Wasanii wa Tanzania wanazingua mjue, mfumo wa maisha wanaoishi ni wa Kimarekani kabisa wanapokuwa na pesa zao ingawaje hatutakiwi kuwapangia cha kufanya.
Zikiisha na wakipatwa na matatizo wanataka kurudi kwenye mfumo wa Kitanzania tuwachangie.
SIsi watanzania wa vipato vya hali zote tutawachangia sawa, ila na sisi tukipatwa na majanga wao wasanii wanatusaidia nini?
Kuna watu kila siku wanatangazwa ITV wakiomba msaada wa kimatibabu husikii msanii fulani kusaidia, ila wanangoja kwenye majanga makubwa na kamera nyingi wajipatie umaarufu.
Wanaishi mfumo wa maisha wa kimarekani, sijawahi kusikia wamarekani wakimchangia Whitney Houston kutokana na tatizo lake la matumizi ya madawa.