Wasanii wa Kizazi Kipya-Jiungeni Vita Dhidi Ya Ufisadi.

Wasanii wa Kizazi Kipya-Jiungeni Vita Dhidi Ya Ufisadi.

Mmhhh, kweli JF ni ya WOTE.

Umeambiwa wanataka mashairi? na hayo wanayoimba ni nini?

Kaazi kweli kweli.

Ndio watanzania sisi.

Mkuu Fair Player...
Unaweza kututajia ni redio ngapi za hapo bongo zinapiga kibao hicho cha wagosi wa kaya na ni zipi hizo hazipigi kibao hicho na wana sababu zozote zile za kutofanya hivyo?
Na ndio maana niliomba ulete lyrics hapa ili tujuwe ni kwanini haswa wanabaniwa.
Ahsante.
 
Mashairi hayo hapo chini ni ya SONGI NINALOLIZIMIA KWA SANA TU LA LUKY DUBE..."HOUSE OF EXILE"

Freedom fighter standing on a mountain
In a foreign country
Trying to send a message
To his people, back in the ghetto
He had a home one time
Love of a girl
But he left all that behind
Oh yes I can hear him clearly as he whispers in the air
His voice came out loud and clear
All he asked for was a prayer and as he turns to walk away he said

Chorus:
I'm still here in the house of exile
For the love of the nation

Sun went down on the mountain
Birds flew back to their hiding places
Leaving him standing there like a telephone pole
In the still of the night
You and I dream
Dreaming of Romeo & Juliet
All he dreams about is the freedom of the nation
When every man will be equal In the eyes of the law
As he closes his eyes
For the last time he said again

Chorus till fade
 
Lyrics za ngoma mpya mpya ya Kizazi kipya ya TOA HELA.

Toa Hela

CHORUS

Popote ulipo au uendapo pia unachotaka fanya ujue lazima usikie hili neno: TOA HELA

JAFFARAI VERSE 1

Bro mapenzi ya bure ni hakuna kwa siku hizi
Na ukienda kwa mganga bure hakupi iko kizizi
We mchizi bora usizi usiibe wakwite mwizi
Kwani wabongo wa siku hizi wanachoma moto waizi
Mwanamme kuwa na hela ndo rijali kamili
Umeme maji ikija bill unaweza kustahimili
Kama huna mchongo si bora upige madili
Ukilemaa hata pamba si utashindwa kubadili

Toa hela upate kitu
Toa hela ongeza siku
Toa hela upate vitu hata maadui watakusifu
Kwani maisha ya sasa hivi hela ndo kila kitu
Na kama utatoa hela si hakwambii mtu kitu

AY VERSE 2

Kila kona kuna utata mtupu
Tena pale hasa huna kitu
Toa upate toa upate
Toa wakuone mtu
Si maji si kupona hata umeme luku
Hata kwa majani usipokata ujue patupuu
Toa pesa si hospitali tu
Toa si kwa vicheche tu
Cheki nikivaa/cheki nikila
Cheki nikilala ujue vyote ni pesa tu
Oh huaminiki toa pesa uaminike
Pole tusione na kitu kwetu mshike mshike
Ole nitoe pesa uibe nikushike
Toa upate kama huna usidate
Toa kamata,dakisha kata mkwanja
Bila hivyo hutopeta hututesa hutodakaa?

JAFFARAI VERSE 3

Huwezi fanya kitu chochote bila ya hela
Hata umaarufu wa siku hizi hauji bila ya hela
Bila ya hela utashindwa kufanya unachotaka
Bila ya hela hata heshima ya kwako hutaipata
Nyumbani wadogo zako hawatakwita tena kaka
Lazima utowe hela heshima ndio itakuja
Vinginevyo utasumbuka huku majasho yakikivuja
Hata ukigombea UBUNGE bila ya hela watakuzuga
Hata kama ni mzawa utaambiwa tu wakuja
Tafuta kwanza hela ndio mambo yote yatakuja
Ukisha toa hela na upendo ndio utakuja
Lazima utoe hela na amani ndio itakuja
 
Jmushi,

Hawa jamaaa kama wangekuwa wanaelewa nini maana ya kazi yao basi kwa muda huu wala wasingekuwa wanaumiza vichwa kufikiria mashairi yaani sidhani kama wanatambua moja ya dhima ya Sanaa ni Kukanya/Kukosoa maovu na kuhimiza Marekebisho hasa ya maisha ya wananchi kwa ujumla wake, wao wanachofikiria ni MAPENZI TUUUUU, UNATEGEMEA TUTAFIKA KWELI..

