Mmhhh, kweli JF ni ya WOTE.
Umeambiwa wanataka mashairi? na hayo wanayoimba ni nini?
Kaazi kweli kweli.
Ndio watanzania sisi.
Jmushi,
Hawa jamaaa kama wangekuwa wanaelewa nini maana ya kazi yao basi kwa muda huu wala wasingekuwa wanaumiza vichwa kufikiria mashairi yaani sidhani kama wanatambua moja ya dhima ya Sanaa ni Kukanya/Kukosoa maovu na kuhimiza Marekebisho hasa ya maisha ya wananchi kwa ujumla wake, wao wanachofikiria ni MAPENZI TUUUUU, UNATEGEMEA TUTAFIKA KWELI..
Mimi ndio maana Prof Jay na nyimbo zake za NDIO MZEE na wimbo wa Nakaaya naukubali sana.
Wimbo wa Nakaaya
http://www.youtube.com/watch?v=KoqAmgywd80
Sorry Jmushi.
I am out of this!
Asante
FP
Hamna shida FP...Mimi niliulizia mashairi tu...Pamoja na radio zinazopiga songi hilo kwani nimelitafuta sijalipata.Bila ya hela hata heshima ya kwako hutaipata
Nyumbani wadogo zako hawatakwita tena kaka
Lazima utowe hela heshima ndio itakuja
Vinginevyo utasumbuka huku majasho yakikivuja
Hata ukigombea UBUNGE bila ya hela watakuzuga
Hata kama ni mzawa utaambiwa tu wakuja
Tafuta kwanza hela ndio mambo yote yatakuja
Ukisha toa hela na upendo ndio utakuja
Lazima utoe hela na amani ndio itakuja
Ni kweli Ma DJ nao ndio tatizo...Na ndio maana nikatowa mfano wa ZE COMEDY pamoja na kwaya kupewa msaada na RA.
Ma DJ wapewe mishahara mizuri ili haya mambo yawe ni kwa manufaa ya Taifa kwani wasanii kwa utamaduni wetu sisi ni kioo cha jamii.
Sasa unafikiri hao mafisadi hawajapenya kwa namna moja ama nyingine kujaribu kuidhibiti hiyo situation?
Ni wakati kwa wasanii kufumbua macho na wafadhili wazalendo kuwasaidia wale wasanii waliojitokeza kama hao wagosi wa kaya nk.
Hawa Ma-DJ wa Bongo njaa kali sana...wanakaa kuabudu watu muda wote na pia wamiliki wa hivi vituo vya redio nao ni tatizo. Angalia Mfano wa Clouds FM na kampuni yao nadhani ya kumiliki wasanii ya Smooth Vibes. Hawa sidhani kama awamewahi toa nyimbo ambayo si ya mapenzi na always huwa wanazifanyia promotion kuhakikisha ya kwamba zinakuwa nyimbo bora!!!
Kwa nini wasingejaribu kuwafanya hao wasanii wao wakaimba Lyrics ambazo zinaonyesha conciousness yao kwa masuala ya hapa home? Wao kutwa kucha ngono tuuu...hakuna lingine...
Safari ni ndefu and as long as watu wataendelea kuendekeza njaa zao basi sidhani kama kutakuwa na kufika!!!
Mzee there is nothing I hate in Bongo'z game kama MaDJ's.Yaani achilia mbali hawa wa Redio hizi kama Clouds na kadhalika.Kuna ndugu yangu kafanya Gospel Album kapeleka kwenye Gospel Radio station wanamwambia bila kutoa kidog kidogo nyimbo zake hazitapigwa! What a crap!!
Leo nikiwa njiani kuelekea sehemu yangu ya kuganga njaa nimepata bahati tena ya kusikia wimbo wa Mkoloni wa Wagosi wa Kaya katika Kipindi cha Power Breakfast...
Kama kuna mtu anaweza tupatia link ya hiyo track ama Lyrics zake itawa jambo jema sana...
Icla kitu kimoja ni kwamba huyu Msanii kaongea... Yale yote yanayojiri Tanzania hii kipindi hiki bila kificho wala kutumia lugha tata!!!
Wapambanaji wengine ambao wanatumia sauti zaidi kufikisha message kwa Hadhira zao wakitokea kwa kweli kutakuwa na mabadiliko. Hayatakuwa ya ghafla but eventually tutakuwa pale tunapotaka kuwa!!!
Salaam.
Jamani tunaomba basi mtu mwenye hizo lyrsics aziweke hapa na pia JF kwanini hawaziposti hizo nyimbo za hao wasanii wazalendo kwenye kitengo chetu cha muziki?
Hao watu ndio wanatakiwa wapewe msaada wa kila namna ili kuwapa moyo wasanii wengine.
Kwani si tunajuwa kuwa mafisadi wana influnce?
Sasa tunaomba hawa watu wapewe kipaumbele kwani wamejitolea,wana kipaji na pia wamekuja wakati muafaka na tuitumie nafasi na kuwapa sapoti wagozi hawa wa kaya!
NB:Mizozo hiyo power Breakfast ni kipindi cha radio stations gani?
Pole nimechelewa kurudi hapa, nilijisahau nikawa nipo tu na Thread nyengine humu Jamvini.
Power Breakfast ni kipindi cha Clouds Fm kila siku za wiki (Weekdays) kuanzia saa kumi na mbili asubuhi mpaka saa tatu. Ni kipindi kina Muelekeo kidogo lakini bado kina walakini nacho. Lakini at least ni kipindi ambacho hata habari za mafisadi na muenendo mzima wa TZ unaweza zisikia... lakini ni kutokana na magazeti yalichoandika ndio wanapata nafasi ya kufanya uchambuzi...
Issue ni habari ya gazeti gani isomwe na ipi ichambuliwe kwa kina!!!