DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Wasanii wa Bongo Flavour wameanza kutoa pole kwa familia na watu wote waliopoteza maisha katika maandamano ya kudai haki. Hata hivyo, ninaona ingekuwa vyema kama wasanii hawa wangetumia sauti zao kutoa nyimbo za kulaani vitendo vilivyofanywa na Jeshi la Polisi dhidi ya raia wasiokuwa na hatia, ambao baadhi yao walipigwa risasi bila sababu za msingi.
Ukweli ni kwamba, kwa sasa wasanii wengi nchini Tanzania wamekuwa kama kioo cha serikali, badala ya kuwa kioo cha jamii kama ilivyokuwa awali.
Ukweli ni kwamba, kwa sasa wasanii wengi nchini Tanzania wamekuwa kama kioo cha serikali, badala ya kuwa kioo cha jamii kama ilivyokuwa awali.