Mimi ndio maana Prof Jay na nyimbo zake za NDIO MZEE na wimbo wa Nakaaya naukubali sana.

Wimbo wa Nakaaya

[media]http://www.youtube.com/watch?v=KoqAmgywd80[/media]
 
Jmushi,

Hawa jamaaa kama wangekuwa wanaelewa nini maana ya kazi yao basi kwa muda huu wala wasingekuwa wanaumiza vichwa kufikiria mashairi yaani sidhani kama wanatambua moja ya dhima ya Sanaa ni Kukanya/Kukosoa maovu na kuhimiza Marekebisho hasa ya maisha ya wananchi kwa ujumla wake, wao wanachofikiria ni MAPENZI TUUUUU, UNATEGEMEA TUTAFIKA KWELI..

Mimi ndio maana Prof Jay na nyimbo zake za NDIO MZEE na wimbo wa Nakaaya naukubali sana.

Wimbo wa Nakaaya

http://www.youtube.com/watch?v=KoqAmgywd80

Kibao safi..Hata mimi nakizimia kwa sana tu...Kwani kinawapa ukweli mafisadi na kuwafumbua macho wananchi.
 
Sorry Jmushi.

I am out of this!

Asante

FP

Bila ya hela hata heshima ya kwako hutaipata
Nyumbani wadogo zako hawatakwita tena kaka
Lazima utowe hela heshima ndio itakuja
Vinginevyo utasumbuka huku majasho yakikivuja
Hata ukigombea UBUNGE bila ya hela watakuzuga
Hata kama ni mzawa utaambiwa tu wakuja

Tafuta kwanza hela ndio mambo yote yatakuja
Ukisha toa hela na upendo ndio utakuja
Lazima utoe hela na amani ndio itakuja
Hamna shida FP...Mimi niliulizia mashairi tu...Pamoja na radio zinazopiga songi hilo kwani nimelitafuta sijalipata.

Sasa naona Kevo mwenye kesha apologize pia...Ila sidhani kama mjadala hapa ni kuhusu mtu.

Hata hivyo mimi nitajenga hoja yangu taratibu tu.

Nadhani unajuwa style yangu...Thread zangu zinahitaji updates tu.

Nitamake argument ya nguvu kwani ni ukweli unaotakiwa kuwekwa wazi.

Kwa mfano kibao hicho cha Toa hela...Kina onyesha wazi kuwa jamii inaweka pesa mbele...Lakini hata hivyo maudhui ya wimbo yanaweza kuwajengea wananchi wasiokuwa na uelewa picha mbaya kwani sasa hata viongozi wakija kuomba kura watadai kupewa HELA BADALA YA SERA.

Mimi sidhani kama huo utakuwa ujumbe mzuri sana kwa jamii...Ni heri wangezungumzia kuwa sasa kila mahali ni rushwa na haki hupati bila kutowa hela...Na hata labda wangekemea kuwa hakuna maana kutowa hela wakati wa kampeni!

Watu watoe sera...To be more specific..Wasitoe sera....WAMWAGE SERA!
Ni maoni yangu kwa sasa.
 
Inasikitisha kuona kuwa Clouds FM wameweza kumuandalia ROSTAM AZIZ Press Conference lakini wanabania mipini yenye ujumbe na mashairi ya nguvu!

Clouds FM nafasi yenu ndiyo hiyo kwenye jamii?

Kusaga ndio style hizo?

Kusaga wewe unaelewa kuhusu mambo ya usanii lakini unaruhusu vipi haya mambo?

Je na wewe unajali pesa tu na hata hufikirii kuhusu kizazi kijacho?

Kuna tofauti gani kati ya kanisa la kinondoni na station yako?

Kwanini hamkumwalika na Mtikila?

Ama Mmeshachaguwa kambi?

Na vipi kama kambi yenu ikipigwa chini?

Na hao mnaowapa majukwaa kwasababu tu ya pesa zao?

Hamkujiuliza kwanini hakwenda maelezo?

Na nyie mtabaki kama kambi ya hao mnaowafagilia ikiangushwa?
 
Jmushi,

kabla sijamaliza kupitia michango yawatu wote katika hili naomba niandike yale ambayo nafahamu mimi husiana na wanamuziki wa Kizazi kipya na mchango wao katika Siasa za Tanzania.

