Wasanii wanaodaiwa kutumia madawa ya kulevya, ni yupi anayekusikitisha?

Kama ni kweli Vanessa Mdee anatumia hizi vitu basi atanisikitisha kuliko wote, nilikuwa namkubali sana na nilivyokuwa namchukulia ni tofauti na wasanii wengine wa kike, sikuwahi kumfikiria anaweza kuwa kwenye huo upande. But lisemwalo lipo....
Usiamini kila kitu cha humu, kuna mengine Ni kweli na mengine ni kuchafuana. Nilichogundua kila mwenye mwili Mdogo au mwembamba basi anahususishwa moja kwa kina na matumizi ya unga hata yupo hivyo toka mwanzo.
 
Usiamini kila kitu cha humu, kuna mengine Ni kweli na mengine ni kuchafuana. Nilichogundua kila mwenye mwili Mdogo au mwembamba basi anahususishwa moja kwa kina na matumizi ya unga hata yupo hivyo toka mwanzo.
Ni kweli siwezi kuamini moja kwa moja, ila naweza kuamini kwa 70%, kwavile mambo mengi ya mastaa kwenye jukwaa hili huwa yanakuja kugundulika baadae kwamba ni kweli, ingawa mwanzoni watu huwa wanapinga sana
 
Maisha ni magum sana afu yanastress sana ukizingatia mtu ni maarufu afu hana mkwanza inabidi ajidozishe
 
1. DAZ BABA
2. CHID BENZ
3. RAY C
4. LOD EYEZ
5. M.R NICE.
6. ROSE MHANDO
7. TID-MNYAMA
8. RACHEL
9. FEROUZ
10.BEN PAUL



*NOTE*
We give very high respect to P FUNK (MAJANI) and Q-CHIEF because they have stopped permanent to use drugs.

Magufuli OKOA VIJANA HAWA.
 
Dears kwani na Mr nice? Mimi najua yeye ni mwalukanga sio vumbi
 
Tatizo la madawa ya kulevya ni kubwa mno kuliko tunavyoweza kufikiri. Kwanza uvutaji wa bangi siku hizi hata sio tatizo tena ni kama jambo la kawaida tu. Hao wa unga ndio janga linguine, umaarufu au kufahamika kwa hawa vijana ndio kufanya watu wajue kwamba wanatumia lakini kuna wimbi kubwa sana kuanzia mtaani, mashuleni, maofisini na kila eneo la watu wanaotumia madawa ya kulevya, athari ni kubwa mno kwa taifa.
 
then what?!

Kwa nini uwanyooshee vidole

Hawa ni watu kama sisi
 
wanahitaji msaada wa hali na mali.. rachel nasikia amechanganyikiwa yupo south africa na ben paul ndio alianza last year ni hatari sana kwa afya
 
Nimestuka nilipoliona hilo jina no. 10, dah hata wewe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…