Dogo janja..
Aslay
Mboso
Mwana fa
Jux
Nedy music
Billnass
Baraka de Prince
Whozu
Masanja
Baba diamond
Hamisa
Na wengine wengi..ningekuwa DJ kwenye radio station nyimbo zao ningekuwa naziweka kwenye ndoo ya uchafu..
Nyimbo zao nyingi ni za kuanzia SAA 12 asubuhi hadi 12 jioni..zinakuwa zimeshaboaaa..nyimbo zao hazina uhai..hazivutiii..ubunifu zerooo...hazifai hata kucheza high club.
Naona wengi wenu mnashindwa kutofautisha kuimba na kurap/kuchana
Sasa kama wewe umemuweka Mwana FA kwenye list yako eti aache kuimba hv huyo anaimba au anachana?
Ungemtaja King Crazy GK wa East cost Team hapo sawa, maana yule aliimba kwenye wimbo wake mmoja hivi unaitwa Baraka au Laana kamshirikisha Yuzo ila verse ya mwisho alichana
Sasa vuta picha GK na ule uongeaji wake (sijui ni kigugumizi au nini) kisha aimbe
N.B;
Kama unajijua hupendi nyimbo za kuchana au kurap, mtuachie sisi hao wasanii ndo tunaowajua maana wengi wenu mmeanza kufuatilia Bongo fleva baada ya Diamond kujulikana
Sisi tulioanza enzi zile unaitwa muziki wa kihuni hakukuwa na msanii anayeimba wote walikuwa wanachana/wanarap huku mwasisi wao akiwa Mr.II a.k.a. Sugu
Kama yupo aliyekuwa anaimba naomba uniwekee hapa na moja ya wimbo wake
Asiwe msanii wa injili tu kama Malebo Munishi
Em tafuta ngoma za Mr.II zinazopatikana kwenye albamu yake ya kwanza inayoitwa Ni Mimi ya mwaka 1995, hii imerekodiwa katika studio za redio Tanzania uone jamaa alivyopangilia vina na mashairi yalivyo kwenye mpangilio mzuri