Juu ya Ushiriki wa Wasanii wa Kizazi kipya katika hili nadhani unakuwa huwatendei haki ukisema wana ushiriki mdogo sana. Kwanza kabisa ni hawa Wagosi wa Kaya, ni jana jioni tu nikiwa katika gari nimesikia wimbo wao mpya wakikemea ufisadi. Sikufanikiwa pata jina la wimbo ila tu una mashairi makali na umetungwa kutokana na matukio ya hivi karibuni hapa Tanzania. Pia hawa jamaa naweza waita Activist maana katika nyimbo zao zote pamoja na kwamba zinatawaliwa na vichekesho vya hapa na pale lakini wako mstari wa mbele kuwekana sawa na jamii inayopotoka. Nautmaini upo familiar nao.

Pia katika wasanii wa Kizazi kipya ukimuongelea Joseph Haule (Proffessor Jay) kuanzia album yake ya kwanza mpaka ya sasa hivi nadhani amekuwa active sana katika kufuatilia siasa za nchi na kuwaweka sawa wanaokosea. Kuanzia mitafaruku ya Siasa na kujaribu kutufanya tuwe waangalifu katika kuchagua viongozi... Sikiliza kwa makini kutoka vibao kama Ndio Mzee, Album nzima ya Mapinduzi Halisi... utafahamu.

Kuna wimbo CCM na CUF wa Juma Nature nadhani umezungumzia migogoro ya siasa visiwani na ujumbe katika wimbo huu ulifikia walengwa sawia.

Katika Kampeni za 2005 ikumbukwe kuwa kuna Wasanii wa Kizazi Kipya wengi waliungana pamoja katika kumsupport Muungwana katika Kampeni zake. Kulikuwa na kina Juma Nature, Ngwair na wengineo... Jaribu kupitia Maktaba yako ya Bongo Flava nadhani utakutana na Vibao vyao. Pia kulikuwa na kibao kikali sana Cha Dr. Levy akiwashirikisha MR II na Juma Nature kinaitwa Kura Yangu.. kama ulifanikiwa kukisikiliza hicho kibao walioyaongea wasanii hao ndio haya yanayotokea sasa.... Yaani ilikuwa ni kama utabiri wa hii 'future' ambayo Watanzania tunaikabiri.

Sasa tatizo ni nini? Hapa ni kwamba tatizo lililo kubwa na ambalo linasababisha Wanamuziki wa Kizazi kipya kushindwa kuwa na mwamko wa kweli katika harakati za Vita dhidi ya Ufisadi ni kutokana na kushindwa kupata support ya kweli kutoka kwa stesheni mbali mbali za redio katika hilo. Utatoa nyimbo yenye siasa nyingi itapigwa mara moja kisha itawekwa kapuni. Najua utahoji je mbona watu kama wakina Nakaaya wanapata airtime vya kutosha na nyimbo kama hizo? Jibu ni rahisi hapo...jambo la kwanza wanalojali ni jina la msanii, anakuwa managed na nani na ni nani aliyeshika 'remote' kwa Radio Presenters kuhakikisha kwamba fulani anapata Airtime ya kutosha. Naomba nieleweke kwamba hapa sijasema kwamba kuna mtu anapendelewa but naongelea past experience na vikwazo ambavyo Wasanii wa Muziki wa Kizazi kipya walivipata walipotoa nyimbo zao kama Wanaharakati.

Wasanii wengi wanajaribu kutafuta maisha kupitia Muziki, na kwamba ukatoa nyimbo ambayo haitapata muda wa kusikika Hewani utakuwa unajiua mwenyewe kisaniii, na Redio za Bongo zinakuwa mstari wa mbele kupiga nyimbo zenye kusifia ngono, bangi na ulevi mwengine... kutokana na hilo inakuwa ni ngumu sana kwao kufikiria kutoa nyimbo hizo... Naweza nikawa nimetoka nje ya mstari lakini ndio mtazamo wa mimi kwa siku ya leo. UFISADI kila Pahala!!!
 
Mizozo,Jmushi,FP na wengine kadhalika mliochangia mjadala huu bila kumsahau mwanakijiji ambaye nitawasiliana naye hivi punde anichongee biti.Nawashukuruni kwa maoni yenu mazuri.

