikua wa moto Sana aisee enzi zile akaja achia lile Pini na "Chokoza" akiwa na arvil ndo Hadi likawa linatumika kama jingo pale EATV kwenye Friday Night Live FNL
 
Rage atoe wapi maigizo tu yale ili kupata followers wengi. Wanajua wafuatiliaji wa umbea wanasisimshwa sana na habari mlipuko kama zile.

Kuna kipindi fulani kuna producer wa muda mrefu sana wa video za muziki. Kipindi Diamond alipokwenda South Africa na Davido kufanya shooting ya wimbo wao ule sijui my number one, yule producer wa Tanzania akaulizwa kuwa inakuwaje wasanii wanaenda sana South Africa na kutumika kampuni za huko badala ya za hapa nyumbani. Jamaa akajibu hata yeye anashangaa wasanii wakienda huko wanatoa pesa huku wanatukopa.

Mtangazaji akamuuliza "unasema?!" Yule producer akasema kama kuna msanii alishawahi nilipa mimi hata milioni tatu tu naomba aje hapa ajitaje na ushahidi nitamtolea video ya wimbo wake mpya buure kwa gharama zangu. Jamaa kasema wazi wasanii huwa wanalia na kuomba kusaidiwa ili watolewe video zao au watatoa pesa kidogo.

Sasa kiukweli wasanii wetu wanakipato cha kawaida na kwa wale wenye kipato kizuri huwezi wakuta wanaongea ongea maana pesa huwa haikai kwa mtu muongeaji ila mtendaji.

Sasa jana natazama kipindi channel 5 producer aliyeproduce ile nyimbo ya zuchu inaitwa "Napambana" sijui. Anasema imegharimu milioni 36.[emoji23][emoji23][emoji23] Hivi unaijua kwa milioni 36 ?!

Nikaona vijana bado hawapo serious na showbiz na ndio maana hata mashabiki hawawachukulii serious. Nenda naijeria hapo wasanii wapo real sana na fans wao. Si kwenye filamu si kwenye muziki na ndio maana ni matajiri sababu wanapata sapoti ya ukweli.
kwanza nimpongeze sana jamaa maana hakujali kuabika wala nini ili kusimama na mama yake naamini Mungu yupo ipo siku atapata malipo yake na cha msingi radhi ya mama yake. Jamani tusidhanie pia ni mzembe hatuwezi jua maana ugonjwa wenyewe uliotajwa hata matajiri unawasumbua mno kifedha ni ugonjwa ambao unagarama kubwa mno. Inawezekana jamaa umemkwangua pesa yote. Siyo kila aliyekuwa nazo akifilisika ni kuwa hana akili au hakuwa akisevu . kuna mambo mengi, kuibiwa , kudhulumiwa n.k
 
Huyu demu alikua wa moto Sana aisee enzi zile akaja achia lile Pini na "Chokoza" akiwa na arvil ndo Hadi likawa linatumika kama jingo pale EATV kwenye Friday Night Live FNL
ila sasa hivi kanenepa mno ule uzuri umepungua
 
ila sasa hivi kanenepa mno ule uzuri umepungua
Da Maisha kupanda na kushuka aisee.. Ile huyo mwamba nilikua namkubali Sana yeye na Collo nimekaa Sana Kenya hawa jamaa kuna muda walitamba Sana.
Hata hizo picha zinazotrendi akifanya saidia fundi naona kama ndoto Maisha haya!!!!.
 
Kuna vitu ukikutana navyo lazima uivie Moshi. Kuna kesi mahakamani na kuuguza mgonjww
 
Rage atoe wapi maigizo tu yale ili kupata followers wengi. Wanajua wafuatiliaji wa umbea wanasisimshwa sana na habari mlipuko kama zile.

Kuna kipindi fulani kuna producer wa muda mrefu sana wa video za muziki. Kipindi Diamond alipokwenda South Africa na Davido kufanya shooting ya wimbo wao ule sijui my number one, yule producer wa Tanzania akaulizwa kuwa inakuwaje wasanii wanaenda sana South Africa na kutumika kampuni za huko badala ya za hapa nyumbani. Jamaa akajibu hata yeye anashangaa wasanii wakienda huko wanatoa pesa huku wanatukopa.

Mtangazaji akamuuliza "unasema?!" Yule producer akasema kama kuna msanii alishawahi nilipa mimi hata milioni tatu tu naomba aje hapa ajitaje na ushahidi nitamtolea video ya wimbo wake mpya buure kwa gharama zangu. Jamaa kasema wazi wasanii huwa wanalia na kuomba kusaidiwa ili watolewe video zao au watatoa pesa kidogo.

Sasa kiukweli wasanii wetu wanakipato cha kawaida na kwa wale wenye kipato kizuri huwezi wakuta wanaongea ongea maana pesa huwa haikai kwa mtu muongeaji ila mtendaji.

Sasa jana natazama kipindi channel 5 producer aliyeproduce ile nyimbo ya zuchu inaitwa "Napambana" sijui. Anasema imegharimu milioni 36.[emoji23][emoji23][emoji23] Hivi unaijua kwa milioni 36 ?!