Nami napenda nichangie kama ifuatacyo;

1:niseme wazi kuwa wasanii wetu wengi nyumbani hawako karibu na mambo yahusuyo taifa moja kwa moja mfano mambo ya siasa.Nitakupa mfano:namfahamu Msanii mmoja aliyekuwa akisoma pale Tanzania House of Talent nilikua nimezungumza naye mambo mbali mbali,Jambo moja aliloniambia ni kuwa walihakikishiwa kabisa kuwa kama Hutoimba nyimbo ya Mapenzi Bongo kutoka inakua ni ngumu sana!! Kutokana na hali hii basi uwakilishaji wa masuala mengine kama siasa na mambo ya Ufisadi itakua ni ngumu sana.Kwa mambo kama haya basi,wasanii wetu wanajikuta wakilazimishwa kukuna vichwa na kujikita zaidi kwenye kufikiria kutoka na nyimbo za mapenzi badala ya kusukuma mawazo yao sehemu zile ambazo hazijaguswa na Muziki.

2:Muziki na Shule?: Twende mbele turudi nyuma,Elimu hata kama sio ile ya darasani;Bali ile hali ya kuwa na tabia ya kujisomea vitabu na kufuatilia habari mbalimbali zitakazomkuza mtu kiakili na kumfanya aone mambo yanayotakiwa kuwasilishwa kwa hadhira, ni kitu ambacho wasanii wetu ama wamekikosa ama hawana kabia.Kushinda baa na kukaa kwenye vijiwe bila kujipa muda wa kuangalia mambo ya kuboresha fikra kunawanya wasanii wetu waone vitu kama Ufisadi si vitu vinavyozungumkika.Wito wangu ni kwa wasanii kuona elimu kama kioo cha kukuza fikra mbadala;

Wasanii na Teknolojia:Sina uhakika mitandao ka JF na mingine mingi tuliyonayo kama inaweza kuwa na members wasanii wanaofika hata ishirini(20) kama kubashiri kunaruhusiwa.kwa hili nasema wasanii na mambo ya teknolojia ni vitu viwili vilivyo mbali kama kaskazini ilivyo mbali na kusini.Kwa hili namaanisha kuwa,Ufahamu wa mambo na uwezo wa kuona vitu kwa ukaribu unaweza kufanikishwa kwa mitandao kama hii!Lakini kwa kutokuona umuhimu wake,wasanii wetu hawajumuiki na wadau wengine katika kupata habari.Hili linawafanya wao kuwa mbali na mambo ambayo nyie mnawesemea wafanye.
 
Ni kweli Ma DJ nao ndio tatizo...Na ndio maana nikatowa mfano wa ZE COMEDY pamoja na kwaya kupewa msaada na RA.
Ma DJ wapewe mishahara mizuri ili haya mambo yawe ni kwa manufaa ya Taifa kwani wasanii kwa utamaduni wetu sisi ni kioo cha jamii.
Sasa unafikiri hao mafisadi hawajapenya kwa namna moja ama nyingine kujaribu kuidhibiti hiyo situation?
Ni wakati kwa wasanii kufumbua macho na wafadhili wazalendo kuwasaidia wale wasanii waliojitokeza kama hao wagosi wa kaya nk.

Hawa Ma-DJ wa Bongo njaa kali sana...wanakaa kuabudu watu muda wote na pia wamiliki wa hivi vituo vya redio nao ni tatizo. Angalia Mfano wa Clouds FM na kampuni yao nadhani ya kumiliki wasanii ya Smooth Vibes. Hawa sidhani kama awamewahi toa nyimbo ambayo si ya mapenzi na always huwa wanazifanyia promotion kuhakikisha ya kwamba zinakuwa nyimbo bora!!!

Kwa nini wasingejaribu kuwafanya hao wasanii wao wakaimba Lyrics ambazo zinaonyesha conciousness yao kwa masuala ya hapa home? Wao kutwa kucha ngono tuuu...hakuna lingine...

Safari ni ndefu and as long as watu wataendelea kuendekeza njaa zao basi sidhani kama kutakuwa na kufika!!!
 
Mzee there is nothing I hate in Bongo'z game kama MaDJ's.Yaani achilia mbali hawa wa Redio hizi kama Clouds na kadhalika.Kuna ndugu yangu kafanya Gospel Album kapeleka kwenye Gospel Radio station wanamwambia bila kutoa kidog kidogo nyimbo zake hazitapigwa! What a crap!!
 
Wakuu Amangk na Mzozo wa mizozo nakubaliana na nyie kwa asilimia zote 100!

Hata hapa USA ndiyo hivyo hivyo!

Unapoona HIP HOP HIVI...

Nyuma yake, wafadhili wake ni WAZUNGU NA WAMEWEKA MASHARTI KUWA WIMBO KAMA HAUNA MATUSI NA UDHALILISHAJI KWA MWANAMKE NA MTU MWEUSI.....

BASI HAUTAUZA NA WAO HAWATA UFADHILI NA KUUPIGA KWENYE TV STATIONS NA RADIOS.

Na ndio maana unaona kuwa watu kama kina KRS ONE, PUBLIC ENEMY NA KINA TALIB KWELI..MESSAGE ZAO HAZIPATI NAFASI TENA ZAIDI YA MATUSI NA UPUUZI WA KINA 50 CENT NA WENZAO!

Sasa tunahitaji message!

Kama ilivyo kwa mzungu kuwa nyuma ya Industry ya Hip hop na kuwafanya weusi kuonekana ni mashetani na wafedhuli wenye kujali madawa na ngono na udhalilishaji...Kuwajengea picha kwamba wao ni wanyama waliostahili kuwa kwenye CAGE!

Sasa Bongo ni mafisadi tena WAARABU NA WEUSI WENGINE WENYE FIKRA ZA KITUMWA!

KWANINI HAWAPIGI NGOMA ZA KIZALENDO NA BADALA YAKE WANA ANDAA ETI PRESS CONFERENCE YA FISADI?

Kwani wanafikiri yeye ni mpuuzi na hawezi kujiandalia press conference na ama hata kwenda maelezo?

Na mimi ujumbe wangu kwa CLOUDS FM...Kama kweli mmechaguwa upande wa MAFISADI MTAPATA SHIDA KAMA MAMBO YASIPOTULIA KWANI HUU NI WAKATI WA EITHER KUWA MOTO AMA BARIDI!

NO VUGU VUGU!
 
Mzee there is nothing I hate in Bongo'z game kama MaDJ's.Yaani achilia mbali hawa wa Redio hizi kama Clouds na kadhalika.Kuna ndugu yangu kafanya Gospel Album kapeleka kwenye Gospel Radio station wanamwambia bila kutoa kidog kidogo nyimbo zake hazitapigwa! What a crap!!

Hii ya watu wa Gospel nao kudai rushwa ili wapige nyimbo wanazodai ni za Mungu...!

Jamani....Nyimbo ikipigwa kwa rushwa bado ni ya Mungu?

Kivipi ujumbe wa Mungu upelekwe kwa rushwa?
Jamani!

Haya...Na kina Kusaga nao.

Wapeni ma dj mshiko wa kutosha na usiwafanye kama wao ni makenika ama deiwaka!

Sasa kwanini hakuna fees kama ni hivyo kuliko kubania miziki ya watu?

Sasa si ndio maana jamii inakuwa CORRUPT kwasababu si message inayopewa kipaumbele!?

Tusisahau kuwa ni muhimu sana kuhakikisha kuwa tunajenga society ya watu civilized maana BONGO NI VERY SHAGALA BHAGALA!

Yani hakuna tena UTU!

Sijui kwanini sisi wabongo hatukujifunza kwa wakenya ambao waliukumbatia UBEPARI TOKA MWANZO!

Tungejifunza kutoka kwao kwani licha ya uchumi wao kudaiwa kuwa uko juu lakini gap ya masikini na matajiri ni kubwa sana tu na bongo sasa hatukuzowea hilo na wananchi wanakiona cha mtema kuni!

Wakenya walishazoea na pesa kule ni kila kitu na rushwa wakati wa Baba Moi Ile JOGOO YA KENYA...RUSHWA ilikuwa ni kama chai ya asubuhi!

Na hivyo basi tuhakikishe tunajifunza kutokana na makosa na kama wimbo unakuja na ma dj wanaona hawawezi kuupiga kwasababu msanii hajatoa pesa..Basi ni muhimu waweke kabisa viwango hili ijulikane na hao wasanii wajuwe ni namna gani ya kuvifikia viwango hivyo ikiwemo pia na gharama za kuupromte nk.

Na kama msanii ni masikini na hajiwezi na huku akiwa na kipaji na kazi yake ni nzuri...Basi msisite kuleta habari na kuwatafutia watu wanaoweza kujitolea ili kuwafanikisha provided wana kipaji na message.

Na pia kwa utaratibu ninaoufahamu...Muziki mara nyingi hupata more air time kutokana na REQUEST ZA WASIKILIZAJI NA SI VINGINEVYO!