Nikaona vijana bado hawapo serious na showbiz na ndio maana hata mashabiki hawawachukulii serious. Nenda naijeria hapo wasanii wapo real sana na fans wao. Si kwenye filamu si kwenye muziki na ndio maana ni matajiri sababu wanapata sapoti ya ukweli.
Kwa kweliii, wasanii hamna kitu ni fake tyuuh
 
2buRU0dO75NSYwueugG79nL2XDJmefwhvi1AYIYq.jpg

Mapema wiki hii, imetrend habari imuhusuyo aliyekuwa Rapa Maarufu nchini Kenya, Colonel Mustafa baada ya kuonekana akifanya kazi za Ujenzi.

Katika mahojiano rapa huyo alikiri kuwa amelazimika kuingia mzigoni ili apate fedha za kumtibia Mama yake aliye mgonjwa wa Saratani. Wakenya wenye roho safi walijitolea kumchangia huku wengine wakipinga kwa kuhoji inakuwaje mtu mwenye uwezo wa kupata Ksh. 950,000 kwa mwezi kushindwa kuweka akiba?

Maswali ni Je, wanajua kuwa kuna dharura? Ugonjwa, ajali au kufilisika? Matukio kama hayo kama huna akiba utajua hujui, yaani hata kama kuna ndugu wa kukusaidia watachoka na cha moto utakiona.

Sasa basi ni vyema Maselebrity wetu kujifunza na kuchukua hatua kutokana na hili. Hii iwe tahadhari kwa wanamuziki na watu maarufu wa Tanzania kuwa makini na tabia zao za matumizi na mipango ya kifedha kwa ajili ya siku zijazo.

Na ili kuepuka kusimangwa wakati wa kuchangiwa ni muhimu kuzingatia yafuatayo:-

Weka akiba ya sehemu ya mapato yako kwa ajili ya matukio yasiyotarajiwa, dharura, na kustaafu. Hii inaweza kufanikiwa kwa kuwekeza, kuanzisha akaunti ya akiba, au hata kununua bima. Hautaimba au kuigiza milele, na kuna wakati soko lako kama brand linashuka, huu ndo wakati wa kutumia akiba huku ukisikilizia mishe zingine

Epukeni matumizi makubwa kwa matumizi yasiyo ya lazima na weka kipaumbele cha matumizi yako kwenye mambo muhimu zaidi. Mambo ya Kidimbwi kila Jumapili, sjui Elements kupop Moet na Kuletewa Henessy na Vitaa mpunguze

Wekeza katika biashara au sekta nyingine, au hata kujaribu fani ya uigizaji au fani nyingine zinazohusiana.

Tafuta ushauri wa kitaalam wa kifedha: Ni muhimu kutafuta ushauri wa kitaalam kutoka kwa washauri wa kifedha, wahasibu, au mawakili. Wataalam hawa wanaweza kukusaidia kufanya maamuzi sahihi na kukuelekeza kuelekea utulivu wa kifedha. Wengi wenu hata wana sheria hamna

Usipozingatia yanaweza yakakutokea yaliyomtokea Colonel au makubwa zaidi, halafu muanze kulia kulia Tanzania haiwathamini wanamuziki na wasanii wakongwe

Mwenye masikio na asikie
Hiyo ni miaka michache unamuuguza mgonjwa!!!!!!!! Wakati huo maisha mengine yanatakiwa yaendelee!!!!!!!!!! Mtoa mada naomba uniambie kwa uwekaji wako wa akiba na kuwekeza utatoboa?????

Jaribu kuongea na Ocean Road Cancer Institute wakupe hali halisi ya kumuuguza mgonjwa wa cancer!!!!!!!!!

Post Address P.O.Box 3592
Tel: 2127597
Email: info@orci.or.tz
Dar Es Salaam. Tanzania

World Cancer Day 2017: Effective cure will happen in five ...​

The Independent
https://www.independent.co.uk › ... › Health News

2 Feb 2017 — An effective cure for all types of cancer could be just five to 10 years away, according to one of the world's leading experts on the ...

Understanding the Difference Between Cure and Remission
In a complete remission, all signs and symptoms of cancer have disappeared. If you remain in complete remission for 5 years or more, some doctors may say that you are cured.17 Jun 2019

Understanding Cancer Prognosis - NCI​

National Cancer Institute (.gov)
https://www.cancer.gov › about-cancer › diagnosis-staging

Nb: Omba Mungu akuepushe na kikombe hiki cha kuuguza mtu anayeumwa magonjwa ya muda mrefu kansa ni mfano tu!!!!!!! Halafu usione wewe ndiye unajua kuhusu kuweka akiba na kuwekeza!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Weka ngoma yake... Tumkumbuke...
 
Ugonjwa usikie tu... ingekuwa msanii mwingine sawa ila colonel mustafa ni moja ya wasanii waliokuwa wamejiwekeza kwenye biashara na mpunga alikuwa nao kimtindo... itakuwa gharama za matibabu zimemzidi
 
Back
Top Bottom