Lakini Bongo ni tofauti kwani ni more money...More air time!
Na kwahiyo hata muziki ukifa sioni ajabu.
 
Leo nikiwa njiani kuelekea sehemu yangu ya kuganga njaa nimepata bahati tena ya kusikia wimbo wa Mkoloni wa Wagosi wa Kaya katika Kipindi cha Power Breakfast...

Kama kuna mtu anaweza tupatia link ya hiyo track ama Lyrics zake itawa jambo jema sana...

Icla kitu kimoja ni kwamba huyu Msanii kaongea... Yale yote yanayojiri Tanzania hii kipindi hiki bila kificho wala kutumia lugha tata!!!

Wapambanaji wengine ambao wanatumia sauti zaidi kufikisha message kwa Hadhira zao wakitokea kwa kweli kutakuwa na mabadiliko. Hayatakuwa ya ghafla but eventually tutakuwa pale tunapotaka kuwa!!!

Salaam.
 
Jamani tunaomba basi mtu mwenye hizo lyrsics aziweke hapa na pia JF kwanini hawaziposti hizo nyimbo za hao wasanii wazalendo kwenye kitengo chetu cha muziki?

Hao watu ndio wanatakiwa wapewe msaada wa kila namna ili kuwapa moyo wasanii wengine.

Kwani si tunajuwa kuwa mafisadi wana influnce?

Sasa tunaomba hawa watu wapewe kipaumbele kwani wamejitolea,wana kipaji na pia wamekuja wakati muafaka na tuitumie nafasi na kuwapa sapoti wagozi hawa wa kaya!

NB:Mizozo hiyo power Breakfast ni kipindi cha radio stations gani?
 
Pole nimechelewa kurudi hapa, nilijisahau nikawa nipo tu na Thread nyengine humu Jamvini.

Power Breakfast ni kipindi cha Clouds Fm kila siku za wiki (Weekdays) kuanzia saa kumi na mbili asubuhi mpaka saa tatu. Ni kipindi kina Muelekeo kidogo lakini bado kina walakini nacho. Lakini at least ni kipindi ambacho hata habari za mafisadi na muenendo mzima wa TZ unaweza zisikia... lakini ni kutokana na magazeti yalichoandika ndio wanapata nafasi ya kufanya uchambuzi...

Issue ni habari ya gazeti gani isomwe na ipi ichambuliwe kwa kina!!!
 
Jmush1
Mdogo wangu siku zote mimi huzikubali fikra zako kwa % 100, ila usisahau hapa home hawa mafisadi wakikusikia basi umeimba wimbo wa kuwa kinyeme na wao basi hapo utatafutiwa kesi, na kama haitoshi kama una kausafiri kako utapata matatizo hadi ukome,
nadhani kuna kila sababu sasa mrudi home tupigane sote, hii vita ni ngumu,usisahau tunacheza mpira huku tukiwa pekupeku.
 
Pole nimechelewa kurudi hapa, nilijisahau nikawa nipo tu na Thread nyengine humu Jamvini.

Power Breakfast ni kipindi cha Clouds Fm kila siku za wiki (Weekdays) kuanzia saa kumi na mbili asubuhi mpaka saa tatu. Ni kipindi kina Muelekeo kidogo lakini bado kina walakini nacho. Lakini at least ni kipindi ambacho hata habari za mafisadi na muenendo mzima wa TZ unaweza zisikia... lakini ni kutokana na magazeti yalichoandika ndio wanapata nafasi ya kufanya uchambuzi...

Issue ni habari ya gazeti gani isomwe na ipi ichambuliwe kwa kina!!!

Nina hamu sana ya kuwasikia wagosi hao wa Kaya na pia kuona hayo mashairi yao!
Maana kwa kweli mimi hupenda sana mipini yenye message.
Pia kama ni clouds basi ni habari zenye matumaini kwani sasa tuna starting point...Na pia clouds kama ni ya mzalendo mwenye uchungu na nchi yetu basi iwape mambo wananchi ili washiriki kikamilifu kwenye vita ya rushwa kwani vita hii kama sisi wenyewe wananchi hatutashiriki itakuwa ni kama Isaya Mwita alivyosema kuwa tunacheza peku peku...Na mimi ninasema kuwa itakuwa ni sawa na kumlazimisha mlevi mbwa avae kondom.
 
Back
Top Bottom